Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

Uwanja umeshajengwa, mvimbe mpasuke mtajijua wenyewe.

Watetea mafisadi na wabaguzi wakubwa nyinyi( malofa)
Ukiyaja kujua ufahami wetu watz ni ea sija gani basi soma mawazo ya huyu mwasita kama siyo mwasaba. haiingii akilini mtu katoa uchambuzi wa kitaalamu nawe baada ya kujibu kitaalamu unajibu kifenengefenenge. taifa ili kuna mambo yanaudhi. mtu anatoa hoja nzuri na si mwanachama wa chama chochote, basi kwa kuwa anampinga mkuu basi huyo utaambiwa si mwanaccm bali mpinzani. akiandika jambo muislam lenye mashiko basi mkiristo anasema huyu lazima ni muislam. akiandika uchambuzi mzuri ka huu na yawezekana mr barafu anatoke chato, utasikia huyu ni wa kasikazini. kama taifa kea style hii hatutafika. uwanja huu hauna manufaa.kutoka bukoba to chato ni zaidi ya km 130, geita ni kama km >100, bihalamulo ni km 100, ngara, >200, kahama 250 nk. ni watu gani watatumia uwanja huu tofauti na mtukufu?
 
Uwanja umeshajengwa, mvimbe mpasuke mtajijua wenyewe.

Watetea mafisadi na wabaguzi wakubwa nyinyi( malofa)
Ukiyaja kujua ufahami wetu watz ni wa aina gani basi soma mawazo ya huyu mwasita kama siyo mwasaba. haiingii akilini mtu katoa uchambuzi wa kitaalamu nawe baada ya kujibu kitaalamu unajibu kifenengefenenge. taifa ili kuna mambo yanaudhi. mtu anatoa hoja nzuri na si mwanachama wa chama chochote, basi kwa kuwa anampinga mkuu basi huyo utaambiwa si mwanaccm bali mpinzani. akiandika jambo muislam lenye mashiko basi mkiristo anasema huyu lazima ni muislam alkadharika kama muandishi ni mkiristo utasikia muislam anasema huyu si mwenzetu. mtu akiandika uchambuzi mzuri ka huu na yawezekana mr barafu anatoke chato, utasikia huyu ni wa kasikazini. kama taifa kwa style hii hatutafika. uwanja huu hauna manufaa. kutoka bukoba to chato ni zaidi ya km 130, geita ni kama km >100, bihalamulo ni km 100, ngara, >200, kahama 250 nk. ni watu gani watatumia uwanja huu tofauti na mtukufu?
 
Kwani bajeti ya huo uwanja ni shilingi ngapi?

I wish I could cry! Kuko wapi kumu enzi Baba wa Taifa Mwl. Nyerere(RIP) kwa Viongozi uchwara wa CCM?
Baba wa Taifa alikaa Ikulu zaidi ya miongo 2! Leo JPM ana mwaka tu tayari anajenga International Airport kwao! This is ridiculous.Baba wa Taifa hakuwahi kufanya ujinga kama huu! Hatuoni Kiwanja CHA NDEGE CHA KIMATAIFA PALE BUTIAMA wala MUSOMA yenyewe!
Je, Magufuli anafikiria nini huko mbele kwa muktadha huu?Je, yawezekana ni dalili ya kuanza kuweka mazingira ya kuitawala Tanzania kwa miaka mingi ijayo kama dikteta?
 
***
WAZEE WA CHAMA WANALO JIBU LAKE.....!/
*wafanyaje 2020, kabla jambo halija zua jambo.
 
Mleta mada ameongelea umuhimu wa ujenzi wa uwanja wa kuhudumia mbuga ya serengeti. Na akapendekeza uwanja wa mwanza. Na hapo ndipo nimetofautiana naye. Wewe hili unaliongeleaje?

Mleta mada ametia sababu dhaifu ya idadi ya watu kuwa ndiyo hoja yake ya kutojenga kiwanja chato inaposimamia. Ndiyo maana nikamuuliza wakati KIA inajengwa kulikuwa na wakaazi wangapi BOMANG'OMBE.
 
Ili la CHATO on a serious note mwenzenu nimekwazwa maana naangalia faida zake kwa uchumi wa Tz bado naona Nyota.
Anyway naendelea kusoma maoni ya wadau labda mishowe ntakuja kuwa convinced uwepo wa iki kiwanja.
Nakubaliana na wadau kuwa uwanja karibu na Serengeti NP ni jambo la muhimu mno ukizingatia tuko na mabombadia then boing 787 izi mbuga plus Ruaha NP lazima tuzitengnezee mazingira utalii wetu ukue
 
Kwa taarifa tu mkuu, kuboreshwa kwa Uwanja wa Mwanza lilikuwa wazo miaka ya 80 wakati waziri wa maliasili na utalii akiwa Jetrude Mongela- Wakaskazini wote ndani ya utumishi wa serkali na Umma wakaupinga na kuhakikisha kuwa Mongela anaongolewa wizarani hapo na KIA ikajengwa badala yake. Sasa leo hao hao wa KASKAZINI wanakuja na oho CHATO huu ni muendelezo wa siasa za kuchafuana, uchanguzi wa 2015, na maandalizi ya uchaguzi wa 2020. Kutesa kwa zamu- wacha kanda ya ziwa nao watese- na wanahasira na KASKAZINI
 

Ndugu yangu Eudorite,
Hivi barafu anaupigia chapuo Uwanja wa Mwanza au alichosema ni kwamba, ikiwa hapakuwa na namna ya kujenga Serengeti basi option ingekuwa ni kujenga Mwanza badala ya Chato! Sehemu ya thread yake ni hii: Ingawaje umeleta habari za ukanda; nitangulie kusema kwamba, binafsi sina maslahi yoyote ama iwe na Kanda ya Kaskazini ambayo hamuishi kuisemanga na wala kanda ya Ziwa!

But on top of that, sina hata maslahi kwenye siasa za upinzani haidhuru hata kama wengine wanaweza kuona hivyo kwavile huwa napinga mambo mengi. Hata hizo Bombadier ambazo ndugu yangu barafu anaziunga mkono; mimi nimeanza kuzipinga since Day 1 na nitaendelea kuzipinga japo kwa sasa! Na si hivyo tu, nilianza kupinga ununuzi wa ndege tangia enzi za JK!!!!

Lakini pamoja na yote hayo, barafu yupo sahihi kwa 100%.

Kama umemsoma vizuri best option kwake ni Serengeti and not Mwanza!

Lakini ikiwa hapana namna ya kujenga Uwanja wa Serengeti, basi best option kwa sasa ni Mwanza kwa sababu ndio shortest economical distance to Serengeti lakini sio Chato unless kama unataka kutuambia ni rahisi zaidi kufika Serengenti kutokea Chato kuliko kutokea Mwanza!

That's one but second, hata kama ingekuwa ni rahisi zaidi kufika Serengeti kutokea Chato kuliko Mwanza; bado hiyo peke yake haiwezi kuwa decisive criteria ya kufikia maamuzi ya kuchagua Chato badala ya Mwanza!

Moja ya mambo ambayo wachumi watahoji; is Chato economically viable compared to Mwanza? Kwamba, fine... ni rahisi Watalii kutokea Chato kuliko Mwanza... ni hilo tu?! Watalii wana msimu wake... je, wakati wa offseason uwanja utaendelea kutumika?!

Hapo nimejaribu kuupendelea Uwanja wa Chato kwamba utakuwa unahudumia watalii (you know it's impractical) lakini pamoja na yote hayo, bado tunaona hatari ya kuwa underutilized wakati wa offseason.

Ukweli huo hapo juu ndio unajibu hoja yako kwamba huoni ni kwanini Uwanja usijengwe Chato! Sababu ni moja tu, Chato hawana uchumi wa ku-utilize international airport throughout the year! As of now, Chato Airport haiwezi kuendeshwa economically... NO WAY!

I hate to say this but ukweli ni kwamba, ingawaje Chato Airport is too big even to kule kwetu Mafia; lakini ni bora Mafia ungeweza kutumika throughout the year hata kama ungetumiwa na ndege ndogo compared to Chato!!
 
Aah bora angetokea kwetu tungepata hata kauwanja maaana!!!!!
 
Tutakifanya kiwe ni kiwanja pekee kwa kusafirisha organic food zote, mboga za majani, maua holtculture kwa ujumla na minofu ya samaki yote iendayo abroad. Na mambo mengine yote ya kuingizia taifa pesa
 
Sawa bwana lakini Musoma tuna uwanja mzuri tu.nimekusoma tu.
 
Najiuliza kwanini tumekataa majina yetu tukakubali ya wazungu na waarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…