Hatimae hukumu imetoka tayari, siku ya kwanza tu ya kesi kusikilizwa

Tumeshamwambia mleta mada, akijifanya kuregeza kamba mbeleni kwa kujifanya atamsamehe huyo mwanamke kisa amejifunza, basi ndo utakuwa mwisho wake.
 
Tumeshamwambia mleta mada, akijifanya kuregeza kamba mbeleni kwa kujifanya atamsamehe huyo mwanamke kisa amejifunza, basi ndo utakuwa mwisho wake.
Kuna broh pale kijiweni tunapotafutia mkate yalimkuta,

Iko hivi, yule jamaa alibahatika kujenga kajumba kake kakubwa kubwa tu na miradi miwili mitatu,

Basi mkewe akaanza kutafunwa tafunwa na vijana wadogo mpaka akili zikamuisha akaanza kudai talaka bila sababu ya msingi huku akiaminisha Ummmma kuwa mumewe ana shida sana ,

Yule broh ni wale watu buyu kali kwa siku anaongea maneno 20 imeisha hiyo,
Basi ikaenda wee broh akakubali talaka na mgawanyo wa mali ,

Baada ya taratibu zote ndipo mgawanyo wa mali ukaanza broh akapata washauri pembeni wakampanga,

Basi nyumba ilipopigwa thamani yake na mahakama kwa maana ya nusu kwa nusu yule broh jamaa wakamsaidia hiyo nusu akampa mwanamke,


Aisee hawa viumbe wakatiri mwanamke alitaka kugoma kwa madai anataka nyumba auziwe mtu mwingine ndio wagawame ,

Baada ya kupigwa mkwara mahakamani ndio kukubali kuchukua hela yake nusu,

Broh akaendelea kukaa pale pale mjengoni ,

Yule mwanamke hela zote akazitumbua na vijana wake
Sasa hivi maisha anayoishi aisee KARMA ipo wakuu kabisa kabisa
 
Yah, Karma is real. Lakini pia wanaume wenye upendo wa dhati tuna tabia ya kumuamini sana mwanamke.

Mwanaume anaingia ktk ndoa kwa kupenda. Yaani kumpenda mwanamke, mwanamke anaingia ktk ndoa baada ya kuona status ya sasa ya maisha ya mwanaume na ijayo pia. Kwahiyo akishazoea yale maisha, kukukana wewe mwanaume mbeleni ni rahisi tu.

Anguko la mwanaume aliyesimama kwa zaidi ya 90% hutokana na mwanamke wake anayempenda.
 
pongezi kwa kumaliza kesi kiume big up sana
 
Mmbo ni ya moto hivi na hamsemi
 
Pole sana kaka, kila nifikili kuhusu swala la watoto huwa nakosa nguvu, sijui kwanini ila itakuwa ngumu kuishi mbali na watoto wangu. Ndoa za sasa Mungu aturehemu tu. Binafsi nitaoa tu kikombe hiki hakiwezi kuniepuka.
Sasa jiulize huyo mwanamke ni kiumbe cha namna gani mpaka aone ni bora mwenzie aishi bila watoto ila yeye aishi nao.
 
Wanaume mkishamzalisha mtu tena mtoto zaidi ya 1 huwa mna vitabia vyenu ambavyo mnaviendekeza mkijua wanawake hawana pa kwenda.
Mwanaume cku zote anapambana awe na family bora na kuitunza.. Ataanzaje kumdharau mwanamke wa ndan alie mtiifu kwake na mwaminifu?

Mwanamke akikuzalia watoto anajua amefka sasa ko ataanza kuleta vitabia fulan iv, Akijua amefka na mwanaume huna pakwenda koz kuna watoto. Tena usiombe kama kuna MAKARATASI YA NDOA, ni KIFUNGO
 
Hiyo ya kuishi na mwanamke mwingine alizingua sana, hakuna kitu inauma kama usaliti. Maumivu yake hayaelezekei. Niliwahi pitia scenaria ya kusalitiwa, unaweza ukakaa chumbani ukawa unataja tu jina la mpenzi wako bila sababu. Maumivu yanaambatana na stress za hali ya juu hasa ukikumbuka ulivyojitoa kumpenda.
 
Huyo anashindana na Mungu, sasa Mungu akitaka amtandike mtu huwa anamuinua juu kisha anamdondosha. Hilo anguko linakuwa ni zito. We subiri muda utakuja kukupa majibu.
 
ahahahahhahhaa nilijifunza kutokujilaumu kwa kumpenda mtu!
 
aisee pole sana ila hako ka-ujumbe ka kwenda mahakani kusubiria kwa nje made my day, thanks mkuu
 
Kwa nini ulichelewa kumuacha?
Unadhani kukubali kuwa imeisha ni swala la kuamka tu na kusema basi.
Ehehehehh, mi huwa nawasikiliza watu wanaodhani swala la kuachana na mwe
una uhakika moyo una amani mkuu,...kama kuna tatizo usisite kuniungisha MAPANGA yaliyoNOLEWA kabisa.... thanks in advance..🙏🙏
eiissh!
Ya nn sasa?
 
Mwanamke akiwa na uhakika wa kula, kuvaa, kulala, watoto wa kutosha. Hawezi tena kuthamini ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…