Hataki kuzaa kabla ya ndoa

Teh, asikudanganye mtu hakuna kanuni maalum ya mtu kuoa au kuolewa.

Njia ulizotumia wewe sizo alizotumia au atakazotumia mwingine, ndiyo maisha.
Tatizo binadamu wanataka ndoa ya makaratasi na sio ndoa ya upendo
 
kama atakuwa hazai , gegeda beki tatu manake huwa wanashika mimba chap
 
'Mimi sina wazo baya, wala sitaki kumfanyia uhuni wa kumzalisha na kumkimbia, mimi sina mwanamke mwingine zaidi yake ila wasiwasi wangu ni uzazi.'

Ushauri ni mmoja tuu...

muoe binti wa watu... mengine mauchie Mungu, wewe siyo muumbaji...



Cc: mahondaw
 
Nampongeza huyo mdada, anajua uhuni wa wanaume, unaweza kujidai innocent na baada kumpa mimba ukabadilika.

Historia "mbaya" ya familia yake pia inafanya asiweze kukukubalia, hata ingekuwa mimi nisingekubali, single parenting ina changamoto nyingi mno. Waulize walioko humu watakuambia.

She's right!!!
 
Kabla ya yote, Karibu sana jamii foram, naona umejiunga leo asubuhi.

Mleta Mada chukua huu uchauri,na cha zaidi basi mnaweza kwenda hospital kupima nani ana tatizo au ukampime Yeye kama ana huo ugumba au la, ila cha luzingatia Watoto ni majaliwa japo amefanya kosa kitoa mimba hongera umemsamehe lakini, huyo binti ameonja uchungu wa single mother so hapendi kurudia mwelewe na me namsurpport huyo binti na usimuuzi au kumlazimisha ana uchungu na hapendi kufanya makosa Kama ya familia yake.

Kontoro@
pujo
financial services

Karibuni jamani Wapendwa mseme machache.
 
Kwahiyo ukigundua kuwa hawezi kuzaa ina maana hautamuoa ??

We muoe tu akishindwa kuzaa basi mtazaa kupitia surrogate mother !!
Mkuu naomba kufahamu kuhusu surrogate mother tafadhali, naona itakuwa suluhisho kwangu.
 
Ooh unahitaji kujua maana yake au jinsi wanavyopatikana
Daah yani hata sielewi mkuu kuna hali napitia ngumu sana nimeona sehemu umeandika kwamba kama hatakuwa na uwezo kuzaa watatumia hyo nikajikuta natamani kujua kila kitu kuhusu hicho kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…