Hatimae hukumu imetoka tayari, siku ya kwanza tu ya kesi kusikilizwa

Kwanza nikupe pole kwa yote. Pili kama ni mechi ndio kwanzaaaa imeanza. Sikutishi bali uhalisia utauona baada ya hizo siku 45. I wish ningejua tangu awali una moango wa talaka. Ninvekushauri vingine. Muziki upo kwenye mali na watoto.

Kiufupi mkeo wa zamani ndani ya siku hizo 45 anaenda kukusanya ushauri wa kila aina na vumbi litatimka upya. Mahakama bila kesi hakuna mishahara kwa mahakimu na watendaji wengine pamoja na mawakili, hivyo sio wa kucheka nao. Yani ni bora mngetengana na kila mmoja kuishi kivyake. Pengine ingefika siku mkapata ufunuo. Nakupa pole tena. Bado hujachomoka
 
I DID THE SAME. hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiivyo hivyo na iliisha chap kwa haraka! Mi sikutaka hata mali, sikutaka hata matunzo ya mtoto(mmoja ndo yuko under 18) . Nilisema tu naomba full custody, oh atanizuia kuona mwanangu, nikamwambia hakimu yeye ndiye Baba, anapohitaji kuona mwanae atoe taarifa asinivamie nyumbani kwangu, nilishahama kwenye nyumba tuliyokuwa tunaishi, nikamuona anafuta jasho, mara aaombe udhuru aende toilet, alifuta jasho, alitamani kuniongelesha , alitaka sijui kufanyaje. Mi nilinyooka na maamuzi na sijawahi jutia the process na hukumu iliyotoka.

Kuna watu wanaamini talaka ni kifo, aiseeeh sio kweli.
Mtu anakuhamishia msala wakati yeye ndo ana kila makosa anakutishia talaka, we bana ileteeee! Mambo yawe mafupi.
Kudos mkuu, karibu uraiani tupambane na hukumu za walimwengu za yule kaachika yule ni mtalaka yule kashindwa ndoa.

WE KOMAA NA UNACHOJUA KILICHOTOKEA NA AMANI YAKO YA NDANI!
 
mfano..
kati ya mke/mme wa mtu akionekana vyumba vya wagen/lodge hebu nipe jibu nani ataonekana malaya asilimia kubwa?
Unaona sasa! Unataka kusema mume wa mtu akiwa guest sio malaya ila mke wa mtu akiwa guest ndiye malaya.

Nyie endekezeni tabia zenu hizo ila msisahau wanawake wengi wa siku hizi ndoa haziwababaishi tena waliopo kwenye ndoa.
Labda wale ambao hawajawahi kuolewa ndio wanazitamani na wao wakiingia wanatafuta njia ya kusepa.
 
Hayo mambo ya mwanamke pekee ndie akae kuilinda familia siku hizi hayapo.
Wote tulinde familia mwanamke na mwanaume.

Ndio maana talaka ni nyingi siku hizi sbabu wanawake wengi hawapo tayari kuteseka kwa kigezo cha kulinda familia.

Wote tunawajibu wa kuilinda familia ila hoja ya kusema mke anasaliti sababu mwanaume kazembea mahali, hiyo sio sawa.
Ukianza kutambua madhaifu ya mwenzako na wewe uwe pale kama kufidia alipofeli, familia yako itakuwa salama.

Ila ukitumia kusaliti kama kufidia mme alipofeli, familia itakushinda. Sababu hata huko utakapoenda, mwanaume hatakuwa perfect, kwahiyo napo utasaliti pia. Circle ya usaliti itaendelea.
 
Wanaume mnateteana kuchepuka mnateteana mkiachwa mnateteana.
Hizi cases za cheating zipo nyingi sana. Hata wanawake huwa wanapitia magumu. Ishu ni kwamba jamaa huyu ametoa mustakabali mzima yaliyomkuta, ndio maana tunajadili yaliyomkuta na si hisia kwamba 'hata Wanaume wanacheat na wana vinyongo na kutosamehe'. Ishu sio kutetea, ni kuandika kulingana na aliyoeleza. Hata angekuwa ni mwanamke basi tegemea ungeona comments nyingi tu. Shida unaleta sana hisia za kutaka kuonekana kama anatetewa. Jadili ishu iliyopo jukwaani na sio hisia.
 
Akitaka asisumbuane nae , amwachie kila kitu!
Kwani nini bana, mali ni nini over the inner peace.
AKAANZE UPYA! af rahisi kuliko maelezo, mwaka wa 3 tuu na sijawahi kujuta na sitajuta.

Kuhusu watoto wala asigombee mtoto, amwache huyo mama aamue, yani hakuna kitu kizuri kama kujifanya umeshindwa ! WEWE UNAJUA ULICHOSHINDA.

AMPE USHINDI anaotaka!
 
Mkasa wa fanton mahali nimeusoma tokea mwanzo na nipo upande wake.

Hisia zangu zimekuja katika kumjibu eroni aliposema kwanini ishu kama hizi wanawake huchangii kidogo.
 
mimi ni Ke,
a divorcee mwaka wa 3 huu.
Mtalaka wangu aliniletea hizi hizi za kiwehu, aseeee nilimnyoosha!
Unajua watu hudhani maisha yanaishia kwenye kuoa/kuolewa.
Hapana , far as i love to be loved and to love, i love myself too.
Huwezi kufanya ujinga wote in the life, nikireact unanitishia SHAURI LA MAHAKAMA, ehehehhehee
Mpaka kesho sidhani ile scenario ataisahau.

Naulizwa na hakimu unataka talaka, namjibu yes
mimi aliniwekea kosa la cheating, ilhali yeye ndo anaishi na mwanamke (shauri la talaka lazima liwe na kosa)ahahahahaha nyau yule aliweka na kosa la namtishia uhai(nikamwambia hakimu na mkimuacha msimpe talaka anayotaka siku mtanihukumu kesi ya murder, nilichukia sana kiukweli)
Yani unashtakiwa makosa ambayo yeye ndo anayafanya, afa anakuwahi Baraza la Kata.
AH NILIMFURAHISHA!
Mi nikamwambia hakimu ndio ,(mwanasehria alishanitonya ukitaka hjii kesi iishe fasta kubali kila kosa analoshatki)
So nikakubali kila alichotaka, nyumba sijui nini nini, nikasema na yenyewe siitaki!
Mtoto oh nikitakiwa kulea basi nikae nae , akikaa nae yeye mimi baba nisihusike
Nikamwambia hakimu no worries mi mamake nipewe nitalea mwanangu na sitauliza mia ya mtu.
Ustawi wananiuliza mara mbili mbili, we mama , nawambia jamani mi nisipewe matunzo, naombeni tu mtoto wangu kwa 100%custody.
Jambo likaenda chap kwa haraka.
 
Ephen sikiliza wakubwa zako utapata heri duniani soma JF 20:20 πŸ˜‚πŸ˜‚

inasema hivi

"Ukiwa unashauriwa na aliyepitia magumu heri ufuate mazuri yake, ili mtesi wako akija ujue kujikinga na wewe uchunge mdomo yako na matendo yako yasije haribu matunda uyaonayo na kuyapataa"
πŸ˜…
Hii ndio JF 20:20 πŸ˜‚
 
Facts
 
Wanaona wanawake wana mioyo ya chuma na wanatakiwa kutendewa kila aina ya unyanyasaji. Wanasahau kuwa hata chuma huwa kinapata kutu with time.
 
Wanaona wanawake wana mioyo ya chuma na wanatakiwa kutendewa kila aina ya unyanyasaji. Wanasahau kuwa hata chuma huwa kinapata kutu with time.
Wakubali tu dunia imebadilika, wanawake wa zamani walikua wakipewa talaka wanasakamwa dunia nxima ilibidi wavumilie mateso ili wasitoke ndoani.

Wanawake wa siku hizi wanajua kutafuta hela, kupewa talaka sio ishu tena hakuna anayekubali kuvumilia mateso.
 
Hawara mtamu kama mtu Γ natunza huyo mke. Ajiachiwa majukumu lazima nae aingie mitini.
Ndiyo maana nikakuandikia kwamba maliza kesi haraka mgawane mali maana aliyekuwa mkeo ni mshali sana angeweza kurudi kimabavu akasema hujampa talaka wewe bado ni mumewe.
Mahakimu ujue nao wanawadharau wanawake wanaong'ang' ana na talaka.
Tayari huyo X wife keshapigwa na kitu kizito.
Atarudi kulia sana.
 

Mwanamke anajua exactly kadi gani azicheze ili mwamba acheze ngoma yake.

Hiyo ni leverage. Jamaa akimnyang'anya leverage huyo mwanamke hana pa kumpigia

Naam,
Imetimia kama ilivyoandikwa. Hongera sana mkuu picha limegeuka starring haamini.
 
Pole na hongera pia. Kwenye hili suala imeonyesha kwamba mkeo ana makosa tangu mwanzo, na talaka kaitaka mwenyewe. Umempa kila kitu anachohitaji ili kuepusha migogoro zaidi.
Nikwambie tu kwamba huko anapokwenda anaenda kukipata cha mtema kuni miaka si mingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…