Hatari, nimeongea na Ex-Wangu, nimejisikia vizuri sana

Hatari, nimeongea na Ex-Wangu, nimejisikia vizuri sana

Wakuu, haya maisha yanafunzo.

Niliwahi kuwa na mahusiano na binti mmoja tukapata mtoto mmoja, maisha yakatuchanganya, tukaachana, Kila mtu akaendelea na Maisha yake!

Mtoto aliniachia mawasiliano kumhusu yalibakia kati yake na Mama yangu na alivyofika darasa la 6 nikampeleka Boarding.

Nikaoa, sikujua habari zake tena.

Leo nikakutana na ka diary mahali, nikafungua kujua kinahusu nini, ni cha binti yangu! na nilipofungua macho yangu yalikutana moja kwa moja na namba ya Mama yake.

Sijaonana naye almost 12years now!
Nikapata msukumo kutoka ndani yangu kujaribu kumpigia, as ilikuwa mchana nikajua atakuwa katika mazingira ya kazi.

Nilivyopiga ile namba haikupokelewa, na baada ya dakika kama 10 ikanipigia.
Nilimsalimia tu akanitambua! Alizungumza na mimi kwa heshima sana na kwa sauti ya upole.

Nikatamani kujua status yake, ameshaolewa with two kids.
Yeye anajua kuhusu mimi via my daughter wanawasiliana.
Basi tukapongezana pale na kuagana.

Nimejisikia vizuri mno, nimeona hii ni platform yakushare ninavyojisikia

Natamani sana kumwona tena!

Muhusika anaweza kuona pia, natamani ajue

Sijui nafanyaje hapa wadau...
Wewe ni mharibifu na nia a yako ni ovu.
 
Nyege zinakusumbua
 
Yes ni hivyo ila sidhani kama mna huo uwezo wa kutukataa vile mpo cheapest.

As for now ni ngumu mno kwa mwanaume kutafuta mbwa wa kumfuga inaweza kumchukua muda na pesa nyingi lkn mwanamke wa kumuoa ni rahisi mno hata kama unaishi jalalani atakuja naye muanze nae maisha mkiwa hapo.
Mkuu siyo kweli. Hakuna kazi ngumu kama kutafuta mwanamke wa kuoa hasa siku hizi. Labda kama unatafuta tu mwanamke wa aina yo yote ali mradi tu mwanamke. Na hapo utaishia kupata mafurushi yasiyojitambua; na ambayo yako desperate ali mradi tu yapate ndoa ili kuondoa nuksi na kujionyesha kwa watu.

Lakini kama unatafuta mwanamke wife material mwenye angalau vigezo vichache ulivyojiwekea kwa matarajio ya kuja kuwa na familia bora kwa ajili ya wanao na wakati ujao ulio mwema aisee ni shughuli pevu. Jaribu uone!
 
Mkuu siyo kweli. Hakuna kazi ngumu kama kutafuta mwanamke wa kuoa hasa siku hizi. Labda kama unatafuta tu mwanamke wa aina yo yote ali mradi tu mwanamke. Na hapo utapata mafurushi yasiyojitambua au ambaye yuko desperate ali mradi tu apate ndoa.

Lakini kama unatafuta mwanamke wife material mwenye angalau vigezo vichache ulivyojiwekea kwa ajili ya kuja kuwa na familia bora kwa ajili ya wanenu aisee ni shughuli pevu.
Comment iwekewe lamination hii [emoji419]
 
Mkuu unanionea tu!
Mtoto tumekuwa nae sisi throughout.

Nimemlea binti yangu mwenyewe, Mama yangu/mke wangu wa sasa wangekuwa na uwezo wakumficha mtoto, wala asingekaa ajue Mama yake ni nani. Alimwacha akiwa mdogo sanaa...

Ni huruma ya Mama yangu tu
This is exactly why huna akili.... After 12 years za kulea mtoto wenyewe kinachokuwasha wewe ni nini?
Kwa mkeo hujisikii vizuri enough?
 
Yaani Jamaa eti anashangaa kwanini wajumbe wanamtupia Mawe [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ana tabia chafu....
Hana huruma kwa mkewe wala mume wa mzazi mwenzie.
Sababu likitokea la kutoka chances are mkewe yeye hawezi kumuacha, ila mwenzie ataachika.

Binafsi ningekua ni huyo dada, ningempa mume wangu namba yake ili next time aongee na mimi kupitia yeye kama kuna jambo la muhimu.
 
Pole bro , nahisi unacho kihisi maana nami iliwahi kujikuta hali kama yako, unaweza kuhukumiwa hapa na wadau lakini najua hauna dhamira mbaya dhidi yake , ila tu kuna hali fulani inakupata hamna namna unaweza kueleza ukaeleweka, tena wewe mlifika mbali hadi kuwa na mtoto, mimi sikua na mtoto naye ila nilipoongea nae mara ya kwanza baada ya kuachana kwa miaka kumi ilinitokea kama wewe.

Upendo wa kweli haufi aisee, kama kuna sababu ndogo ya kuachana usiachane na mpenzi wako.

Pia mwanaume ndie anaye penda na pendo huanzia moyoni, inapotokea pendo lile kuharibika moyo ama nafsi haikubali , hutengeneza kitu kisicho futika daima.

Yote ya yote bro Linda mahusiano yake na yako pia .
Umalaya unaanziaga ndani. Hamu zote za kimalaya malaya zinakuja kama hisia, unajisikia umalaya malaya unadhani sijui ni real love.

Yaani mtu ushindwe kujisikia upendo kwa mume/mke anayekuombea hapo miaka na miaka ukajisikie upendo kwa mtu mliyeachana miaka 12 iliyopita?

Huko ni kujisikia umalaya na mwisho wake huwa ni majuto ndani yako iwapo mtakutana na mkajikuta mmefanya ngono.
 
Yaani roho yako haiwezi kutulia mpaka ukutane nae, amini nakuambia ukishakutana nae lazima utapasha kiporo na mapenzi yatachanua.............baada ya mambo yote hayo unajua kitafuata nini??
Sio mchezo kabisa!!
 
Back
Top Bottom