Nangu Nyau
JF-Expert Member
- Jul 1, 2022
- 5,015
- 14,139
Moja kwa moja kwenye hoja.
Ni wakati sasa wa kuangalia kwa jicho kali ulinzi wa ajira za vijana wa Kitanzania na Watanzania kwa ujumla.
Milango tulioifungua kwa kuruhusu wageni kuingia na kupata ajira kwa hoja ya kadili muwekezaji aonavyo inaanza kuwa hatari kwa ajira za wazawa na mustakabali wa wasomi wa kitanzania.
Hali imeaanza kuwa mbaya mitaani kwa ajira nyingi kupewa wageni sasa hata pale ambako hapastahili.
Serikali inapaswa kuweka jicho kali sasa ili kulinda ajira za wazawa, Waajiri wengi sasa wameanza kuleta wageni hasa indians kutoka India kwa kazi ambazo watanzania wanaweza kuzifanya.
Kenyans, Ugandans nao hawako nyuma wamechangamkia fursa hiyo hasa makampuni ambayo ni mali ya wakenya na waganda. Wahindi wameanza kumiminika kwa wingi saana, na makampuni ya kihindi yanatoa priority kwa indians wenzao bila kujali wako ardhi yenye watu pia.
Kwenye constructions na mining pia kumekuwa na hii changamoto kwa sasa kwa expert wengi kuletwa kwa kigezo cha wazawa hakuna, hata kwa zile kazi ambazo unaweza kufundisha mtu ndani ya mwezi akazifanya au ukapromote mtu ndani ya organization husika.
Upande wa biashara, wageni wanaachwa kuingia ndani kabisa huko kufuata bidhaa za kilimo na kufanya biashara nyinginezo ambazo wazawa wanapaswa kufanya, mkenya hapaswi kufuata parachichi Njombe au nanasi bagamoyo bali ni mtanzania anapaswa kupeleka Kenya au Mkenya asubiri border kwenye soko.
Mchina hapaswi kuwa na duka kariakoo bali ni mtanzania anapaswa kuagiza bidhaa china na kuleta hapa, Mturuki hapaswi kuwa na duka kariakoo bali mtanzania anapaswa kuagiza bidhaa na kuzileta hapa.
Tusipolinda ajira za vijana wetu basi kuna hatari ya vijana wetu kuwa watumwa na wapagazi ndani ya ardhi yao, Jicho kali sana linahitajika hapa na watanzania tuwe wazalendo sasa kulinda ajira za wenzetu hata kama sisi tuna nafasi ya kuishi.
Kenya huwezi kupeleka bidhaa hovyohovyo kwenye masoko yao kama sio mkenya, Kenya huwezi mtanzania kuomba ajira ukapata kirahisirahisi. Kenya ni mfano tu katika mifano mingi katika nchi nyinginezo kama West Africa.