Credit
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 1,490
- 1,881
Mpenzi wangu niliyempenda sana aliniambia nimempa mimba. Akapima nikathibitisha kuwa ana mimba. Nilimwahidi kulea hiyo mimba, nilimwambia uwezo, sababu na nia ya kulea hiyo mimba NINAZO. Baada ya mwezi mmoja tu aliitoa ile mimba. Niliumia sana, nilijuta sana, nililia sana. Sikuwahi kulia kabla lakini niliililia ile mimba. Hadi leo nikikumbuka machozi hunitoka.