Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
HANANG'
Jumla ya hati miliki 266 za viwanja na mashamba zimetolewa kwa wananchi wa Kata ya Dawar mkoani Manyara.
Hati hizo zimetolewa Oktoba 8, 2026 na Mkuu wa Wilaya ya Hanang’, aliyekuwa Mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi hati hizo Mhe. Vita Rashid Kawawa, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (KKK).
Akizungumza katika hafla hiyo, mhe. Kawawa amesisitiza umuhimu wa wananchi kumiliki maeneo kwa hati ili kulinda haki zao, kuimarisha usalama wa milki pamoja na kupunguza migogoro ya ardhi.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Ardhi mkoa wa Manyara Bw. Erick Mbeya akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa huo amesema, malengo ya Ofisi ya Ardhi ni kupima mashamba 3,000 katika kata ya Dawar, vijiji vya Dawar, Kinyamburi pamoja na Gasaboy ili kuwawezesha wananchi kupata nyaraka rasmi za umiliki.
Amesema, hatua zilizofikiwa mpaka sasa za malengo hayo ni pamoja na kutoa elimu ya upimaji, kuandaa mpango wa matumizi bora ya Ardhi ya kijiji, kutambua mipaka na kuhakiki taarifa za wamiliki.
Aidha, amesema mchato wa kuandaa na kusajili hati za kimila, zitakazosaidia kutambua na kulinda milki za wananchi kwa mujibu wa taratibu husika umefanyika.
Hafla ya kukabidhi hati milki za viwanja na mashamba imehudhuriwa na wananchi kutoka vijiji vya Dawar, Gasaboy, Kinyamburi, Masakta, Bassotu, Nangwa na Mogitu, pamoja na madiwani na viongozi wa dini.