Hatari, nimeongea na Ex-Wangu, nimejisikia vizuri sana

Ushafikiria kumla kisa TU uliwahi kupita naye na mkazaa naye mtoto, basi unahisi una haki ya kumuomba game na hatokukatalia.
Na hisia umezileta baada ya kukujibu kistaarabu, sisi wanaume kurogwa na kufa kupo karibu mnoooooooo, mwenzako anaweza kuwa amekutunza kwa sababu anajua udhaifu wa mwanaume ni kumpa K au ukimnyima K akili yake umeivuruga.

Huyo ni mke wa mtu na zaidi ulimzalisha na hukumuoa hujui amekutunzia kisasi gani?
 
Ni kweli, lakini yeye ndio ameanza kunitengenezea mazingira
 
ninachopea kujua, amefanikiwaje kuishi na mtoto nje ya mama yake kwa miaka 12 na bila kuwasiliana na mama wa mtoto, na, roho ya mama wa mtoto ipoje, ngumu kiasi gani kumwacha mtoto kwa mwanaume 12 years, huyo sio mwanamke halisi hata kwenye hiyo ndoa anayoishi nayo mwanaume wake awe makini anaishi na mwanadamu mwenye roho ngumu sana.

kuhusu mawasiliano, wengi tu hapa tuna watoto wa kambo, kabla hatujaokoka tulikuwa wazinzi. huwa tunawasiliana na mama watoto wetu na tunatuma matumizi na kuna wakati tunapanga kikao kwenda kukutana na watoto wetu, meaning mama mtoto atakuja na mwanae au nitaenda sehemu salama kama kwa ndugu zake tukakutanie hapo hasa wale wenye waume, nikaongea na kucheza na mtoto. ila kuna mipaka, tunakwepa mazingira ya kuharibiana kila mtu ndoa yake, tunakwepa mazingira ya kutuweka sisi wawili tu pamoja bila mtu mwingine manake la sivyo mtazini, mazingira ya urafiki marufuku manake mkianza kuongea friendly mara utani n.k mtazini, mawasiliano yenu ni salamu, mtoto anaendelaje, mahitaji ya mtoto, naomba kuonana na mtoto n.k. hii ni kuheshimu pia mahusiano yake kule aliko na kuepuka usitende dhambi tena.

all in all, nawaasa, wanaume wenzangu ambao hamjaoa, jitahidi mwanamke atakayekuzalia awe ndio yule uliyemwoa, mtoto wa kambo anatunzwa kwa shida sana na hakuna uhuru wa kujumuika naye kama wazazi hamuishi pamoja. epukeni icho kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…