Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili


Sio tu kulewa madaraka ila wamelewa mbenge , hivi chato na Geita wapi kumeendelea na kuna kuwa kwa haraka? hata kasamwa ni better kuliko chato, kwa nini tusiangalie walau eneo karibu na Geita tukajenga huo uwanja to boost and rapid growth of Geita region? kama tu mini-Bus zenye abilia 23 haziwezi kujaza abiria kutoka chato iweje kwa ndenge? tuweni na vipaumbele kama Taifa, tujenge viwanja hivi kulingana na mahitaji ya kiuchumi Tanzania sio mahitaji ya kikanda ,mfano wadau wengi wanadai Serengeti ndio hitaji kuu sasa hivi basi nguvu ya chato ilitakiwa ihamishiwe Musoma/Tarime/Mwanza nk.
 
Ni ujinga na upumbavu kwa mpigo kuinyanyapaa "itikadi"
 
Ni kosa la KATIBA yetu ya Nchi haielekezi SHERIA, SERA, VIPAUMBELE vya TAIFA ambavyo vitafuatwa na kiongozi anayeingia madarakani kutekeleza sera na vipaumbele vya Taifa kuanzia pale ambapo kiongozi aliyepita ameachia, matokeo yake vyama vya Siasa kwa kiasi kikubwa huwaachia wagombea wao kutengeneza sera na vipaumbele pindi wakishinda uchaguzi matokeo yake utaona kila kiongozi anayeingia madarakani anakuya na YAKE..........

Hujui Kiongozi ajae atasema nini.....!!!! Miradi kuachwa, Sera kubadilishwa au kufutwa.......!!!!
MAONI YA KATIBA YA WANANCHI ILIKUWA SULUHISHO.............
 
Daaa kama nakuona vile unavyoongea...
 
Ni sawa na kuweka taa za barabarani chato huku miji mikubwa inayozunguka chato na yenye magari mengi na watu wengi hakuna. Mfano Geita mjini hakuna, katoro hakuna, bukoba hata kakola hakuna unaweka chato .
Ni bora wangeboresha stand za Geita, chato ambazo zinatumiwa na watu wengi na magari mengi kuliko uwanja wa ndege wa 4D, hizo emirates, precision air n.k zinapandwa na watu wangapi kwenda chato kila SKU na kwa kivutio kipi? Huu ni ubinafsi tu hakuna hoja ya maana hapo
 


Ningependa kujifunza
KIA inamilikiwa na KADCO .....hii ni taasisi gani na code ya uwanja huu ni ngapi

Je viwanja hivi vina code gani na vimepewa code hizo kutokana na kukidhi vigezo gani
Songwe
Arusha
Mtwara
Tanga
Dodoma
Iringa
Mafia
Bukoba
Tabora
Kigoma
Katavi

Na kama kuna vingine vyenye lami please jazia
 
Nyie watu wapi hamuelewi?Hoja ya mleta mada si kukataa kujengwa kwa uwanja huko,ila kiwango cha kiwanja kinachojengwa sambamba na muitikio wa kiuchumi.

Huyu huyu mnamuita mnafiki,mlimsifia wakati analeta habari za bombadia na watu tukawa tuanazipinga!!Sasa leo kawa mnafiki?Hakuna anayekaa kujemgwa huko,lkn je ni ujenzi wa kiwango gani?
 
Yaani centre ya EAC uipeleke Kagera (sijui ulitaka kumaanisha Bukoba) utakuwa na akili wewe?
Wewe ulitaka uipeleke arusha?? Kwa kuzingatia videos vipi. ...au kwanza kwa vigezo vipiii???


Forums ninkati kwa Tanzania. ....je kagera ama bukoba na moshi ipi uko katikati mwa EAC !!!

Natumai utawaza kwa akili
 
Nimesoma mada kwa marefu na mapana yake,bahati mbaya wapo baadhi ya wachangiaji wana viwango vidogo sana vya uchangiaji.Hatuna namna ya kuwaondoa labda mods wangeweza kusaidia.

Mfano mleta mada kaeleza vizuri kwanini ujenzi wa uwanja CHATO ni kukosa mwelekeo,anakuja mtu utadhani kalazimishwa kuchangia "Eti kwani Chato ipo Sudani" mwingine mbona KIA ilipojengwa Bomang'ombe kulikuwa na nini.Unabaki kushangaa na kujiuliza maswali kibao ni jinsi gani shule,college... vimezalisha watu wa hovyo kwa kiwango hiki.Watu hawapendi kushughulisha bongo zao wanasema hovyo hovyo.

Nirejee kwenye mada.

Mosi,Ujenzi wa uwanja wa CHATO ulikuwepo katika mipango tangu mwanzo au uliibuka baada ya Dr Magufuli kuchaguliwa ?.Katika ilani ya CCM ujenzi wa viwanja vya ndege kiwanja cha ndege cha Chato kipo ?.

Pili,Ujenzi wa uwanja wa ndege unaambatana na sababu za kiuchumi,kijamii,kiusalama na nk.Kabla ujenzi haujaanza mambo yote yalingatiwa au tuliamua kwakuwa Rais anatoka eneo hilo,ikiwa ni hivyo maana yake tutakuwa tunafanya maamuzi kwa kuangalia maeneo wanakotoka viongozi na si kuangalia sababu za kiuchumi ?.

Tatu,Suala la kujenga miundombinu based on wanakotoka viongozi si jambo geni Afrika.Ukisoma historia ya kijiji cha Yamoussoukro alichozaliwa kiongozi wa mwanzo wa taifa la Ivory Coast Mh Felix Houphouet Boigny ambacho baadae kiligeuzwa makao makuu ya serekali badala ya Abdjan.Mh Felix Houphouet Boigny alianza na ujenzi wa kanisa kubwa dunia Basillica of our Lady of peace,ujenzi wa uwanja wa ndege wenye uwezo wa kutua ndege aina ya Concord (Afrika wakati huo vilikuwa viwili tu Gbadolite na Yamoussoukro Airport) na majengo ya kisasa kwaajili ya shughuli za kiserekali.Ukienda kule Zaire sasa Congo aliyekuwa Rais wake Marehemu Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga hakuishiwa vituko alijenga uwanja wa ndege mkubwa kuliko wowote Afrika wakati huo Gbadolite International Airport,Jumba la starehe na miundombinu ya kisasa kijiji alichozaliwa leo ni mahame kabisa hakuna kinachoendelea kwakuwa wakati wa ujenzi hawakuzingatia masuala ya uchumi,jamii,usalama na nk.







Control tower ilivyosasa.






Baadhi ya majengo yamegeuzwa madarasa.



Hotel ya kifahari leo haina wageni hata kiduchu.



Hata Mbuzi hawapatiki.



Bwawa la kuogelea lilivyo sasa.






Ulevi wa madaraka ulivyoteketeza mabilioni ya fedha za walipa kodi katika uwekezaji wa kijinga.
 
Nawashangaa sana wabongo, what economic potentials are you referring and leave away Rubondo game reserve.Mwaka Jana mheshimiwa Raila odinga alitumia sikukuu ya mwaka mpya kwenda kupumzika kama mtalii yeye na familia yake.Lakini jiulize alifikaje huko? Alitumia Helicopita ya kukodi ambayo gharama zake kurudi Tena mana ziko juu. Kibiashara feedback tunapata kutoka kwa customers wetu.Hatuwezi jua feedbacks za wateja zinasemaje.Lakini tu nadhani kuna with kutoka kwa wateja wa high rank like Raila wameshauri uboreshaji. Tumezoea kusikia traditional mbunga za wanyama Kama serengeti, ngorongoro, Lakini Rubondo Nani anajua? Ambako tunaambiwa kuna ndege adimu duniani wako kule huwezi kuwapata popote duniani.Acha cha to internaltional airport ijengwe bana tukaone ndege adimu duniani. Raila kaanza wengine tufuate
 
Mkuu wasiojua wanashangilia lakini project imesimama juzi juzi Makame amepita na kiswahili kingine tumerogwa
 
hahahaaaahaaaaaaaaaaaa hii kweli ni hatari kibwa sana maana watu wanafanya vitu bila kiangalia kesho itakuaje
 
Jukumu lako wacha kulalamika. Pray your part. Uwanja hauna shida mbona wa songwe ulipelekwa polini hakuna aliye seema!!

Infact wa bukoba wanamalizia kulipa fidia ili uhanze kujengwa!! Sijui utakuja na hoja kuwa wajengewe nyumba kwanza!!!
 
 
Wewe ulitaka uipeleke arusha?? Kwa kuzingatia videos vipi. ...au kwanza kwa vigezo vipiii???


Forums ninkati kwa Tanzania. ....je kagera ama bukoba na moshi ipi uko katikati mwa EAC !!!

Natumai utawaza kwa akili
Acha pombe,,, kumbuka EAC ni mpaka bahari YA Hindi huko Sasa chukua eneo lote hilo uone kama centre CYO Arushaa
 
Wacha kubabaisha watu bwana. Unahisi wale wanao kwenda mleba au biharamuro ama geita ama katoro ama kahama watalazimika kutumia mabasi..

Usisemehe mifuko yavwenzio kama Nina hela wenzako wanazo. Na habari ya viwanda na hayo mengine yatakuja.
Wewe ndio mbabaishaji na hujawahi kupanda ndege hata mara moja. Kweli kabisa naenda Kahama nipande ndege kwenda Chato halafu nisafiri toka Chato hadi Kahama nisishukie uwanja wa ndege wa Buzwagi kwa Auric au Shinyanga? Au naenda Muleba nisishukie Bukoba niende Chato. Ndio maana watu wote wenye uelewa wameshauri kama kipaumbele ni uwanja wa ndege kwa ajili ya makabira ya huko kwenu basi uwanja wa kimataifa ungejengwa Omukajunguti na sio Chato. Mimi naifahamu Chato toka miaka ya 90 nimepiga sana madili kule maeneo ya Mwendakulima, Mwabasabi, Munekezi, Nyakayonda, Lubambangwe na tulikuwa tunalala kwenye Guest ya mzee wetu Makufuli enzi hizo na naheshimu raisi kuwa na uwanja wa ndege nyumbani kwake asitumie muda mrefu safarini, lakini sio uwanja wa ndege wa kiwango cha kimataifa kwa kuwa nchi yetu bado maskini haina uwezo wa kujenga viwanja vya kimataifa kila mkoa au wilaya. Bukoba kwenyewe ndege hazijai ndo iwe huko Chato? Nyerere alishawashtukia nyie ni wabinafsi toka siku nyingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…