Wo shi niubi
JF-Expert Member
- Aug 14, 2015
- 1,353
- 1,784
Tatizo lenu mmelewa ulevi wa madaraka, kama suala ni kupata upendeleo mngeanza na mambo ya msingi kwenu kama ugonjwa wa mnyauko wa migomba, awasaidie research na suluhisho mngeondokana na njaa kali mliyonayo sasa.
Basi la Sabuni au Lushanga kwenda Chato halijazi abiria nauli chini ya elfu kumi mtajaza ndege nyie? Tumieni upendeleo huu wa raisi kutoka kwenu awasaidie vya maana sio white elephants.
Hakuna mmiliki wa ndege Chato, hakuna kiwanda zaidi ya ginnery ya ushirika, hakuna hata Hotel pale zaidi ya tule tu Lodge tuchafu nani apande ndege kwenda Chato mtukufu akitoka. Mwanakijiji wa Ilyamchele atapanda ndege?
Sio tu kulewa madaraka ila wamelewa mbenge , hivi chato na Geita wapi kumeendelea na kuna kuwa kwa haraka? hata kasamwa ni better kuliko chato, kwa nini tusiangalie walau eneo karibu na Geita tukajenga huo uwanja to boost and rapid growth of Geita region? kama tu mini-Bus zenye abilia 23 haziwezi kujaza abiria kutoka chato iweje kwa ndenge? tuweni na vipaumbele kama Taifa, tujenge viwanja hivi kulingana na mahitaji ya kiuchumi Tanzania sio mahitaji ya kikanda ,mfano wadau wengi wanadai Serengeti ndio hitaji kuu sasa hivi basi nguvu ya chato ilitakiwa ihamishiwe Musoma/Tarime/Mwanza nk.