ndenga
JF-Expert Member
- Dec 20, 2010
- 1,824
- 1,427
Kwa muda sasa kumekuwa na kundi kubwa la vijana wanaolala barabarani kama makazi yao ya kuishi maeneo ya Barabara ya Sam Nujoma kuingia Sinza Makaburini. Idadi ya vijana hawa imekuwa kubwa na wanakuwa wamelala mpaka hata saa mbili asubuhi bila kuamka kuonyesha kwamba usiku mzima wamekuwa wakikesha. Kuna haja serikali kuangalia hili swala. Maana mwisho wa siku vijana hawa wamejichukulia sheria na kuhamia hili eneo na wanaweza kuwa mwanzo wa vibaka katika maeneo husika. Wengi wao ni vijana wenye nguvu ya kufanya kazi na kuweza kujipatia kipato. Ni hatari kwa usalama wao pale gari linaweza kufeli break na kuwagonga na husababisha hatari na vifo.
Naomba Mkuu wetu wa Mkoa Uliangalie hili: To: Polisi CC: Mh Chalamila
Naomba Mkuu wetu wa Mkoa Uliangalie hili: To: Polisi CC: Mh Chalamila