Hatimae hukumu imetoka tayari, siku ya kwanza tu ya kesi kusikilizwa

Hajataka tu kuwa na mambo mengi na kuwa na mlolongo mrefu wa kesi.
 
Nakupongeza sana kwa ujasiri ndugu, kuna mambo hapa duniani sio ya kupambania kabisa, as long as wewe ndo ulitafuta mali, utapata nyingine.Wanawake sijui wana-ushetani gani tu - ubinafsi mwingi sana- yaani mtu unawatoto unang'ang'ania talaka - si ukichaa huu kabisa.
Hongera mwamba Mungu akutangulie katika maisha mapya.
 
Kuna ndezi flani uzi uliopita lilisema sheria itampa asilimia 10 kisa watoto watabaki na mama alafu mwanamke achukue 90. Nililiuliza hao watoto kuna mali yoyote walichangia kuitafuta likabaki linamanga manga tu
 
Hajataka tu kuwa na mambo mengi na kuwa na mlolongo mrefu wa kesi.
Kesi ni jaka moyo mkuu,nilikuwa na kesi mahakama ya kisutu ilikaa miaka minne hadi kwisha, ukitaka kusafiri nje ya mkoa hadi kibali sijui,ukiumwa uwe na cheti cha hospital ya serikali kuthibitisha ukwenda mahakamani sababu ya ugonjwa,nk nk,

bora jamaa amehamua tu liishe kwa haraka awe huru.
 
Huu uzi wanawake mmechangia wachache sana, aishi ushauri wako.
 
Ahsante sana mkuu, nashkuru
 
Mjomba angu alikimbiwa na mke aliyezaa nae watoto watatu, mke akadai talaka kisa kupigwa kwa kutoa mimba ya mwanaume mwingine.

Mpaka mwaka jana mjomba angu alikua anatuma watu kwa mkewe kuomba msamaha warudiane ila mke akakataa wakati makosa ni yake.

Sasa hivi ana mimba na mwanaume kamkataa kumbe ni mume wa mtu.

Mjomba angu amepata mwanamke mwingine wanatarajia kufunga ndoa mwezi wa 6 mwaka huu.
 
Na kuna mazingira huwa inakua mpaka 70% 30% mkuu..inategemeana na mazingira vinginevyo mnatakiwa muanze ku establisha proof kwann upewe au usipewe % unayotaka endapo hujaridhika
 
Daah..sijui kwann huwa wanakua wepesi kushauriwa namna hii.
Ila anyway, huyu mwenzangu natumaini yeye alishajipanga
 
Daaahhh pole sana mkuu. Pole sanaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…