Hatimae Naona Kama 1+1 = 2 Inaleta Maana

Nadhani jamaa kajieleza vizuri tu,la kwanza ni conection amekili hana ndo alikuwa anavizia ashikwe mkono.la pili muziki hautabiriki kupanda na kushuka ni kawaida kumbuka pamoja na kuwa pamoja akawa anatamba dimpoz na dai hawana kolabo na dimpoz aliamini atatoka akiwa karibu na dai so ukitafuta faida ya ukaribu wao ni wa kawaida labda nje ya muziki,la tatu naona kama umechagua unaempenda kumtetea labda tungeacha ushabiki tungesaidia kitu coz ushamuona dimpoz mkosaji mnafiki na labda hana shukrani.
 
Mkuu subiri nitulie nitaandika hapa comment ndefu sana kueleza hoja zangu..

Huyu dimpoz ni mnafiki sana na mchonganishi! Kama ningepewa fursa ya kuwashauri vijana wanaoanza muziki ningewashauri wasiige mfano wa huyu jamaa..
 
Hahahaa.... halafu nilikuwa sijaiona hii! Ukipata muda ndugu yangu; wewe sikiliza tu!!
 
Usemayo yote ni sawa na mimi ndo nimeuliza hapo ingawaje mnakwepa kujibu! Hivi kweli Diamond wa 2014 alikuwa na uwezo wa kumtafutia mtu collabo na msanii wa Marekani?! Hivi ni kweli anapaswa kulaumiwa hapa?! Si ni huyu huyu Diamond alikuwa anamuombaga JK awaunganishie na artists wa US... sasa kama alikuwa na uwezo mwenyewe kiasi cha Dimpoz kulalamika; kwanini hizo collabo hakuzifanya mwenyewe Diamond? Leo hii mtu akimlaumu Diamond kumbania collabo na Nigerians au Wa-South nitaelewa manake ana jina kubwa kwenye hizo nchi! Lakini vile vile mbona hao akina Davido na Iyanya hadi kesho wapo? Nini kinamfanya asifanye nao collabo miaka yote hii?!
 
Wadau tupo pamoja na nyinyi,mimi sitamuuliza nifah NASUBIRIA HILI JIBU maana mimi anaichukia avatar yangu kama ananijua kwa kuniona. MAANA UKIJENGA HOJA KUHUSU SHUTUMA ANAZOPEWA MOND BASI WEWE HUNA AKILI KWAKE,ILA ONGEA KWA KUMPONDA MONDI HATA PICHA YA KIKOMBE ATAKUWEKEA,JARIBUNI KUANGALIA HOJA ANAZOZIUNGA MKONO ZINAMUONGELEAJE MOND NDIO MUTAMJUA MTU HUYU.Na nawahakikishia ukiwa na tabia ya KILA MARA kumkosoa anapomponda MOND basi nanyi muda si mrefu atawanunia. ANAPANIKI KWA HARAKA SANA.
 
Mkuu kweli kabisa!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Wallah ungesema tofauti na hivi ningeshangaa sana.
Ningetilia shaka huenda anayehost ID yako ni mwingine na sio wewe.

Kwakuwa umesema bado hujasikiliza,ngoja niweke akiba ya maneno na nikupe nafasi.
Utakapoleta uchambuzi wako rasmi kuhusiana na hili nitalala na wewe mbele kama ilivyo sasa kwa chige.[emoji12]
 
Mkuu nilivyomuelewa jamaa amesema alikuwa anavizia kolabo za nje ambazo aliona dai anaweza kumshika mkono coz ye alikuwa hana uwezo,hata iyanya na davido bado asingeweza bila mkono wa dai na menejimenti yake.kushikwa mkono na kutambulishwa kuombewa kolabo na mkubwa sio sawa na kwenda front mwenyewe na exposure hakuwa nayo nilivyoelewa jamaa alijishusha akiamini atasaidiwa na haikuwa hivyo.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] ujue nimecheka sana?
Kama uyasemayo ni kweli basi amini leo hii nisingeweza hata kumquote The bold nini chige?
Hao watu tumetoka mbali, tumeparuana vibaya sana lakini nje ya hizi mada ni marafiki wazuri tu.

Hivyo ondoa shaka katika hilo.

Hivi mbona wewe umewahi kunitukana sana?Umewahi kuniambia mimi nafanya kazi reception kwenye hotel gani sijui.
Ulinichambua kana kwamba unanijua kuliko mimi nijijuavyo...lakini mbona huwa nakupa gwala katika mada nyingine?
Umesahau ambavyo huwa nakupa likes na misifa kedekede tuwapo kwenye mada za ligi kuu Tz juu ya Club yetu kipenzi Yanga?
C'mon samsun!

Kuhusu mada za namna hii...inafahamika kila mmoja wetu yuko upande gani.
Hakuna anayekubali kushindwa au kukiri pale 'boss' wake anapoteleza.
 

Chige... Umekurupuka kunijibu post yangu.Hukunisoma ukanielewa kabisa.

Collabo Marekani mimi nimeliongelea kama connection na fursa kwa pamoja.

Yooote uliyohoji nimekujibu katika post ya kwanza kabisa.

Nadhani The bold kaliona hili ndio maana ikabidi akusaidie kwa kunitwanga maswali...ngoja nimjibu.
 
Diamond ana matatizo sana huo umaarufu uchwara unamvimbisha kichwa...mpuuzi sana kuanzia leo sisikilizi tena nyimbo zake.
Labda upasue ngoma za maskio yako tofauti na hapo utasikiliza hata kwenye dala dala au mabasi ya mkoani
 

Point kubwa mnayoimiss (nadhani mnaijua ila kwa ushabiki mnajitia upofu)

Ommy Dimpoz na Diamond kwa wakati ule saga linaanza nani aliyekuwa star na connection nyingi?
Bila shaka hadi leo hii ni Diamond.
Hivyo kivyovyote Ommy alitegemea ile friends with benefits kutoka kwa Diamond.
Ndio maana hata safari ya Marekani alililia ashikwe japo mkono nae aende ili atumie safari ile kama fursa ya kupata connection.
Kilichotokea kinafahamika tayari.

Hivyo baada ya Ommy kupotezewa na ikumbukwe tayari alishapigwa bao katika collabo na Wanaija najaribu kuvivaa viatu vyake ni lazima alivunjika moyo sana.
Rafiki aliyemtegemea amshike mkono kamtosa!
Alijitahidi kujitutumua na Wanjera na nyinginezo lakini hakufua dafu.
Ikumbukwe hapo Kiba alisharejea katika kiti chake...hivyo media na attention yote ilikuwa kwa Kiba kafanya nini?
Diamond kafanya nini?
Ommy alikosa nguvu na ikumbukwe alishanyea kambi kwa Kiba pia.
(Kiufupi ni kwamba Ommy ni ile aina ya watu wasioweza kujisogeza hadi washikwe mkono)
Ndio maana ameshindwa kutoboa kama solo,kaamua ajirudi kwa Kiba kupata support.

Nadhani kwa maelezo hayo nimeua ndege wawili kwa wakati mmoja,yanajitosheleza.

Ommy ni mnafiki kiasi ndio maana hata mimi alinikera aliposhindwa kumpa support Ali Kiba aliyemtoa alipoamua kurejea katika muziki.
Nilimchukia sana.

Ila katika hili suala Diamond hawezi kukikwepa kikombe cha unafiki na roho mbaya pia.
Hapa ndio panapoleta malumbano maana mnashindwa kukiri hili ilhali liko wazi.
 
Hahahahahaha duuuuuuuhh.!!
Nimejisikia nimtag team kiba damu damu.. Cc: Nifah

[emoji23] [emoji23] [emoji23]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] design kama inatuhusu hiviiiiii?
Ila sisi tunajielewa bwana,ni kiasi cha kujua upi wakati wa 'ligi' na mengineyo.

Sina shaka katika hili.
 
Nashukuru! Umeongea point muhimu sana ambayo hawa wenzetu wanaifumbia macho.
Cheers
 
Mkuu, Diamond anaezungumziwa na Ommy Dimpoz ni wa 2014 kurudi nyuma...!! Diamond anayezungumziwa na Dimpoz ni pamoja na yule ambae watu walikuwa wanamzomea hapa JF kwamba amezamia harusi ya P Square guy hadi akatolewa nishai! Diamond anayemzungumzia Ommy Dimpoz kuhusu collabo na akina Davido hata ukaribu na Sallam hakuwa nao! Diamond anayemzungumzia Ommy Dimpoz ilibidi hata yeye mwenyewe (Diamond) aunganishiwe na akina AY ili afanye kazi na Davido na Iyanya!


Sasa anachotuambia Ommy Dimpoz; yeye alishakubaliana na Sallam (kabla hajawa meneja wa Diamond) kwamba afanye kazi na Davido! Diamond nae akawasiliana na AY, akamkutanisha na Sallam ili afanye kazi na Davido! Wakati Ommy Dimpoz aliambiwa $3000, Diamond akaambiwa $5000... Diamond akalipa na akafanya kazi!!

Hapo kabla ikumbukwe Dimpoz alishafanya kazi na J Martins kwa kubebwa bebwa hivyo hivyo... yaani for FREE na ndio maana Sallam akamkomalia kwamba collabo na Davido lazima alipie! Na ukiangalia trend vizuri; utagundua enzi hizo Ommy Dimpoz alikuwa karibu zaidi na Sallam kuliko Diamond alivyokuwa na Sallam; kwa sababu hiyo collabo ya bure, wawezeshaji ni hao akina Sallam! Na ndio maana, hata kwa Davido, Ommy Dimpoz alitajiwa pesa ndogo kuliko aliyokuwa ametajiwa Diamond!!!

Sasa ndo tunarudi kule kule...!!! Ikiwa kuna kila dalili kwamba Dimpoz alikuwa karibu sana na akina Sallam; nini kilimfanya asifanye hiyo collabo na Davido/Iyanya hata kama Diamond alifanya nao? Hivi inawezekana kweli Diamond ambae hakuwa na ukaribu wowote na akina Davido au hata Sallam bado angeweza kumbania Ommy Dimpoz? Kwani Davido/Iyanya kufanya collabo na Diamond inazuia nini Ommy nae kufanya nao? Ndo maana nikahoji; au ALISUSA au bado alitaka vya bure bure kama ilivyokuwa kwa J Martins?

Sasa baada ya hiyo remix na Davido, Diamond ndo akaanza kusikika nje... zikamtoa sana tuzo 3 za Channel O.
Pia akawa amepata nomination ya kwanza BET. Akapata nomination za kwanza AFRIMA/AFRIMMA! Sasa katika kipindi hicho ndo ambacho Dimpoz anadai alimuomba Diamond amtafutie collabo Marekani kwa madai Dai alishakuwa na connection!

Sasa hata kama wewe unafuatilia muziki ndipo nami nahoji... hivi Diamond alikuwa na jina gani 2014 hadi aweze kumtafutia mtu collabo Marekani? Na kama alikuwa na uwezo huo, mbona hata mwenyewe hakujitafutia? Jina la Diamond lilikuwa kubwa zaidi baada ya kushinda tuzo ya MTV MAMA na MTV EMA na hapo walikuwa wameshazinguana na Dimpoz kitambo!
 
Nimekurupuka wapi?! Nifah unajua vizuri sana tena sana kwamba Diamond wa 2014 hakuwa na ubavu wa kumtafutia mtu collabo Marekani na ndio maana hata mwenyewe hakuwahi kuwa na hiyo collabo! Na unajua sana kwamba there's no way ka-nomination kamoja ka BET na kengine kengine ka AFRIMMA eti ndo tayari Diamond akawa star home kwa Trump... kwanza wewe mwenyewe hapo ukishasahau tu huu mjadala hapo baadae halafu mtu aseme Diamond ni bonge la star mwenye connection kwa Mjomba Trump nitakuona utakavyoongea kinyume chake...! Aidha, unajua Diamond alipata nguvu sana baada ya kuchukua MTV... na wakati huo tayari walishakorofishana na Dimpoz kitambo!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…