Hatimae Vijana wa CHADEMA waliopewa kesi ya UBAKAJI na CCM washinda dhuluma

Ukitakata kushindana nao utaumia tu. Kwa jinsi walivyo polisi wa Tanzania, wanaweza kukubambikia kesi nyingine za kifala ukiwazingua. Ni bora tu kuendelea na maisha yako kama umeshinda kesi. Kuanzisha ligi na polisi itaku cost sana
Hawa Una deal nao kimya Kimya Tu Mmoja baada ya mwingine calmly
 
Yale MASHETANI YA CCM KWA KUTUMIA MASHETANI YA POLISI YAMEAIBIKA THOUGH KWA KUCHELEWA
Wanachama wa CHADEMA, Katala Kikaja na Ng'hulima Lilanga, wakazi wa kata ya Dutwa, Wilaya ya Bariadi, walihukumiwa kitumikia kifungo cha maisha gerezani.

Katala Kikaja na Ng'hulima Lilanga walikuwa mawakala wa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA katika jimbo la Bariadi, kamanda Benard Makoye Maendeleo

27.10.2020 kama wengine, walipokea vitisho wasiende kusimamia kura za CHADEMA katika vituo vya uchaguzi. Wao wakaamua kupuuza vitisho hivyo.

28.10.2020 wakawahi katika vituo vya kupiga kura kama mawakala wa CHADEMA. Dutwa A na Dutwa B. Wakaelezwa mawakala wamezuiwa wasiingie.

Wakaendelea kubaki ndani ya vituo vya kupiga kura wakisubiri zoezi la kupiga kura lianze. Ghafla wakaingia askari polisi. Wakatumia nguvu kuwakamata wote.

Wakapelekwa kituo cha polisi bila kuelezaa makosa waliyopewa. Uchaguzi ukafanyika. Matokeo ya uchaguzi yakatangazea wakiwa wapo mahabusu ya Polisi.

Mwezi mmoja baadae wakapandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu kwa tuhuma za ubakaji na unyang’anyi wa kutumia silaha. Wakashangaa sana.

Hati ya mashtaka inaeleza alfajiri 28.10.2020 katika kituo cha kupiga kura walimkuta msimamizi msaidizi wa uchaguzi ambaye walimbaka kwa zamu.

Baada ya kumbaka wakampora pesa taslimu TZS 300,000/- na baada ya kufanya hivyo wakaendelea kubaki kituo cha kupiga kura kama MAWAKALA.

Hati ya mashtaka bila kumtaja huyo mtu aliyebakwa na hakuwahi kuitwa mahakamani kutoa ushahidi, aliwasilisha ushahidi wake kwa njia ya maandishi.

Mahakama ikaeleza kwamba hiyo ni kulinda UTU wa shahidi huyo wa upande wa Jamhuri. Mahakama ikawakuta na hatia na kuwakuhumu kifungo cha maisha

Tangu 28.10.2020 wanahamishwa magereza ya mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mwanza. 12 April 2022 wakahukumiwa kutumikia kifungo cha maisha gerezani

Uongozi wa CHADEMA kanda ya Serengeti walikata rufaa baada ya hukumu hiyo ya kihuni iliyowatia hatiani makamanda Katala Kikaja na Ng'hulima Lilanga

Waliamua kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, kanda ya Shinyanga. Nitakupitisha katika hukumu, ujionee JAMHURI ilivyokuwa HOVYO.

Jaji Athumani Matuma akisoma uamuzi wa Mahakama ya Rufani anasema upande wa mashtaka (Jamhuri) walifanya jitihada kubwa za kuficha taarifa zote.

Kwamba warufani (washtakiwa) walikuwa mawakala wa CHADEMA katika kata ya Dutwa iliyopo katika Jimbo la Bariadi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020

Jaji Athumani Matuma anasema hoja za Mawakili wa upande wa utetezi (mawakili wa washtakiwa zote zina Mashiko). Amezipitia na kuziona zimebeba misingi.

Jaji Athumani Matuma anasisitiza, Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu aliyesikiliza shauri hili hatua za awali, hakufuatilia Ushahidi kwa kina,

Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu aliamua kuwatia hatiani Watuhumiwa hao wawili kwa ushahidi wenye kutia shaka. Ushahidi usiothibitika.

Ushahidi wa upande wa utetezi kutoka kwa aliyekuwa mgombea udiwani wa CHADEMA, ulionyesha mshtakiwa namba 1 alikuwa kituo cha kupiga kura.

Mshtakiwa namba 2 alikuwa dereva wa mgombea udiwani katika uchaguzi huo. Hoja zote zilifichwa na Upande wa Jamhuri, kwa maelezo ya hukumu ya Jaji.

Jaji Athumani Matuma anasema mazingira ya kesi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu ilitakiwa kutambua kwa kina ushahidi wa Watuhumiwa, bila kupuuza.

Hususani kwa kuzingatia ilikuwa usiku. Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu hakuelekeza akili yake sawa sawa kwenye utoaji wa hukumu hiyo.

Upande wa mashtaka walipaswa kumleta msimamizi wa uchaguzi (returning officer) kuthibitisha kama kweli matukio hayo tajwa (ubakaji na uporaji) yalitokea.

Upande wa mashtaka hawakumleta msimamizi wa uchanguzi. Msimamizi wa uchaguzi alikuwa ni shahidi muhimu katika kesi hii, hakuletwa Mahakamani.

Msimamizi wa uchaguzi alikuwa lazima atoe ushahidi kwa kuwa kulikuwa na upotevu wa vifaa vya uchaguzi kwa mujibu wa taarifa yao ya upelelezi.

Hakuna ofisa yeyote wa Polisi aliitwa na kufika Mahakamani kuthibitisha kama kweli kuna tukio la wizi wa vifaa vya kupiga kura lilitokea katika kituo hicho.

Kutoitwa Afisa wa Polisi yeyote kutoa ushahidi Mahakaman katika shauri hili, kunafanya hata ushahidi mwingine wowote kutoaminika na kukosa nguvu.

Nani ambaye alithibitisha kwamba kulitokea wizi wa vifaa vya tume ya taifa ya uchaguzi na uporaji wa fedha kama Polisi hajafika? Afisa gani wa polisi alipeleleza?

Jaji Athumani Matuma anasema, katika hali ya kushangaza upande wa mashtaka walimkataa shahidi Pili Masunga ambaye alikuwa shahidi wao muhimu.

Na wao (upande wa mashtaka) walishindwa kumleta mahakamani na baadae washtakiwa walimleta kuwa shahidi upande wao, lakini alikataliwa na Jamhuri.

Jaji Athumani Matuma anaendelea kusoma uamuzi akisema, kushindwa kuwaleta mashahidi muhimu ni jambo baya katika ushahidi wa mashtaka ya Jinai.

Shahidi Pili Masunga alikataa kwanba hakuna tukio lililotokea nyumbani kwake ambapo walalamikaji walisema matukio yalifanyika nyumbani kwa Masunga.

Jaji Athumani Matuma anasema, upande wa mashtaka (Jamhuri) walishindwa kuleta na kuwasilisha mashahidi na ushahidi wao muhimu mbele ya Mahakama.

Walifanya kila linalowezekana kuzuia washtakiwa na mashahidi wao kutoa ushahidi Mahakamani. Jaji akakemea vikali sana tabia hii mbaya ya Jamhuri.

Jaji anasema utambuzi wa ubakaji ulifanyika nyumbani kwa Pili Masunga kwanini Jamhuri hawakumleta Pili Masunga kutoa ushahidi kama shahidi wao muhimu?

Jaji Athumani Matuma anasema ushahidi wa Jamhuri uliosalia Mahakamani, kamwe hauwezi kuwatia hatiani washtakiwa kwa tuhuma za ubakaji na uporaji.

Jaji Athumani Matuma anaamua kufutilia mbali ushahidi wote wa Jamhuri na anaamuru washtakiwa wote waachiwe huru mara moja kwa amri ya Mahakama.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kanda ya Shinyanga, Athumani Matuma ameacha 'precedent' nzuri, itatumika kama rejea kwa kesi za mchongo.

Watu wetu wanakamatwa, wanashtakiwa kwa makosa ya uongo, wanaishi gerezani kwa makosa ya kusingiziwa wakati wa uchaguzi. Nchi nzima. Hatari.

Ndiyo maana nafikiri tukipata REFORMS itasaidia kuwalinda watu wetu dhidi ya makosa ya kuzusha na uongo wakati wa uchaguzi #noreformsnoelection.View attachment 3305894

Dhulma mbaya sana
 
DU hii ni hatari hayo tumeyajua je yapo mangapi yamefanyika na hatujayajua, MNAPO LETA HABARI HIZI MUWE MNAMTAJA NA HAKIMU ALIYEFANYA UNYAMA HUO, P sema neno
Ili uonekane ujinga wake huyonHakimu!
 
Kwa hiyo hizi Mahakama tuziamini au bado zinaendeshwa na serikali?
 
Hawa Una deal nao kimya Kimya Tu Mmoja baada ya mwingine calmly
Naona it only language they will understand kwa maumiv wanao sababishia watu.
And watawala they wonder waasi waanzaje? Sindio kwa mambo kama hayo ya kuchelewesha justice au ku temper na mifumo ya kutoa haki
 
Miaka mitano unamfunga mtu kwa kesi ya uongo, mbwa hawa! Kisha huko bungeni mnaanza Bunge kwa kusali, Hawa jamaa hawajui kuwa MUNGU hadhihakiwi!
 
Kwa hiyo hizi Mahakama tuziamini au bado zinaendeshwa na serikali?
Swali la kipumbavu mno Ndugu yangu, soma huo mtiririko then jiweke kwenye position yao, hao ni watoto wa Watanzania wenzetu, imagine hao Ndio ingekua Ndugu zako, then jiulize hilo swali.
 
Ujinga huu ndio maana tunataka Rais apunguziwe madaraka kuwepo na sheria kali hasa. Huyu Hakimu mungu amlaani yeye na kizazi chake. Sintoshiriki uchaguzi.
 
Miaka mitano unamfunga mtu kwa kesi ya uongo, mbwa hawa! Kisha huko bungeni mnaanza Bunge kwa kusali, Hawa jamaa hawajui kuwa MUNGU hadhihakiwi!
At this point Mungu si relevant kwao tena. Pla eni kutimiza tu ratiba za bunge ila most of them dont care

Tumefikaje hapa? Wananchi wenyewe wameruhusu.
 
Angalia MTU kama huyu, anajua mengi Sana kuhusu walipo Ndugu zetu
 
Ukitakata kushindana nao utaumia tu. Kwa jinsi walivyo polisi wa Tanzania, wanaweza kukubambikia kesi nyingine za kifala ukiwazingua. Ni bora tu kuendelea na maisha yako kama umeshinda kesi. Kuanzisha ligi na polisi itaku cost sana
Mkuu nakuelewa ila tukiendelea na mentality hiyo uonevu utaendelea. Lazima wajulikane na kuandikwa majina yao kwenye kumbukumbu zetu na kuwaambia watoto na vijana wetu uzalimu tuliofanyiwa ili siku hao waovu wakizeeka au wakistaafu hata tusipokuwepo watashughulikiwa kimya kimya vizazi vyetu.
 
Back
Top Bottom