Pole sana mkuu
Kinoamiguu kwa tukio lililomkuta ndugu yako. Sijaziona nyaraka alizopewa nduguyo ikiwa ni pamoja na barua ya kufukuzwa na hati ya mashtaka ya kinidhamu, ningeweza kushauri vyema hatua za kufanya.
Umepewa ushauri na
Prosperity96 na wengine kuwa nduguyo aende CMA na wengine wamesema aende Mahakamani, lakini kwa jinsi ulivyosema 'enzi za giza' ni kama unaamanisha nduguyo alikuwa mtumishi wa umma.
Kama nipo sawa kuwa alikua mtumishi wa umma basi asithubutu kwenda CMA au Mahakamani maana ataangukia pua asubuhi tu kwa ma-PO kutoka kwa mawakili wa serikali. Kuanzia tarehe 28.03.2022 CMA ilipigwa marufuku kusikiliza migogoro inayohusu watumishi wa umma.
Nipo Dar, nitafute tushauriane njia ya kupita.