Hatimae hukumu imetoka tayari, siku ya kwanza tu ya kesi kusikilizwa

Hatimae hukumu imetoka tayari, siku ya kwanza tu ya kesi kusikilizwa

Ukiwmua kufànya umalàya wewe fanya, usitafute sàbabu eti mbona wànaume wànafanya.
Ni maamuzi yako usitafute uhalali wa kuws malaya kisà mwanaume nae ni malaya.
Ila aangalie asikamatwe aanze kusema mbona ye anafanyaga.Wanawake wakichepuka wanaelemewa na mtu wa nje hawawezagi kubalance.Shauri yake
 
sema hapo kwenye mgao wa mali baada ya pendekezo la 50/50% toka kwa hakimu na wife kuomba 60% ungemwambia hakimu nampa 70%

ajue kabisa hutaki mazoea hata siku za mbele asilete huruma
 
Wakuu heshma kwenu.
Habari za jioni.

Nimeona ni vyema kuwa update kuhusu mwenendo wa suala ambalo nilileta hapa jukwaani siku ya jumatatu katika uzi huu 👇👇👇👇


"Samansi" ya mahakama ilielekeza nifike mahamani siku ya leo tarehe 12 Feb 025 nami nikafanya hivyo.
Katika kesi hii mimi kama mdaiwa na aliyekua mke wangu kama mdai.

Niseme tu kitu, katika mfumo wa serikali na personally katika suala hili, nimekuja kugundua, wanawake wame occupy sana nafasi nyingi serikalini, sasa sijui sababu ni nini?
Maana ;
- nilipoitwa dawati, incharge pale alikuwa mwanamke.
  • nilipoitwa baraza, kikao chote kilijawa na wazee wa baraza wanawake
  • leo hii mahakamani, hakimu alikua mwanamke.
Hakika wanawake wametaradadi everywhere, tukiendelea kwa mwendo huu, wanaume twafaaa
😁😁😁😁😁.

Anyway,.

Kama ambavyo nilikua nimeamua kuwa natamani hili suala liishe tu, na pia kwa kuzingatia ushauri wa baadhi yenu ndugu zangu wana JF, sikupemda kesi iwe na mambo mengi.

Tulipoitwa chamber na hakimu, alianza kwa kusema "hii kesi leo mmeitwa ili iweze kutajwa tu na kipangiwa siku nyingine, hivyo, mdaiwa utasomewa tu charges zako kisha kama una neno utatamka"

Akasoma,kama ilivyo ainishwa kwenye "samansi" niliopokea ,kuwa mdai anataka
1. Talaka
2. Mgawanyo wa mali
3. Kuishi na watoto
4. Matunzo ya watoto

Akauliza "unasemaje?"

Nikamjibu, "nimesikia na sina pingamizi juu ya lolote katika hayo, na kwasababu sina pingamizi naomba mahakama kama inaweza, hili suala tulimalize hapa hapa na leo leo mheshimiwa hakimu"

Akauliza "umekubaliana na haya yote?"

Nikamjibu "ndiyo, nakubaliana na dai lake la talaka, pia nakubaliana na dai la mgawanyo wa mali, japo nitaomba kujua muongozo wa mahakama unasemaje kuhusu hilo , pia muongozo wa mahakama unasema nini kuhusu matunzo ya watoto na kuishi ma watoto, maana yote niko tayari ku comply"

Akasema "kama ni hivyo, basi hii kesi ni nyepesi na itakwenda vizuri, kuhusu mgawanyo wa mali, mahakama ina suggest 50% 50%, unless kama kama mmoja wenu hajaridhika na mtahitaji tuingie katika ushahidi wa kuthibitisha mchango wa kila mmoja kwa vithibitisho.

Pia matunzo ya watoto yamejikita katika chakula, malazi, afya, na ada. Jukumu hili ni la baba kikawaida, lakini mahakama inaangalia kama mama naye anajiweza, basi jukumu hili wote mtagawana.

Na mwisho kuhusu kuishi na watoto, maadam wako chini ya miaka 18, wataishi na mama, ila baba una ruhusa ya kuwaona . Kama unahama mkoa, maana yake watoto watakuja kwako likizo ambapo, mama atagharamia nauli za kwenda likizo na baba atagharamia nauli za kurudi.

Hivyo basi , ndugu mdai nitakuuliza na utajibu hoja moja baada ya nyingine.

1. Talaka.

Hapa nikawaambia sina pingamizi, niko tayari mke wangu apewe haki yale kama anavyo hitaji. Hapo, wife nikaona kashusha pumzi ndedu nzito. Na muda mwingi alikua anajifuta jasho ingawa ndani pana feni. Katika session yote honestly, sikumtazama usoni. Na hatukusalimiana.

2. Mgawanyo wa mali.

Nikasema, kwakua kesi hii imeshanigharimu suala la muda , nakubaliana na pendekezo la mahakama la fifty fifty, kama mwenzagu, mdai anaona amebanwa naomba apewe uhuru wa kuchagua ratio itayompa comfort. Akasema mimi nataka 60%. Hakimu akauliza, mdaiwa (mimi yani) uko tayari, nikasema SINA PINGAMIZI, mahakama impe hiyo 60% anayotaka.

3. Matunzo ya watoto

Hapa nikasema, always nimekua nalipa ada miaka yote, hivyo hili nitae delea nalo, na pia nitawahudumia gharama ya chakula isiyozidi 150,000/= kwa mwezi kwa kuanzia kwasababu, suala hili limeniathiri biashara zangu pia nahitaji ku settle na kuanza upya maisha, hivyo nikitulia nita adjust.

4. Kuishi na watoto.

Nikasema, nakubaliana na pendekezo la mahakama hapo juu.

Hakimu akasema, aisee, hii kesi imeemda vizuri sana.

Wife akaomba "mheshimiwa naomba kidogo niongee na baba .... pembeni, kuhusu suala la mgawanyo wa mali"

Nikajibu "hakimu, sihitaji kuzungumza private , maana sioni kama kuna suala lolote ambalo kwasasa naweza ongea nae tukaelewana, kama ana jambo lolote aliseme hapa mbele yako"

Wife muda woote alikua anafuta jasho sijui maana yake ni nini, lakini katika vitu naamini, ni kwamba alitegemea confrontation na mimi labda nimuwekee kauzibe na vikwazo vya kukubali ombi la talaka, lakini akaona kila kitu nimekubaliana nae kama alivyotaka. Na kila alipotaka kuibua malalamiko, hakimu akawa anasema, naomba tusiguse sababu za mgogoro wenu kwakua sio sehemu ya madai yako mdai, yote uliyodai, tujikite hapo.

Hakim, akayasoma maandishi aliyoandika kisha akaita kila mtu asaini, nikasaini na yeye akasaini, lakini anaposaini akawa anajilalamisha chini chini, hata sijui anaongea nini.

Basi baada ya hapo tukaambiwa , baada ya siku 45 hati ya talaka itatoka na taratibu za utathmini zitaanza, hivyo tutakiwa kufika.

PIa nikatumia fursa hiyo kueleza kuhusu uharibu wa wa wizi uliotokea nyumbani kuonyesha RB ili ifahamike kuwa mali imeharibiwa na wezi.

Pia , ikafamika pale katika shauri kuwa mimi nilishahama nyumbani, na hii nikaona imem suprise mdai wangu, na sijui sababu ni nini!.

Baada ya yote, hakimu, akasema tumemaliza.
Nikanyanyuka na kutoka, japo niliona yf anaaga huku amekaa ana delay kutoka, like she was exhausted with the proceeding that ended.

Sijajua sasa kama walikua wanayapanga yao mengine au lah!!

Ikaisha hivyo.

Sasa baada ya siku ya 45 days ndio mengine yatafuata.
Kifupi nimefurahi hili suala halijawa extended, ngoma imeitwa leo na imetamatika leo, maana wengi walikua wanasema hii kitu inaweza ikaenda 2 months.

ADDITION:
Wakuu, kesi za kuvunjika ndoa ni nyingi sanaa nimekuatana nazo leo mahakamani. Hali sio nzuri kwenye hii taasisi ya kwanza kuanzishwa duniani

SHUKRANI WAKUU.
Usiku mwema

Pole sana sana ndugu yangu kwa ndoa yako kufikia hapo ilipofikia.Shetani amefanikiwa kufanya uharibifu mkubwa kwa taasis yenu.Tazama sana watoto wako wasije wakaathirika negarively kwenye maisha yao na jambo hili.Hao hawana hatia,endelea kuwafuatilia kuhakikisha wanapata matunzo sahihi
 
Mjomba angu alikimbiwa na mke aliyezaa nae watoto watatu, mke akadai talaka kisa kupigwa kwa kutoa mimba ya mwanaume mwingine.

Mpaka mwaka jana mjomba angu alikua anatuma watu kwa mkewe kuomba msamaha warudiane ila mke akakataa wakati makosa ni yake.

Sasa hivi ana mimba na mwanaume kamkataa kumbe ni mume wa mtu.

Mjomba angu amepata mwanamke mwingine wanatarajia kufunga ndoa mwezi wa 6 mwaka huu.
Hii dunia ukiwa mtu wa kushangaa utajikuta unapoteza muda mwingi sana maana kila siku wajinga wanazaliwa ona situation kama hii.

Vitu vya ajabu kabisa,in short hapa walikutana pipa na mfuniko yaani wote akili hawana.
 
Mkuu Fanton Mahal kwanza pole na habari za kesi (kesi zinakula sana muda wa wadaawa) ila Mkuu nikuhakikishie jambo moja hapo hakuna mlichokifanya wala kukikwepa kwenye swala la muda. Nitakuambia kwasababu gani nasema hivyo.

Kwanza kabisa kesi zote za madai ya hamri ya talaka ni sharti la lazima zisikilizwe ushahidi hii ni ili Mahakama ijiridhishe kupitia ushahidi uliotolewa kuwa kweli hiyo ndoa imevunjika kiasi cha kushindikana kurekebishwa.

Nimesikitika sana juu ya mwenendo uliochukuliwa na Mh. Hakimu husika maana ni amefanya kituko cha aibu sana.

Tukiachana na hili la amri ya talaka embu tuangalie hapo kwenye chumo la pamoja yaani mgawanyo wa mali na mali zenyewe.

Kwanza kama imeenda hivi ulivyosimulia hapa ni dhahiri na wazi kuwa mkeo ameshindwa kuthibitisha kwanza uwepo wa hizo mali zilizotokana na ndoa, kwanini nasema hivyo ni kwasababu hizo mali ambazo bado mkapewa mgao wa 60%kwa 40% bado hata hazijatajwa hapo Mahakamani. Sasa mimi na wewe na wana JF wote tujiulize mmegawana mali gani na ipi hiyo ambayo imetajwa Mahakamani?

Tuache hili la mali na mgawanyo wake embu tuangalie hilo lingine la kuhusu watoto ambao nao mmesema wakae na mama yao, tujiulize swali tena ni watoto wapi hao?, ni nani na nani kwa majina yao?, je walitajwa hapo Mahakamani na kutambuliwa inavyopaswa kuwa?.

Hii ni aibu nyingine kwa mhimili wa Mahakama, na hapa haujatoa rushwa (sababu hujataja swala hilo) ila Mh. Hakimu kwa uzembe wa kukosa weledi amekinzana na taratibu zote na sheria zote zinazosimamia mashauri ya migogoro ya ndoa.

Nina uhakikakama utaitaja hiyo Mahakama basi hilo jalada litaitwa na Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya maana hii ni aibu na imeshakuwa mazoea sasa.

Hata kwa kuokoa muda wenu basi Mahakama ingepokea ushahidina utetezi siku hii hii moja kuliko kukanyagataratibu hivi zilivyokanyagwa. Ninaelewa kusudio lako la kuokoa muda na gharama lakini hii wiki na wewe umejifunza utaratibu usio sahihi wa namna kesi za talaka zinavyoenda.

Kesho au keshokutwa utamshauri mtu au kumpa uzoefu wako huu na akikutana na Mh. Hakimu anayejua nini kinatakiwa kufanyika ataanza kuhisi au kufikiri kuwa Hakimu husika anaweka mazingira magumu ili adai rushwa, mwisho wa yoteni kukosa imani na Mahakama na mfumo wake wote.

Hili linasikitisha sana.
Aliyekiukwa haki, ndiye amekubali yaishe.
hamna kesi hapo,
 
Mimi ni mwanamke na nilifanya hiki hiki alichofanya huyu.
Yani kama alikuwa anasimulia session ya talaka ilivyoenda kwangu.
Kila neno kila nukta!
Mali tunapata na kupoteza kila siku.
wacha iende
Sema man wako alizingua, yan yeye ndio alikupeleka baraza la kata? Why? Kwann akalie lie huko ?yan mwanaume akakushtaki mwanamke??
 
Mtalaka wangu amhakamani alileta hati ya shamba aliyonunua na mamake, akasema nyumba ni ya familia.
ilhali nilijenga ile nyumba kwa 80%
Hakuamini ambavyo niliridhia kuwa hatukuwa na mali yoyote zote ni za familia alikozaliwa.

Unaanza tu moja, mradi una uhai, afya, amani na matumaini kuwa kila kitu ni mipango ya Mungu and you did your best kufanya hiyo siku isifikie.
Mi nilijuliza maswali nikapata majibu kuwa kuliko kuendelea kuburuzana na habari za changu chake changu.
MI NILIACHA KILA KITU nikaondoka na moyo wangu.
Sijawahi kujutia ule uamuzi

SO USIOGOPE, u will be fine.
TULIZA KICHWA, USIPAMBANE NAE! USIJIELEZE SANA! USITAKE WATU WAKUONE HUNA MAKOSA, ANAYEONA UNA MAKOSA FRESH TU!
Focus kwenye mambo yako binafsi, taafrifa nyingine ATAWAPA YEYE!
Mkuu, ahsante sana. Mwanzoni nilivurugwa sana na hisia mchanganyiko. Hasira, huzuni, chuki, kuonewa. Nilikua nahsi kupasula kichwa bas kuna time niko ndani peke yangu na shout makelele kama chizi. Kwakwel kwa jinsi Mungu amenihurumia sijaemda milembe kipindi hiki, bas sijui tena.

Kama ulivyosema, nikawa nataman kujieleza kwa kila mtu anayetufahamu, kuonyesha namna gani yf hajanitendea haki. Kila mara nataman kuongea hisia za kuonyesha jinsi nimeonewa na huyu mama watoto tulietoka nae mbali, yeye wala hana habari ame relaaaaax.

Nikaona yote hayatanisaidia.
Nikaamua kukaa kimyaaa.

Hata janaa baada ya hukumu, sijampigia mshkaji wangu yeyote kumueleza chochote. Na mwishoni mwezi huu am planning nipotee kabisa isijulikane nilipo, nikaanze upya everything. Only circle ambayo niko nayo in biznes labda ndio tutakua in touch
 
Pole sana mkuu.
Hakika nafahamu haikuwa malengo yako ila kwakuwa mzigo mzito umeutua hilo ndo kubwa na ni jambo la kumshukuru Mungu yakuwa umelimaliza salama.

Nakumbuka niliwahi nunua mali yangu mwenyewe ili kupisha shetani kama aloathiri ndoa yako
 
Anaweza kuamua kuahirisha. Kwani unafikiri hizo siku zote zimewekwa kwa ajili ya nini?

Ndani ya hizo siku 45 mnaweza kufanya reconciliation na kutangua torati.

Mke wa rafiki yangu aliomba talaka. Wakiwa katika process za mwisho mke huyohuyo akaamua kuahirisha baada ya kupata ushauri toka jamaa na marafikii. ...
Nimekuelewa, ila kwel 45 days why nying namna hii??
 
Sema man wako alizingua, yan yeye ndio alikupeleka baraza la kata? Why? Kwann akalie lie huko ?yan mwanaume akakushtaki mwanamke??
Dunia ina mambo wewe hii.
Tulitengana, sasa akaanza kuishi na mtu.
Akarudi kuwa turudiane , nikampa masharti aondoe aliyekuwa anaishi naye.
Akasema kamuondoa, only tu kujua alitaka iwe double life as mi nilishaanzisha mji mwingine.
Nikawaka, akaniwekea mkwara wa shauri la mahakama, akijua nitarudi nyuma as si unajua tena wanawake wengi wa kitanzania na ndoa!
Mi nikakanyagia wese, wakamshauri asiendelee nikafuatwa nishuke niombe msamaha ili asinitaliki, nikawambia nyie we banaa hii ngoma iende ikienda!
nikasubiriwa nishuke, nikaaawambia lets meet mahakamani
Akapeleka shauri mahakamani ni mashtaka ya kubambika, akijua nitaona aibu tuyasuluhishe.
Nikamwambia we twende tu unachotaka na mi ndo nataka!
Mashtaka yote nikayakari,(mind you ni uongo)
Madai yote anayotaka kuhusu mali, watoto na talaka nikayaridhia.
Akajua nitasanda ndani ya siku 45, zikaisha
siku ya hukumu nikaenda na nikapokea hukumu.
nikatoka zangu pale Temeke, nikapita kula nikatafuta sehemu nikaliaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
Nkarudi nyumbani, nikaomba likizo!
Nkajiruhusu kuumia, nikalia mno ila sio kuwa najutia bali hasira ya kuonewa
Mwisho nikakubali , na maisha yanaendelea!

With no regrets,
af sio kitu sijui cha miaka 5, ilikuwa na miaka 16.
 
Nimekuelewa, ila kwel 45 days why nying namna hii??
relaaax! you need these 45 days ukiwa kwenye utulivu wa hali ya juu sana!
Wana akili kufanya hizi siku 45.
Hata akienda kutaka mchakato usitoshwe, KOMAA na msimamo!
Umia kivyako na wala asikupitishe kwenye guilty trip.
Hicho hicho anachotaka na wewe taka hicho hicho!
Utaena kuponea mbele, nimesoma kesi yako, yani yeye ndo mkosaji na kisha anakuletea mahakama!
ASEEE WE KANYAGIA WESE! hapo hapo!
 
Back
Top Bottom