Tusikariri. Tuchambue. Kwani maisha nini? Hivi Biblia unaisoma kuanzia kitabu gani, ndugu Francoo. Maana ndoa zilikuwepo tangu enzi za agano LA kale ambalo halikutenguliwa na agano jipya bali lilitimilizwa. Hivyo, sio busara kusoma yale tu yanayokupendeza moyoni bali hata yasiyokupendeza maana kwayo utajenga msingi wa kuimarisha utetezi juu ya yanayokupendeza pasipo kuikwaza kweli. Biblia inasema, itafuteni kweli na kweli itakuweka huru. Ukikwepa ukweli utaumia wewe maana kweli haibadiliki.
Huwezi leo kukataa kuwepo yasiyovumilika.
By the way, angebaki pasipo kuolewa kwa faida ya nani? Asiolewe ili kumfurahisha nani? Maana uzinzi upo hata kutamani tu demu anayepita mbele yako, unamwangalia hadi unamzini. Ni uzinzi tu huo kama ulivo wa kitandani au kichakani.
Hivyo, iwapo asingeolewa ni wazi angeendelea kuzini kwa mawazo. Angekuwa ni mtu wa kuelekeza macho yake kwenye suruali za wanaume kuona zinavyotuna kwenye zip. Ameamua sahihi na Mungu ndiye mwenye hatma yake.
Ni vema tukaheshimu maamuzi yake.
Aidha, wengine wanasema kaoa kijana; duuuuuh, kwani kambaka? Ikumbukwe ndoa ni mchakato ambao hata wazazi huridhia, sasa wewe unayesumbuliwa na tukueleweje kama sio wivu?