barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,880
Chopa hiyo itaanza kutumika kwenye nusu ya pili ya harakati za kampeni kuelekea October 28,chopa hiyo yenye usajili wa 5Y-HSN imekodiwa toka nchini Kenya kwa mmoja wa wanasiasa na mfanyabiashara maarufu Ndugu Simeon Nyachae.
Simon Nyachae, mwanasiasa wa County ya Kisii nchini Kenya, ni rafiki na mshirika pia wa Rais Magufuli, kwani hapo awali wakati wa Utawala wa Mwai Kibaki, Nyachae aliwahi kuhudumu kama Waziri wa barabara.
Wakati Muungano wa Rais Kibaki wa NARC ulipoanza kudhoofika kwenye uungwaji mkono, chama cha FORD-People cha Nyachae kikajiunga naye, na rais Mwai Kibaki akamteua Nyachae kama Waziri wa Nishati na baadae akampa kuwa waziri wa Barabara.
Nyachae alitajwa katika ripoti ya Waki kama mmoja wa wahusika wa vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007-2008 ambapo zaidi ya watu 1,600 walifariki.
Aliaminika kupanga mashambulizi dhidi ya viongozi wa upinzani wa ODM.
Aligombea na kupoteza uchaguzi wa ubunge wa mwaka 2007.