Kagosi DJ
Member
- May 5, 2020
- 19
- 69
Tuanze na swala la uanachama, ICC ni mahakama ya kimataifa inayoshughulikia makosa ya kivita(War crime), uharifu dhidi ya binadamu( Crime against humanity), Mauaji ya Kimbali (Genocide) na Uvamizi (Act of Agression) Mahakama hii ilianzishwa Julai 1, 2002 huku ikiwa na wanachama 60 kufuatia Mkataba wa Roma wa Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (Rome Statute) wa mwaka 1998. Baadhi ya mataifa ambayo hayakukubali kuwa wanachama wa Mahakama hii ni Marekani, China, Iran, Israel, Qatar, na Libya.
Urusi ilisaini mkataba wa ‘Rome statute’ lakini haikuwahi kuthibitisha ‘ratify’ ili kuwa mwanachama halali hadi mwaka 2016 ilipojitoa rasmi kwenye mkataba huo. Kwa upande wa Ukraine haikuwahi kuwa mwanachama. Hapo unaweza kujiuliza imekuwaje ICC iingilie kati mgogoro kati ya mataifa ambayo sio wanachama wake? Ipo hivi kwenye mkataba wa kuanziswa kwa Mahakama hii ya Kimataifa Kifungu cha 87(5) kinaelezea ushirikiano kwa mataifa yasiyo wanachama wa ICC. Kifungu hicho Kinabainisha kwamba Mahakama ‘’inaweza kualika Nchi yoyote isiyohusika na Mkataba huu kutoa msaada chini ya Sehemu hii kwa misingi ya mpangilio wa dharura au kwa makubaliano na Nchi hiyo au misingi yoyote inayofaa. Hivyo Ukraine pamoja na kutokuwa mwanachama imetumia nafasi hiyo kutoa ushahidi dhidi ya Putin kuhusu makosa ya kivita na uhamishaji haramu wa binadamu (hasa watoto).
Swali la mihimu ni je Putin atakamatwa baada ya hati ya kukamatwa kwake kutolewa na ICC?
Tunapaswa kujua kwamba ICC haina nguvu ya dora kama jeshi na Polisi hivyo hutumia wanachama wake kukamata waarifu na kuwapeleka mbele ya Mahakama (Baada ya Hati ya kukamatwa kwa muharifu kutolewa kama mtu huyo ni raia wa nchi isiyo mwanachama wa ICC atasubiliwa hadi atakapo toka nje ya nchi yake na kutembelea nchi mwanachama wa ICC Inchi hiyo iliyotembelewa ndiyo inaweza kumkamata ingawa swala hili sio la lazoma kwa nchi husika)
Raisi wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir alitolewa hati kama hii mwaka 2009 wakati akiwa bado madarakani na alitembelea nchi kadhaa wanachama wa ICC bila kukamatwa licha ya ICC katika Mkataba wake kutotambua ‘Immunity’ kwa viongozi wa nchi.
Swala la kukamatwa kwa Raisi wa nchi flani tena akiwa ziarani katika nchi nyingine ni gumu kutokana na makubaliano mengi ya kidiplomasia kabla ya Ziara ya kiongozi wa nchi katika nchi nyingine hivyo swala la Putin kukamatwa ni ndoto ambayo ni ngumu sana kutimia tena pengine haitotimia.