Hati ya kukamatwa kwa Rais Vladimir Putin: Je, utaratibu upoje?

Hati ya kukamatwa kwa Rais Vladimir Putin: Je, utaratibu upoje?

Wa Iran na North Korea wenyewe wamechoka na nchi zao aende kufanya nini tunazungumzia nchi zenye ushawishi duniani nchi za Ulaya na US., hata wewe ukifungiwa usiende uganda unahisi italeta athari gani, naongelea nchi zenye ushawishi kiuchumi ulimwenguni putin hatakakanyaga atafia Kremlin
China anaenda freshi tu
 
Akikamatwa Dmitry atatuma kombora la nuclear kwa nchi iliyomkata, ana roho ngumu kuliko Putin
Nashangaa hawa jamaa wanaohisi kwamba Putin watamfanyia upuuzi kirahisi rahisi tu.
 
Sasa nimeelewa MWAMBA humaanisha nini kwa kundi fulani la hapa kwetu.

Kumbe wakisema MWAMBA wanamaanisha MUUAJI. Putin ameondoa maelfu ya roho za watu wasio na hatia. Huo ndiyo umwamba ambao shetani na watu wake wanausifia.
Putin anaunganisha dunia kwa sasa, we endelea kugawa mataco kama mabosi zako NATO wanavyowahimiza.
 
Vipi kuhusu majemedari wema wanaotofautiana na Putini ndani ya Urusi, unafkiri hawatakuwa na namna na kutoa mashirikiano kukamatwa ama kumpeleka Putin mbele ya ICC?

Unafkiria anayofanya putin yanawafurahisha wote urusi? ni suala muda lakini madam Warrant imetoka na namna ya kumkamata tayari ipo kwenye malengo sasa wacha jamaa aishi na khofu kwanza
Mmemshindwa kwenye uwanja wa vita mmeamua mtafute mahakama ya mchongo mumsakizie kesi?
NATO wapumbavu sana wanataka ushindi wa Mezani na ambao Putin hatakaa akubali kuwapa.
 
Ceremonial? Unaota hiyo hati ya ICC ina nguvu mno hata kwa wapinzani wake ndani ya Chama chake, ndani ya Jeshi na ndani ya vyama vya upinzani Russia kupata nguvu kuwa wana support ya kimataifa wakiamua kushughulika na mhalifu wa kivita Putin

Ina maana makundi yote ya upinzani dhidi ya Putin Russia wanaruhusiwa kuomba misaada ya kimataifa ya lumuondoa Putin madarakani na watapewa

Sababu jumuiya ya kimataifa inamtambua kama criminal

Hivyo yeyote Russia anayehitaji msaada wa fedha, silaha au logistics za kumpindua Putin,kumuua au kumkamata kumpeleka the Hague ana support ya kimataifa
Hiyo warrant ni go ahead document kwa wapinzani wote wa Putin kuwa jumuiya ya kimataifa iko nanyi ku deal na huyo criminal

Wameupa nguvu upinzani Russia kuwa jumuiya ya kimataifa iko nao

Ni wao tu kusema nini kinatakiwa kummaliza mhalifu Putin wapewe msaada
Nadhani huko the Hague mngeanza kuishitakia CCM maana kuna kundi flani hawaikubali wala nn
 
Hivi wewe unawaza Kwa kiungo gani? anyway JF inatoa Uhuru Kwa kujieleza Kwa kila mtu.
Wewe ndo Bure kabisa,Arrest Warrant hutolewa na competent court yenye jurisdiction Kwa nchi Husika,nambie ICC legal basis ya ICC kutoa hiyo Arrest Warrant ni ipi wakati Urusi haja-ratify mkataba uliounda ICC as per requirement of Public International Law,zaidi ya kuwa ceremonial?otherwise,umeamua kutumia your freedom of expression kushabikia mashoga wa nchi za magharibi
 
View attachment 2556122
Baada ya kutolewa kwa Hati ya kukamatwa kwa rais wa Urusi Vladimir Putin watu wengi wamekuwa na shahuku ya kujua hati hii itafanyaje kazi? Na je raisi huyu anawezaje kukamatwa huku akiwa madarakani tena nchi yake (Urusi) pamoja na nchi aliyotuhumiwa kuifanyia uharifu (Ukraine) zikiwa sio wanachama wa ICC?

Tuanze na swala la uanachama, ICC ni mahakama ya kimataifa inayoshughulikia makosa ya kivita(War crime), uharifu dhidi ya binadamu( Crime against humanity), Mauaji ya Kimbali (Genocide) na Uvamizi (Act of Agression) Mahakama hii ilianzishwa Julai 1, 2002 huku ikiwa na wanachama 60 kufuatia Mkataba wa Roma wa Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (Rome Statute) wa mwaka 1998. Baadhi ya mataifa ambayo hayakukubali kuwa wanachama wa Mahakama hii ni Marekani, China, Iran, Israel, Qatar, na Libya.

View attachment 2556125

Urusi ilisaini mkataba wa ‘Rome statute’ lakini haikuwahi kuthibitisha ‘ratify’ ili kuwa mwanachama halali hadi mwaka 2016 ilipojitoa rasmi kwenye mkataba huo. Kwa upande wa Ukraine haikuwahi kuwa mwanachama. Hapo unaweza kujiuliza imekuwaje ICC iingilie kati mgogoro kati ya mataifa ambayo sio wanachama wake? Ipo hivi kwenye mkataba wa kuanziswa kwa Mahakama hii ya Kimataifa Kifungu cha 87(5) kinaelezea ushirikiano kwa mataifa yasiyo wanachama wa ICC. Kifungu hicho Kinabainisha kwamba Mahakama ‘’inaweza kualika Nchi yoyote isiyohusika na Mkataba huu kutoa msaada chini ya Sehemu hii kwa misingi ya mpangilio wa dharura au kwa makubaliano na Nchi hiyo au misingi yoyote inayofaa. Hivyo Ukraine pamoja na kutokuwa mwanachama imetumia nafasi hiyo kutoa ushahidi dhidi ya Putin kuhusu makosa ya kivita na uhamishaji haramu wa binadamu (hasa watoto).

Swali la mihimu ni je Putin atakamatwa baada ya hati ya kukamatwa kwake kutolewa na ICC?

Tunapaswa kujua kwamba ICC haina nguvu ya dora kama jeshi na Polisi hivyo hutumia wanachama wake kukamata waarifu na kuwapeleka mbele ya Mahakama (Baada ya Hati ya kukamatwa kwa muharifu kutolewa kama mtu huyo ni raia wa nchi isiyo mwanachama wa ICC atasubiliwa hadi atakapo toka nje ya nchi yake na kutembelea nchi mwanachama wa ICC Inchi hiyo iliyotembelewa ndiyo inaweza kumkamata ingawa swala hili sio la lazoma kwa nchi husika)

View attachment 2556126

Raisi wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir alitolewa hati kama hii mwaka 2009 wakati akiwa bado madarakani na alitembelea nchi kadhaa wanachama wa ICC bila kukamatwa licha ya ICC katika Mkataba wake kutotambua ‘Immunity’ kwa viongozi wa nchi. Swala la kukamatwa kwa Raisi wa nchi flani tena akiwa ziarani katika nchi nyingine ni gumu kutokana na makubaliano mengi ya kidiplomasia kabla ya Ziara ya kiongozi wa nchi katika nchi nyingine hivyo swala la Putin kukamatwa ni ndoto ambayo ni ngumu sana kutimia tena pengine haitotimia.
CC: 5523
 
Back
Top Bottom