Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

Umenikumbusha ile bajeti ya ujenzi kipindi cha Mramba, bajeti ya mkoa mmoja ilikuwa sawa na bajeti ya mikoa sita!
Kumbe ilikuwa na Vijiba vya Roho juu ya kanda ileee! Hakika visasi at work! Kaskazini ni wimbo wa wenye chuki na wivu! kule watu wanajibeba wenyewe na kila kilichopo kina matumizi. Hakuna kilichowahi kupelekwa huko kwa kulipa Kisasi kwa kuwa vingi vilipelekwa Nyerere akiwa madarakani. Sababu aliijua Mzee wa watu aliyeipenda Tanzania yote. Hakuwa na ukabila wala Ukanda. La sivyo Butiama ingekuwa Dubai ya Tanzania. RIP mwalimu. Kama kila kinacholalamikiwa au kuhojiwa mnaikomoa the so called Kaskazini mmebug". Muda utasema one day.
 
Huu uwanja utakamilika alafu patakua inatua ndege moja kwa wiki. Kama kuna cha maana sana Chato kwa nini wasingetumia uwanja wowote uliopo karibu, Chato ni 128 km kutoka mwanza, hapo hata bus linachukua chini ya masaa mawili. Hakuna haja ya kujenga uwanja wenye hadhi kubwa eneo hilo, angalau kwa sasa maana hakuna economic activity yoyote ya maana kule, au labda ipo alafu hatujaambiwa!

Watanzania wanajifanya wamefunika macho, kila nikiongea na wazee utasikia "vijana muacheni mtukufu afanye kazi/anajua tunapokwenda/mnamkwamisha" kwa decisions hizi ni lazima tulaumu. Wanavyoongelea swala la transparency ndio wakate wake huu sasa, watupe sababu za msingi za kujenga kiwanja kikubwa sehemu isiyo na manufaa yoyote. Waliopitisha hili swala naomba watoe sababu maana haiingii kichwani kabisa, kuna nini ambacho hatukioni?
 
Kumbe ilikuwa na Vijiba vya Roho juu ya kanda ileee! Hakika visasi at work! Kaskazini ni wimbo wa wenye chuki na wivu! kule watu wanajibeba wenyewe na kila kilichopo kina matumizi. Hakuna kilichowahi kupelekwa huko kwa kulipa Kisasi kwa kuwa vingi vilipelekwa Nyerere akiwa madarakani. Sababu aliijua Mzee wa watu aliyeipenda Tanzania yote. Hakuwa na ukabila wala Ukanda. La sivyo Butiama ingekuwa Dubai ya Tanzania. RIP mwalimu. Kama kila kinacholalamikiwa au kuhojiwa mnaikomoa the so called Kaskazini mmebug". Muda utasema one day.
Sio Butiama tu, sehemu nyingi Tanzania zilikuwa choka tu, alikuwa ame deal na ukombozi wa Africa wakati Watanzania wakibaki majalala...

Mzee Mkapa ndio aliijenga Tanzania upande wa miundombinu, mzee Kikwete akaendelea, JPM anaendelea na yeye...

Viwanja vingine vya ndege vinaendelea kujengwa sio kwamba KIA imesimama kupanuliwa, au uwanja wa Mwanza umesimama, hapana ujenzi pia unaendelea...

Na sio kwamba eti Kaskazini miradi imesimama, hapana inaendelea, na sehemu zote miradi inaendelea, Dar es salaam kuna miradi mingi pia, Dodoma pia...

Hakuna kisasi kwa Kaskazini, wala hakuna kisasi kwa sehemu nyingine, Miradi inaendelea kama kawaida...
 
Mkuu Barafu baada ya kuleta ile habari ya kwanza ya Uwanja wa NDEGE WA CHATO niliona nifuatilie sababu za Ujenzi wa huo Uwanja na umuhimu wake...

Findings....

Nimeelezwa kuwa, Rais Magufuli amejenga Uwanja huo CHATO ili aweze kuziteka nchi za RWANDA, BURUNDI, na UGANDA, Kwamba, Ndege za kutoka mataifa hayo zitatua CHATO INT. AIRPORT, halafu abiria watapanda Gari zao kutoka CHATO hadi MWANZA ambapo watapanda tena NDEGE kwenda wanapopataka ndani au nje ya nchi, (SIJUI NI AKILI GANI ILIYOTUMIKA HAPA) nimeelezwa kwamba, Rais Magufuli anataka kujenga DARAJA La BUSISI ili kurahisisha usafiri huo wa wageni kuja Mwanza kutoka CHATO INT. AIR.

Nimeelezwa kuwa, Mpango wa Magufuli ni Kuutenganisha mkoa wa GEITA Na CHATO hapo baadae, hivyo anaandaa mazingira ya kushawishi ugawaji wa MIKOA Hiyo, na makao makuu ya mkoa wa CHATO yatakuwa eneo moja linaitwa RUSUNGU hivi kama sijakosea jina, nakubali nirekebishwe maana nimesahau jina lake kwa usahihi.

Nimeelezwa kwamba, Eti CHATO kuna Mbuga ya WANYAMA binafsi ya RAIS Magufuli ila sijawa na uhakika na hili...

Kwa kifupi, hata kama Chato walikuwa na uhitaji wa uwanja wa ndege siyo sasahivi jamani, wewe fikiria, Plan zipo kwenye vitabu miaka mingi juu ya ujenzi wa viwanja kama MWANZA, MUSOMA Nk. lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika kwenye viwanja hivyo, ila hiki cha chato ndo kiwe Urgent?

KWELI MANGOMBE tunajenga uwanja wa ndege wa chato tunauacha uwanja wa ndege wa MWANZA hiyo pesa ingepelekwa uwanja wa mwanza ambao mpango wa taifa ni kuufanya mji maarufu wa kibiashara afrika mashariki na maziwa makuu
Tunaharibu resources chache ...kupanga ni kuchagua .....!!!
Mpango wa pili ulikuwa Uwanja wa ndege wa Bukoba ....kuujenga kwa kiwango cha kimataifa ..na Kigoma ili kuteka wasafiri wa nchi jirani pia ..
SASA someni kwa makini dira ya maendeleo muone ni wapi palikuwa na mpango wa CHATO INTERNATIONAL AIRPORT [sic]

Uwanja wa ndege wa Songwe International ..ambao unalenga kuteka biashara ya nchi za kusini ..unahitaji pesa kidogo tu ili ufikie kiwango kinachotakiwa ...hadi sasa pale ndege haziwezi kutua usiku ,bado haijajengwa WAREHOUSE cold rooom ili ku boost biashara ya usafirishaji wa mauwa ,matunda,huko Iringa ,Mbeya na nchi jirani ......

Kwa kweli imenisikitisha sana kutibua mipango ya maendeleo ya taifa kwa ubinafsi ....dalili ya mvua ni mawingu ....kuna watu walijitahidi kuiondoa Chato toka kagera....., walihamisha hadi barabara ipite chato ........sasa wamepata kikubwa watajenga kila kitu hata kama hizo ndege hapandi .......

SAULI aache ubinafsi!!!
 
Sio Butiama tu, sehemu nyingi Tanzania zilikuwa choka tu, alikuwa ame deal na ukombozi wa Africa wakati Watanzania wakibaki majalala...

Mzee Mkapa ndio aliijenga Tanzania upande wa miundombinu, mzee Kikwete akaendelea, JPM anaendelea na yeye...

Viwanja vingine vya ndege vinaendelea kujengwa sio kwamba KIA imesimama kupanuliwa, au uwanja wa Mwanza umesimama, hapana ujenzi pia unaendelea...

Na sio kwamba eti Kaskazini miradi imesimama, hapana inaendelea, na sehemu zote miradi inaendelea, Dar es salaam kuna miradi mingi pia, Dodoma pia...

Hakuna kisasi kwa Kaskazini, wala hakuna kisasi kwa sehemu nyingine, Miradi inaendelea kama kawaida...
Mbona hilo neno KASKAZINI linarudiwa rudiwa ........sana !!! Kwani SAULI hajui sifa ya kuku wa kienyeji ???
Uwanja wa Ndege Wa Mwanza uishe kwanza ......
 
Nahisi mmemiss kukaa kwenye mifuko ya sandarusi na kukutwa mkielea ufukweni!!!!!!
 
Mnaweza kuweka uchambuzi mzuri sana ila ukakosa mashiko kwa kuwa tu una lengo la kiitikadi zaidi.

Mimi huwa najiuliza, je suppose tungechagua huko, kwa bahati mbaya sana umeshindwa kujiendesha wenyewe mkaamua kuturudishia walewale waliokimbia huku baada ya kukatwa je mngeweza kutujengea nchi kweli?, au mngeishia kuandika uchambuzi kama huu wakati mkishuhudia barabara ya Chalinze-Moshi ikiwekwa 4 ways, na kiwanja kama hicho cha chato kikijengwa Hai au Monduli?

Maana wenzetu wa upinzani mmekuwa mabingwa ya kuchambua msivyoviweza, mmekuwa wazuri theoretically but you are not practically oriented, mambo yenu mengi yanakwenda kinyume lakini kwa vile kafanya yule, basi you keep quite kama vile hamuoni huku ukisubiri uongee likifanyika upande wa pili.

Kaskazini ilijengeka mapema kwavile watu wa kaskazini walipata fursa, wakakumbuka kwao ili wapate kwenda mapumzikoni kila mwaka, sasa acha fursa zinapopatikana sehemu zingine basi wazitumie fursa hizo, huku mkiwa wavumilivu mkisubiri 2020 ,

Acha ushabiki usiokuwa na tija. Chato haihitaji airport kubwa hivyo, ingewekewa airstrip tu kama ile ya buzwagi kahama ingefaa kabisa mkuu akitaka kwenda kwake anatua vizuri tu. Ulishafika chato? Kaangalie kioja cha traffic lights za chato, gari ni za kuhesabu, inabidi ziongoze mikokoteni inayovutwa na punda, sasa kwa usawa huo hao wasafiri wa kupanda ndege hapo watatoka wapi? hakuna biashara kubwa chato au kivutio chochote cha utalii!!! Mbaya zaidi hata sehemu zinazoizunguka chato ziko hoi kiuchumi!!! Itazame biharamulo, bwanga, buziku , ngara, muleba, hao abiria watatoka wapi? Nakuhakikishia hakuna shirika la ndege litapeleka ndege zake hapo kwasababu hakutokuwa na abiria, itakayotua hapo ni ndege ya Rais tu, na akistaaf ndo ujue utakuwa mwisho wa matumizi ya uwanja huo. Uzalendo uko wapi kwenye mradi huu??
 
Mbona hilo neno KASKAZINI linarudiwa rudiwa ........sana !!! Kwani SAULI hajui sifa ya kuku wa kienyeji ???
Uwanja wa Ndege Wa Mwanza uishe kwanza ......
Watu wanafanya reference ya kaskazini kila kitu, wengine wakidai analipiza kisasi huko...

Sasa mimi nikauliza ni miradi ipi ya kaskazini imesimama au imeachwa...?!

Mfano uwanja wa KIA unafanyiwa maboresho pia...
 
Mkuu unajua uamuzi wa mkulu ata si mbaya kwa vile uwanja huo upo ndani ya tz hakuna shida, Mimi sikuwa na furahishwa na raisi kutumia mini airport ya pale Anglo gold mining GGM
Kiongozi kwani atatawala milele? Kahama population ni kubwa sana.
 
kuna Uzi humu niliona airport aliyojenga Mobutu kule kijijini kwao ikiwa porini Watu wakichunga ng'ombe na mbuzi japo ilikuwa ya kiwango cha juu.
like above so is bellow
 
Back
Top Bottom