Hatimae sasa hoja zote za upinzani zinajibika ‘With high confidence and logic’ ikiwemo suala la Katiba

Uko sahihi mkuu, wananchi wapewe nafasi ya kupiga kura ya maoni tusonge mbele.
 
Ndugu usiyumbe sana. Tatizo kubwa ni CCM.

Cc Vessel
 
"Katiba ni maridhiano ya watu" uko sahihi kabisa. Maridhiano ya watu ndiyo hiyo "rasimu ya Warioba"

Hiyo rasimu ilitokana na maoni ya wananchi nchi nzima na ilitumia mabilioni ya pesa. Tusipoteze muda, iletwe ile rasimu tuanzie hapo.

Cc Championship
 
Uko sahihi kabisa. Kikwete alikua na dhamira njema kabisa ya kuwaachia watanzania katiba mpya na bora kabisa, kama ilivyo bora rasimu ya Warioba. Tatizo lilikuja baada ya wajumbe wa bunge la katiba wana CCM, waliona ikipita na kuwa katiba, chama chao kinaingia kaburini. Katika vikao vyao vya chama, wakamwambia JK, mzee wewe unaondoka na utabaki kuwa rais mstaafu, sisi unatuachia nini hiki!!?? Ndiyo ulikua mwanzo wa mtifuano ndani ya bunge la katiba, tukafika tulipofika.

CCM hawataki katiba mpya na hasa zaidi itakayotokana na rasimu ya Warioba.

Cc Championship
 

..JK hakutegemea kama tume italeta mapendekezo ya katiba ile, haswa serikali 3.

..alijaza watu wa Ccm katika tume akitegemea watapendeza rasimu inayolinda status quo.

..Warioba, Salim Salim, Butiku, na vigogo wengine wa Ccm ktk tume, walielemewa na maoni ya wananchi kuhusu katiba, na mwisho wakalazimika kuleta rasimu tuliyoiona.
 
Kwa hiyo kumbe tunakubaliana kuwa ndani ya ccm kuna watu wanaoaminika na wanaoweza kufanya kazi kubwa na nzuri kama uliowataja. Kwa hiyo wanaotuambia tatizo ni CCM hawako sahihi kwa mujibu wa maelezo hiyo.

Pili, unataka useme JK angetaka tume tofauti au taarifa tofauti ya tume angeshindwa?
 
Ni sawa lazima kiwe kikubwa japo tunashangaa kimekaa muda mrefu kikiwa na ukuaji duni sana. Bado kimejaa woga na kutojiamini. Kwa umri wake hakikupaswa kuzaidiwa na vyombo vya dola,kama polisi.
Pamoja na umri wake hakina tofauti na RPF cha Kagame au NRM cha Museveni vya juzi.
Kwa umri wake kisingeogopa katiba mpya,kilitegemewa kuwa kama ANC ya South Africa. Kinavizidi vyama vya upinzani miaka 27.
 

..kila chama kina watu wazima na watu wa hovyo.

..what matters ni kundi gani kati ya hayo mawili lina sauti ya maamuzi au kauli ya mwisho ktk uendeshaji wa chama.

..kwa mfano, wakati wa awamu ya 5 wakatili na madhalimu ndani ya Ccm waliwazidi nguvu wapenda haki ndani ya chama hicho.

..Au zaidi tunaweza kusema ktk awamu ya 5 wapenda haki ndani ya Ccm hawakuwa tayari kuitetea haki, bali walijikunyata mpaka pale MOLA alipotenda yake.

..Tatizo la Ccm ni utamaduni wao wa kukijali chama chao kuliko nchi.

..Ccm kama chama kime-underperform kwa muda mrefu but somehow kwa kutumia mbinu, hila, na ujanja-ujanja kimebaki madarakani.

..Haya mazoea ya Ccm ndio tatizo kubwa la siasa zetu, na kikwazo cha demokrasi na maendeleo ya nchi yetu.

NB:

..JK alikuwa akiuma na kupuliza kuhusu suala la katiba mpya.

..ila alipoletewa rasimu ya tume ya Warioba akaamua kuuma moja kwa moja.

..Ni mwanasiasa mjanja kwasababu ameweza kusambaza lawama za kukwamisha katiba kwa bunge maalum badala ya kubeba msalaba huo peke yake.

..Ccm walikwenda ktk bunge maalum wakiwa na maelekezo ya kuvuruga na kuikwamisha rasimu na ndio waliokuwa wengi ktk bunge lile.
 
Mkuu tatizo sio Ccm kama chama. Tatizo ni watu. Yaani kuna tatizo la mtu na mtu. Ndio maana mambo yalivyokuwa kipindi cha Magufuli sivyo yalivyo kipindi cha Rais Kama Samia, wakati chama ni kile kile CCM. So hatuna tatizo la chama tuna tatizo la actors.

Na jamii ikiwa na watu wengi wenye la tatizo, inatarajiwa viongozi watakuwa ni reflexion ya jamii hiyo. Sasa hivi tuna Rais bora, laini mwisho wa siku hawezi kufanikisha kila kitu peke yake.

Hivyo ni kweli kuna matatizo mengi tu lakini ni muhimu kuna source na solution sahihi badala ya coment za jumla jumla.
 
Sema kimeanza kubadilika kama tunayoyaona hayana Hila ndani yake,kutoka kuwa Chama Cha kiharamia kuelekeza kuwa Chama Cha siasa.🤔
Wakati maridhiano yakiendelea, wanakiwasha huko NCCR kupitia mtu wao THIRTY.
 
Ni sahihi
 
Azizi nakuelewa tatizo ni watu
 
M
Mkuu
Huyo thirty anapambania mageuzi au anasapoti yaliyopo!!?
Ila pia huyo 30 si mzee kijana alielelewa na chadema, sasa kaenda kufanya mapinduzi huko nccr, lawama zinaelekezwa CCM, dah!
 
Mkuu
Tambua ccm imeshikwa pabaya kuhusu KATIBA
Ishu ya KATIBA sio ajenda ya cdm pekee wala wananchi pekee bali ni agenda ya state imechoshwa na sarakasi za ccm ambazo zimeleta mtanziko mkubwa Sana HIVI karibuni state umeona wakati umefika hakuna namna ccm inajitahidi kujinasua kwenye mtego HUO lakini safari hii hakuna uchaguzi bila KATIBA MPYA
Tusubiricc
Ila pia huyo 30 si mzee kijana alielelewa na chadema, sasa kaenda kufanya mapinduzi huko nccr, lawama zinaelekezwa CCM, dah!
ccm
 
Ila pia huyo 30 si mzee kijana alielelewa na chadema, sasa kaenda kufanya mapinduzi huko nccr, lawama zinaelekezwa CCM, dah!
Kuna msemo duniani umeanza kuzoeleka Eti ''Mtu fulani amefanya dhambi kubwa Hadi SHETANI anamshagaa''

Ktk uhalisia SHETANI ndo Chanzo Cha Kila DHAMBI na UOVU wowote unaofanyika Duniani. Asiposhiriki DIRECT basi atatenda INDIRECT kupitia mfumo alioweka.

Turudi TANZANIA, mfumo wa SIASA za TANZANIA ulitoka ndani ya CCM, Kwa kila zuri au baya linalotokea Vyama vya Siasa nchini, CCM inahusika Kwa kuwa IMEJISHIKAMANISHA na Serikali.

KATIBA mpya, itatusaidia kuitenganisha CCM kuingilia mifumo yote ya utendaji wa Serikali moja Kwa moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…