Hatari ya Kundi Kubwa la Vijana wanaolala Barabarani Sam Nujoma/Sinza Waangaliwe

Hatari ya Kundi Kubwa la Vijana wanaolala Barabarani Sam Nujoma/Sinza Waangaliwe

Dah hali sio nzuri hiyo ni mbaya sana, ni ongezeko la umasikini kiasi
kwamba mtu anakosa kipato cha kupanga chumba.
 
Dah hali sio nzuri hiyo ni mbaya sana, ni ongezeko la umasikini kiasi
kwamba mtu anakosa kipato cha kupanga chumba.
Na itazidi kuwa mbaya ,kadiri siku zinavyoenda njia za kujipatia kipato zinapozidi kuwa finyu kwa mwananchi wa kawaida nchi hii
 
Kwa muda sasa kumekuwa na kundi kubwa la vijana wanaolala barabarani kama makazi yao ya kuishi maeneo ya Barabara ya Sam Nujoma kuingia Sinza Makaburini. Idadi ya vijana hawa imekuwa kubwa na wanakuwa wamelala mpaka hata saa mbili asubuhi bila kuamka kuonyesha kwamba usiku mzima wamekuwa wakikesha. Kuna haja serikali kuangalia hili swala. Maana mwisho wa siku vijana hawa wamejichukulia sheria na kuhamia hili eneo na wanaweza kuwa mwanzo wa vibaka katika maeneo husika. Wengi wao ni vijana wenye nguvu ya kufanya kazi na kuweza kujipatia kipato. Ni hatari kwa usalama wao pale gari linaweza kufeli break na kuwagonga na husababisha hatari na vifo.
Naomba Mkuu wetu wa Mkoa Uliangalie hili: To: Polisi CC: Mh Chalamila
Muache ukatili majumbani.
 
Mtoa mada upo sahihi. Kazi kubwa wanayofanya ni kufuta futa magari na vitambaa wakati watu wakisubiri taa ziwaruhusu kupita

Pia La kuongezea tu, wale watoto/vijana ni walevi wa pombe na madawa ya kulevya.

Hatua stahiki zinapaswa kuchukuliwa haraka, la sivyo hawa watakuja kuwa sehemu ya wateja wa Ant robbery unit.
 
Kina idadi kubwa ya vijana wanalala stendi, kwenye corridor za maduka, kwenye fremu, kwenye daladala zilizopaki, kwenye makanisa, kwenye misikito, kwenye mastoo n.k
dah huwa nawaonea huruma hawa jamaa, pale uhuru shure ya wasichana hutandikwa viboko na maafande wakichelewa kuamka halooo[emoji1787][emoji1787]

Hii kitu ipo hata Kenya Nairobi na Mombasa wale watoto na vijana wala gundi aisee[emoji848]
 
Hili ni bomu!! Hao watageuka kuwa wanakaba watu na wezi! Tunaomba wakamatwe wote! Sio sawa watu kulala mabarabarani
Ni sawa kukamatwa wote. Je, umewahi fikiri ni kina nani wanaolala? Je, ni mateja wala unga, walala hoi au vibaka, au maskini akina kabwela au ni timamu waliotelekezwa makwao au kufukuzwa kwa kukandamizwa haki zao?

SIO KILA CHOKORAA MTAANI NI CHOKORAA KWELI. WENGINE WAMEUMIZWA NA WAZAZI AMA NDUGU WAKAKOSA PA KWENDA YAANI DUNIA YOTE KWAO HAINA MAANA KWA WAKATI HUO..

TUWAKAMATE TUWAPELEKE VITUO VYA AKILI NA MENGINEO KUFUATA like MISAADA, USHAURI N.K
 
Wabongo si hua wanasema hamna tatizo la homelessness Tanzania ? , Sasa na hao wanalala kwenye mitaro ,macaravat ,madaraja na vibaraza vya fremu na nyumba za watu tuwaiteje ?
Wengi wanao lala nje ni foreigner hasa kutoka Burundi na Congo!!
 
Mtu analala katikati ya Barabara mpaka saa mbili na nusu. Jua kali linawaka kabisa na mtu yuko usingizini je angekuwa nyumbani tena kwenye AC angeamka saa ngapi.
Ndiyo ujue Mungu ni mwaminifu, huwapa watu wake ulinzi, usingizi mzuri. Kuna watu wapo kwenye majumba ya kifahari wanavitanda vya thamani kubwa, ulinzi nje mkali. Lakini nakuhakikishia unaweza kuta hawapati usingizi mzuri kama wanaopata hao vijana wanaolala nje barabarani. Mungu huyu wa ajabu sana.
 
Ni vizuri mkaawafanyia mahojiano wale ambao ni wazima nikimaanisha ambao Akili haijapata break down wapatiwe ushauri na kuelekezea nini wafanye kuondokana na hiyo hali ya kuwa homeless.

Na Ambao wemedata kutokana na pombe , bangi na madawa wapelekwe sober house au (Rehab)

Acheni kuwa na fikra Mgando za kutumia nguvu kila sehemu mpaka MTU analala nje unabidi kujua something is wrong in his or her mind .

Take time to think is the source of power
 
Back
Top Bottom