Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

Hii sijui niite .Chato ina economical potential ipi zaidi ya wasukuma wenye baiskeli ya phonex..tatzo hii serikali kama arsenal..hawana form..wanafanya jambo moja zuri linafuatiwa mambo saba ya kipumbavu kuwahi kutokea.


Hii imeniudhi kwakwli..
Zuri ni lipi ?
 
Nyuma ya pazia huu uwanja wa ndege utatuinua kiutalii sisi wa kanda ya ziwa magharibi
 
Chato International Airport ni project ya hovyo hovyo iliyo fanywa kwa kumuogopa Rais Magufuli
Why ilijengwa chato wakati mwanza kuna airport?
Ukianhalia kitaalam it doesnt make sence...

Inaonekana kuna mihemko ya mtu fulan kutaka kuwajengea wananchi wake airport wakati hao hao wananchi wenyewe ni asilimia ndogo sana wenye uwezo wa kupanda ndege. Sana sana watakuwa wanapiga picha tu
 
Majungu tu, kwani chato wanakaa nyani? Kwani lazima ndege zote wapande watalii? Hacheni ubwe.ge kwani chato ipo sudan?
Wanja wa ndege unajengwa sehem inauoonekana inaingizia nchi pato kubwa. Angalia viwanja vya ndege vingi nchini... vipo pale sababu kuna vichocheo vya kibiashara...

Unaenda kujenga uwanja wa ndege chato, sawa, kuna vichocheo gani pale? Haya itasema ni watu..

Kwa jamii iyoishi chato, wenye uwezo wa kupanda ndege ni wachache mno.. wengine watakuwa wanaziangalia tu.
Be wise man... dont be dumb
 
Lini hii airport yetu pendwa itafunguliwa?

Nani atakuwa mgeni rasmi siku hiyo?

Naomba siku ya ufunguzi, tupewe mapumzuko ili kusudi tupate muda wa kutosha wa kufatilia na kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
 
Sasa ni dhahiri kuwa, kuanzia mwezi Aprili katika mapumziko ya Pasaka, Mkuu wetu atakuwa na uhakika wa kwenda mapumzikoni kwa kutumia uwanja wa ndege mpya wa Chato, yaani Chato Airport.

Kwa sasa uwanja huo unaotegemewa kukamilika mwanzoni mwa mwezi Aprili upo ktk kiwango cha vumbi na unaendelea kufanyiwa matengenezo hadi kiwango cha lami. Tayari ndege ndogo aina ya Beech Craft(King Air) mali ya kampuni binafsi ya TanzanAir imetua kwa mara ya kwanza ktk uwanja wa ndege wa Chato na hivyo kutoa uhakika kuwa sasa Chato inaenda kupokea ndege bila wasiwasi wowote.

Kwa mujibu wa taarifa,uwanja huo una kiwango cha "Aerodrome Reference Code 4D". Hizi "codes" hutolewa na ICAO (International Civil Aviation Organization) kulingana na ubora wa kiwanja kwa kuangalia aina ya ndege zinazoweza kutua, ukubwa wa ndege kwa maana ya uzito na upana wa mabawa.

Codes hizi zipo kuanzia 1A hadi 4F. Hivyo kwa kiwanja kuwa na Code 4D maana yake kimebakiza Code mbili tu kufikia kiwango cha mwisho cha ubora wa viwanja unaotambulika na ICAO.Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere "Code" yake ni 4E, hivyo uwanja wa Chato upo nyuma ya JNIA kwa "code letter" moja lakini upo sawa kwa "Code number" na JNIA kwa sababu vyote vipo kwenye "Code number 4".

Mfululizo wa "Aerodrome Reference Codes" huanza na 1A, 2B, 3C, 4D, 4E, 4F. Hivyo ni hakika sasa Chato Airport kwa kuwa na "Code 4D" inaenda kuwa moja kati ya viwanja vitatu venye kiwango bora Tanzania ikikaa nyuma ya Julius Nyerere na KIA. Uwanja wa Mwanza ni "Code 4D" hadi hapo ukarabati utakapokamilika utakuwa na sifa ya "Code 4E".

Hatuididimizi dhamira ya Mkuu kujenga kiwanja chenye ubora Chato, bali tunahoji kwa uelewa mdogo tu wa kanuni za Uchumi. Kwamba kiwanja hiki huko Chato kinaweza kuwa na matokeo chanya ya kiuchumi kama ambavyo wangeweza kuboresha uwanja wa ndege wa Mwanza?

Tunauhitaji Uwanja wa Mwanza kuliko ule wa Chato kwa sababu za kiuchumi ktk sekta ya Utalii. Tumekuwa tukilalamika sana kwa mbuga yetu ya Serengeti kukosa watalii wa kutosha kisa njia za usafiri kufika huko zilivyokuwa duni kushinda majirani zetu tunaopakana na mbuga ya Maasai Mara.

Uwanja pekee unaohudumia mbuga ya Serengeti kwa njia ya anga ni "Seronera Aistrip" ambapo huwa busy sana na huchukua ndege ndogo zenye abiria wasiozidi 50. Hii ndio moja kati ya "busiest Airstrip" kwa Tanzania.

Ili ufike Serengeti kupitia uwanja wa KIA unahitaji kutembea kilomita 284 kwa gari toka uwanjani, kwa kupitia uwanja wa ndege wa Arusha inakupasa utembee kwa gari umbali wa kama kilomita 226 wakati kwa kupitia Uwanja wa Mwanza,mtalii anatembea kilomita 166 hadi kufika geti la Ndabaka(?).

Kwa mahesabu hayo,kama ujenzi wa Uwanja wa ndege Serengeti ulishindikana,basi Uwanja wa ndege wa Mwanza ndio suluhisho la haraka ktk kuwafikisha watalii kwa urahisi ktk mbuga hiyo.Tukiusahau uwanja huo na kutazama zaidi ule wa Chato, tunaweza kuhoji dhamira hii ya maendeleo ktk kufika uchumi wa kati. Na kuhoji kwetu kusiababishe "hasira" kwa wenye mamlaka, bali ichukuliwe ni kama changamoto za raia kwa serikali yao.

Ukisefu wa usafiri wa uhakika na hasa ule wa njia ya anga, ndio unatukosesha mapato na kupunguza idadi wa Watalii ktk mbuga yetu ya Serengeti na hivyo wengi kuishia Maasai Mara.

Licha ya kuwa Serengeti ina ukubwa mara sita ya Maasai Mara,lakini bado "Vitanda" vya kupokea watalii katika hotel za Serengeti hivizidi 970 wakati wenzetu Maasai Mara ktk mbuga yao, kuna "Vitanda" zaidi ya 4,700. Hakika kupanga ni kuchagua.

Mpaka sasa Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania inamiliki viwanja vya ndege 58(ukijumlisha na Chato itakuwa 59),na wakati Uwanja wa ndege wa KIA ukiwa mikononi mwa Kampuni ya KADCO. TANAPA inamiliki karibu viwanja 26(Vingi vikiwa ni Airstrips),NCAA 2 na viwanja binafsi 93.

Katika hivi vya binafsi,vingi vinamilikiwa na wawekezaji toka nje ambao huvitumia kufanya udanganyifu ktk maliasili zetu.Uwanja wa ndege wa mgodi wa Geita(Mchauru) na Uwanja wa ndege wa Tishwa(HTSW) kule Loliondo unaomilikiwa na mtoto wa mfalme wa UAE ni moja kati ya viwanja vinavyopswa kutazamwa vizuri na serikali hii.

Uwanja huu wa Tishwa Loliondo ndio "unatisha", kwani huku ndege za familia ya mfalme hushuka moja kwa moja na kunyanyuka na mali nyingi. Umejengwa kiasi cha kuweza kutua na kuruka ndege kubwa.

Huu ndio uwanja ulio ktk eneo ambapo ukifika na kuwasha simu unakutana na meseji inasema "Dear Guest,Welcome to the UAE.Enjoy the best network coverage and other unmatched services only with Etisalat.Please use <+> or <00> before the country code for international calls.For directory services call 181,for availability of GPRS,MMS 3G roaming services call Etisalat Travellers help line 8002300 & for inquiries on Tourism,entertainment,shopping,etc call 7000-1-7000(Roaming rates apply).Have a pleasant stay in the UAE"

Labda wengine hatuna utaalamu wa Telecomunication, lkn kweli inawezakana hii kitu iingie tu kwenye simu yako wakati hujafanya "roaming". Haya ndio mambo ya TCRA kututoa tongotongo, sio zile mambo zao za .co.tz

Tunatakiwa tuwekeze ktk usafiri wa anga,lakini tuwekeza kimkakati na kwa faida za uchumi wa pamoja kama Taifa.Tukipewa sababu za kiuchumi zinazoupeleka uwanja wa ndege Chato wenye "Aerodrome Reference Code 4D" hatutakuwa na maswali.Tusipapata majibu yenye faida za kiuchumi,tutaendelea kuhoji hata tukiwa mafichoni.

Tukumbusha umuhimu wa Mwanza ktk kuihudumia Serengeti National Park, tutawakumbusha kuwa mlikuwa na mradi wa kujenge Uwanja wa ndege Serengeti,ila mkapambana na wanaharakati wa Ikolojia. Uwanja wa Serengeti ulipaswa kujengwa kati wa Kiwanja cha Ndege pale Mgumu.

Serengeti International Airport ilikuwa ni Code 4F, ilipaswa kuwa na runway ya mita 3,800 hadi mita 4,200.Mradi huo ulififia,sasa "tumefufukia" Chato na Uwanja wa "Code 4D".Je huku ndio kupanga na kuchagua??

Wakuu ukiyatafakari sana mambo ya nchi hii unaweza kuwa kichaa. Tuishukuru [HASHTAG]#Jamiiforums[/HASHTAG], inatupa wasaa wa kuhoji haya nyuma ya "keyboard". Mambo haya enzi za Waziri wa Maliasili Aboubakari Mgumia yaliondoa maisha ya Ndugu Stan Katabaro. Tunapouanza mwaka mpya, tuzame katika sala na maombi. Ili wale wanaoomba tuwaombee kila siku,tusiwaombee tu wawe na afya njema..Bali walegeze mioyo ktk kuishughulikia mitandao kama mtandao wetu pendwa wa [HASHTAG]#Jamiiforums[/HASHTAG].

Nawatakia Mwaka Mpya mwema. Ninafunga mwaka na "Chato Interantional Airport".... Panapo majaliwa hapo mwakani. Nitakuwa likizo huko kwetu porini.... Ciaoooo!!!!
CHATO IS WHITE ELEPHANT PROJECT
 
Kipigi,

Wengine hatuongozwi na itikadi yoyote,ndio maana tunasifia na kutoa changamoto kwa nia njema.

Tulishangilia ujio wa Pangoboi katikati ya matusi na kashfa tele...Wakati huo hukutuona kama "wa kaskazini"!!Sasa tunahoji kwa staha na kwa nia njema unaamua kutupakazia "ukanda"

Mbona wengine hatutoki huko ulikokutaja?Hivi nani wa kuwekewa mshangao?Wewe unayeandika lugha ya kibaguzi au sisi tunaotoa changamoto?

Jenga hoja bila hisia za ukabila na ukada...Wengine hizo hatua tulishazipita!!Ndio maana tunapongeza na kukosoa kwa staha na nidhamu... Jifungue ktk minyororo ya ukada na ukanda, Utakuwa huru kiakili na kifikra
Mbona faida za kuwepo uwanja wa Chato zimezungumzwa mara kadhaa humu JF?
 
Chato inajengwa airstrip ya kawaida kabisa kama iliyopo seronera kule Serengeti.

Kule chato ni karibu kabisa na Rubondo island national park, kuna umuhimu mkubwa kabisa wa kuwa na uwanja huo.

SERA ZIMEKOSEKANA UKAWA.
sasa imebaki kukaa kwenye ofisi na kuchambua hotuba za magufuli.
Then mnakuja na utumbo wenu kila uchao...shame on all of you!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom