Unamuonea bure JK. Kumbuka yeye ndio aliunda tume ya Warioba na akamchagua kuwa wenyekiti, hivyo alikuwa na total control ya tume. Kwa maana hiyo angataka chake ndio kiwe conclusion, angeiagiza tu tume iandike ripoti kama atakavyo yeye, na tume idai ndio maaoni ya wananchi kisha awaambie wajume waipitishe kwa nguvu moja.
Asingekuwa na sababu ya kuacha tume iandike ripoti asiyotaka halafu awapangie wajumbe cha kusema kupinga ripoti ambayo yeye alikuwa na uwezo wa kuifanya iandikwe atakavyo toka mwanzo.
Hivyo, dhamira yake ilikuwa ipatikane katiba halisi na sio ya kubumba ndio maana yeye akakaa pembeni.