Hatimae Flora Mbasha awa Flora Kusweka

Hatimae Flora Mbasha awa Flora Kusweka

Hatimaye staa wa muziki wa Injili Tanzania Florance Henry 'Madam Flora' amefunga ndoa na Daudi Kusekwa baada ya kukaa muda mrefu wa upweke kutokana na kutengana na aliyekuwa mumewe Emmanuel Mbasha.



Oya ' Masela ' tuliokaa Chuo Kikuu miaka ile ya 1988 hadi 1992 hasa Mtaa wa KILELENI kule juu Mlimani huyu Daudi Kusekwa siyo yule tuliyekuwa tukimpiga sana ' Makwenzi ' ambaye alikuwa na Dada yake Bonge hivi aitwae Penina? Hii sura sasa naanza kuiangalia naona kama vile niko ' familiar ' nayo. Msaada jamani kwa wale wenzangu na Mie wa Kitaa cha Chuo Kikuu ' kitambo ' kile.
 
Kila LA kheri Flora. Maisha ni yako ma maisha ni wewe. Huwezi kuishi maisha ya wengine maana utakuwa mtumwa wa wengine hadi kufa. Umefanya uamuzi sahihi, songa mbele na endelea kumtukuza Mungu maana kila jambo lina maana yake. Mipango ya Mungu sio ya mwanadamu.
Usiruhusu mtu yeyote awaye kuhoji juu ya maisha yako. It's you and only you.
una rahisisha mambo, iman ya kikristu haipo ivo mkuu
 
Umeuliza swali la msingi mkuu naamini wakakapokujibu itanisaidia na mm kupata majibu
Hawawezi kunijibu maana ni mafarisayo, wanakarili na si kuelewa, japo wanajifanya kujua, hawajui hata misingi ya Ndoa wanakarili vifungu vichache,
 
Uko sahihi kabisa! Biblia haijaruhusu kabisa kuacha mke/mume kisha ukaoa tena.
Biblia imeruhusu kuacha mke/mume kwa ajili ya zinaa lakini huyo aliyeacha/achwa asioe/asiolewe ili kutoa nafasi ya kusameheana na kurudiana. Hakuna kuoa/kuolewa tena mpaka kifo kitakapowatenganisha!
Lakini kuna mazingira ambayo biblia huruhusu kuoa/kuolewa. Mazingira menyewe ni kuwa ikitokea mmoja ya wanandoa si mwamini wa ukristo, na huyo asiyeamini akaamua kuondoka kwenye ndoa, yule aliyeachwa katika mazingira hayo anaruhusiwa kuoa/kuolewa tena! Lakini mwamini haruhusiwi kuondoka kwenye ndoa hata kama mwenzi wake si muumini wa ukristo ili maadam yuko tayari kukaa naye!
Na vp km mwanandoa mmoja atakuwa kuingia kwenye Ndoa na kukiri viapo kiutapeli Yaani hakuwa na Nia ya dhati ya kuishi milele,aliitika ama kuingia ili kutimiza jambo na hii unasemaje
 
MTU hufungwa kwa kamba za kinywa chake! Ukiapa inakuwa hivyo hata kama ulikuwa unadhani unatania! Ukiunganishwa umeunganishwa maana umetoa nafasi kwa kinywa chako kuunganishwa! Suala kuwa ulikuwa unadanganya halipo Bali ulikuwa unaidanganya nafsi yako mwenyewe! Na utavuna matunda ya udanganyifu kwa kujifunga kwenye ndoa mpaka kifo kikutenganishe! Vinginevyo utakuwa umeikana IMANI na sahau habari ya kufika mbinguni!
Umeongelea adhabu ya tapeli alodanganya hii kila MTU anajua, sasa imefika mahali tapeli kaamua kuvunja Ndoa baada ya kutimiza azma, Vipo juu ya mwenza wake alokuwa na dhati?
Halafu swali langu ni kuhusu ubatili na uhalali wa Ndoa,
Ndoa inasisitiza Nia ya dhati ya kuishi Mpaka mwisho wa Maisha, inasisitiza makubaliano ya hiari yasiyoshawishika Kwa kitu,ndoa na mtu alodanganya viapo ni Ndoa halali?
Na mdanganyifu akileta shida manteso na visa vya makusudi ili waaachane na ikawa hivyo na hii mtasemaje, maana Toka awali palikuwa Hapana udhati na utayari Kwa mmoja,
 
Back
Top Bottom