Hoja hii inatokana na mapungufu ya kutafuta habari kwa kina
Tulijadili sana hapa JF kwaini KIA ilijengwa.
Mpango wa pili wa maendeleo 1964-1969. Tazama sababu za ujenzi wa kiwanja hicho na historia yake
Ni fair point, usiishie hapo tueleze kwa ukubwa unaotarajiwa nini faida za ujenzi wa uwanja huo? Hicho ndicho muhimu kujadili hapa
Tunarudi pale pale, kuwekeza lazima kuwe na sababu.
Hautuwezi kuwekeza kiwanja kikubwa Segera bila sababu.
Hakuna kashfa ya Chato, kinachohojiwa ni sababu nzuri tu ziwe za kiuchumi, kijamii au kiusalama. Tunaomba msaada wa hiloHakuna tatizo kabisa.
Korogwe ilikuwa council wakati wa Mkoloni.
Ni Moja ya Wilaya kongwe katika taifa hili haina Kiwanja.
Tunduru ni Wilaya Kongwe katika Taifa hili, kiwanja chake ni airstrip tu
Hatuhitaji kiwanja nyumbani Bondei- Muheza kwasababu ni saa 1 kutoka Pongwe Tanga
Hatuhitaji Kiwanja Kisarawe kwasababu ni saa 1 kutoka JNIA
Hatuhitaji likiwanja likubwa Mkuranga na Nyamato kwasababu ni saa 1 kufika JNIA
Tunahitaji kuwekeza kwa malengo.
Hatuhitaji uwanja mkubwa Kigoma, tunahitaji Reli ya STG na daraja la maragarasi kwasababu kiuchumi ina maana sana.
Hoja yako kuwa kila Wilaya iwe na kiwanja ni mfu.
Hatuhitaji kiwanja Kibaha na ni ujinga uliotukuka kuwekeza tu likiwanja kwasababu baada ya miaka 20 litakuwa na faida
Ni akili pevu kama fedha hizo zitajenga reli ya Mtwara-Liganga
Hatuhitaji likiwanja likuubwa Wilaya ya Butiama ili watumiaji 6 watumie.
Tunahitaji fedha hizo kujenga reli ya kuunganisha Musoma na Mwanza
Inatosha Ningemuomba JPM na serikali yake wafikirie kuunganisha reli ya kati ifike Musoma
Uwanja wa Musoma ulikuwa kama airstrip wakati huo EA Airways DC ikitua.
Niliona kwa macho yangu wakati mkuu wa mkoa akiwa Kisoki kama si Wasira na Mkurgenzi akiwa Marehemu Khalidi aliyejenga Makondeko.
Ndege ziliposhindwa kutua mkandarasi aliyeweka 'moram' ni P.F.Nyakutonya
Hii Jet ya Rais ilifanyiwa majaribio baada ya uwanja kukamilika.
Mgeni wa kwanza kutua alikuwa Chancellor wa Ujerumani Wilbrandt akimtembelea Nyerere Butiama
Nyerere hakukifiri njia nzuri ni kujenga kiwanja kikubwa.
Mahitaji ya watu wa Mara yalikuwa Daraja la Kirumi lililojengwa na Maulidad & Rose.
Matete yalibomoa kwanza,niliona nikitoka Kinesi, niliogopa boti za Hosea na maji
Tukapita pale Kirumi kwa kivuko ambacho kilikuwa ni hatari
Daraja la Kirumi lilitumika na KAMATA na Tanganyika Bus wakati yanapitia Kenya kwenda Mwanza. Barabara ya kati ilikuwa haipitiki kwa baadhi ya nyakati
Kirumi ni kiungo kizuri hadi sasa kati ya Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda
Huo ndio uwekezaji wenye tija.
Nyerere angeweza kujenga uwanja Butiama mkubwa tu.
Alifikiria Taifa kwanza na si yeye kama mtu
Hapa niwaalike wakubwa tutete ya enzi
Jasusi na
JokaKuu