Kwa hiyo kumbe tunakubaliana kuwa ndani ya ccm kuna watu wanaoaminika na wanaoweza kufanya kazi kubwa na nzuri kama uliowataja. Kwa hiyo wanaotuambia tatizo ni CCM hawako sahihi kwa mujibu wa maelezo hiyo.
Pili, unataka useme JK angetaka tume tofauti au taarifa tofauti ya tume angeshindwa?
..kila chama kina watu wazima na watu wa hovyo.
..what matters ni kundi gani kati ya hayo mawili lina sauti ya maamuzi au kauli ya mwisho ktk uendeshaji wa chama.
..kwa mfano, wakati wa awamu ya 5 wakatili na madhalimu ndani ya Ccm waliwazidi nguvu wapenda haki ndani ya chama hicho.
..Au zaidi tunaweza kusema ktk awamu ya 5 wapenda haki ndani ya Ccm hawakuwa tayari kuitetea haki, bali walijikunyata mpaka pale MOLA alipotenda yake.
..Tatizo la Ccm ni utamaduni wao wa kukijali chama chao kuliko nchi.
..Ccm kama chama kime-underperform kwa muda mrefu but somehow kwa kutumia mbinu, hila, na ujanja-ujanja kimebaki madarakani.
..Haya mazoea ya Ccm ndio tatizo kubwa la siasa zetu, na kikwazo cha demokrasi na maendeleo ya nchi yetu.
NB:
..JK alikuwa akiuma na kupuliza kuhusu suala la katiba mpya.
..ila alipoletewa rasimu ya tume ya Warioba akaamua kuuma moja kwa moja.
..Ni mwanasiasa mjanja kwasababu ameweza kusambaza lawama za kukwamisha katiba kwa bunge maalum badala ya kubeba msalaba huo peke yake.
..Ccm walikwenda ktk bunge maalum wakiwa na maelekezo ya kuvuruga na kuikwamisha rasimu na ndio waliokuwa wengi ktk bunge lile.