Hatimaye David Kafulila akabidhi ofisi, aendelea kusisitiza Rais Samia hakamatiki utekelezaji wa Ilani, amtaja kuvunja rekodi ya miaka 20 kwenye maji

Hatimaye David Kafulila akabidhi ofisi, aendelea kusisitiza Rais Samia hakamatiki utekelezaji wa Ilani, amtaja kuvunja rekodi ya miaka 20 kwenye maji

Ivi kweli, Kafulila ni maneno matupu?

1. Kuvunja mkataba na CHICCO baada ya kuteengeneza barabara chini ya kiwango na kuokoa fedha za serikali 15bilioni ni maneno matupu haya?

2. Ivi kweli kuzui michomoko iliyoua maelfu Tanzania ni maneno matupu?

3. Ivi kweli Kuongeza bei ya pamba toka 800/kg mpaka 1,800/kg haya ni maneno matupu?

4. Ivi kweli kukamata wezi wa Pamba na kuwafunga na wengine kujinyonga ni haya ni maneno matupu?

5. Kumnyang'anya kada wa CCM yaani MNEC soko la madini alilolimiliki kinyume cha sheria haya ni maneno matupu?

Let's be serious guys Kafulila ni asset kwa Taifa letu,


Ova.
Jamaa ni asset kwelikweli kwa CCM na Taifa kwa ujumla wake
 
Ilani ya Nani ?

Huyu kuwa mpinzani alikuwa anapinga itikadi au Watu ?

Kwa Siasa full Usanii especially Bongo Chama ni Platform ya kuweza kwenda kupata ulaji na sio sehemu ya mawazo mbadala
Jaribu kuchungulia wenzetu pale Kenya, Vyama is nothing but a Nation
 
Ukiona Rais anafanya maamuzi na wanaofurahia ni hawa CHADEMA nadhani hayo maamuzi yanawapa nafuu wao kama Upinzani,

#Naamimi Kafulila anapelekwa juu na Mama ili kuwanyoosha vizuri.Time will tell
Kafulila atarudi juu, hiyo ni given
 
Atapangiwa Kazi zingine ale kwanza alizopata
 
Dr Slaa alimuita Sisimizi

AG akamuita Tu2
Rejelea ni kwanini alimwita hivyo?

Nasisitiza Kafulila ni material Sana kwa nchi hii hasa sasa,

Nitakuwa mkweli kama nilivyomkweli kuMsemea Rais Samia
 
Huyu kazi yake ni kumfurahisha Rais ama

Kuwatumikia wananchi.
 
Kafulila atarudi juu, hiyo ni given
Hii itawapa nguvu hata RCS wengine,

Uchawa hauepukiki hasa kwenye nchi za vyama vingi kama hii,

Winners takes all hii ni hatari Sana
 
Kama kuna RC alimwelewa na kumwelezea Vizuri Rais Samia kwa Umma basi ni Kafulila

Hamu yangu RCs waige mazuri ya Kafulila hasa kusema mazuri ya Rais wetu na Serikali anayoiongoza.
Chawa chawa kazini
 
"RAIS SAMIA AMEVUNJA REKODI YA MIAKA 20 SEKTA YA MAJI, AMEOKOA TRILIONI 3 AMBAZO ZINGETUMIKA KUTIBU MAGONJWA YATOKANAYO NA UKOSEFU WA MAJI."


Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe David Kafulila amesema Rais Samia Suluhu Hassan amevunja rekodi ya utekelezaji wa bajeti ya maji ya miaka ishirini mfululizo iliyopita,

Mhe David Kafulila anasema, wakati nakuja Simiyu baada ya kuaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan nilikuta kero kubwa kuliko zote kwa Mkoa wa Simiyu ni " Maji "

Leo Mwaka mmoja huu niliokaa hapa tumeshirikiana kusimamia mabilioni ya fedha za miradi ya maji ninyi nyote mtakuwa mashahidi wangu,

Leo naondoka Mkoa Simiyu wote tunaona tatizo la maji limepungua sana hapa lazima tumshukuru Sana na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan,

Simiyu upatikanaji wa maji safi na salama kwa mwaka 2020/21 nilikuta ni asilimia 56% leo tumefikia asilimia 73% na hii ni kufikia Juni 2022 lazima wana Simiyu kumshukuru Sana Rais Samia Suluhu Hassan,

Lakini Rais Samia huyu huyu tayari ametuletea mradi mkubwa wa bomba la kilometa 190 kutoka ziwa victoria wenye thamani ya Shilingi billioni 400.

Ndugu zangu Wanasimiyu mradi huu utapita zaidi ya vijiji vyenu 200 ambao kazi za awali nadhani mnaona zimeanza,Asanteni Sana kwa ushirikiano wenu huu mkubwa,

Kafulila anaendelea kusema, Niwambie ukweli, Nimesoma bajeti za miradi ya maji za miaka 20 mfululizo kuanzia ile ya mwaka 2000 mpaka ya mwaka 2020,

Nataka niwaambie kwa miaka yote hii hakuna mwaka ambao fedha za miradi ya maji zilitolewa hata kwa asilimia 80%.

Lazima mfahamu,Bajeti ya kwanza tu ya awamu ya sita( 2021/22) fedha za miradi ya maji zilizotolewa ni billioni 743 sawa na asilimia 95% ya bajeti iliyopitishwa na bunge na hii ni ndani ya miezi 9 tu Sio mwaka.

Huu ni ushahidi mwingine kuwa Rais wetu anatekeleza kauli mbiu yake ya kumtua ndoo mama kichwani kwa vitendo.

Rais Samia anaelewa kuwa maji ni uchumi, maji ni ustaarabu, maji ni afya... Maji ni Uhai,

Mtakumbuka,Ripoti ya shirika la Afya duniani mwaka 2014 ilionesha kuwa kwenye kila dola moja inayowekezwa kwenye maji, inaokoa dola 4.2 ambazo zingetumika kutibu magonjwa yanayotokana na ukosefu wa maji safi na salama( UN- News, Nov19, 2014).

Hivyo hivyo billioni 743 za miradi ya maji katika mwaka mmoja wa Rais Samia wa 2021/22 ni sawa na kusema Rais wetu kaokoa Shilingi trilioni 3.1 ambazo zingetumika kutibu magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji.

Kafulila anaendelea kusema, Labda niwakumbushe tu kwamba utafiti uliofanywa na taasisi ya SYNOVATE mwaka 2008 ulionesha kuwa kero namba moja kwa mtazania ni maji.

Msiojua,SYNOVATE ni taasisi 5 kwa sayansi ya uratibu wa maoni duniani wakati huo kabla haijachukulia na IPSOS ambayo kwa sasa ni moja ya taasisi 3 kubwa duniani kwa kazi hiyo(OPINION SURVEY).

Mkuu huyu wa mkoa anasema, Hiki ni kielelezo kuwa Kiongozi anaetatua tatizo la maji anagusa maisha ya watanzania walio wengi na hasa vijijini ambao inawezekana hawana kelele nyingi kwenye mitandao..wanaitwa ' silent majority'..Hivyo tunaposema Mama anaupiga mwingi sio sisi ni takwimu za kitafiti.

Hivyo tuendelee kuwasaidia wananchi kwa kuhakikisha wakandarasi wanatekeleza mikataba na tuendelee kuvunja mikataba ya wababaishaji kama tulivyofanya siku zote kuhakikisha kuwa fedha anazoleta Mhe.Rais kukabili kero ya maji zinafanya kazi kwelikweli,

Hayo yamesemwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe David Kafulila leo wakati wa makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kati yake na Mkuu wa Mkoa Mpya Dr Yahaya Mawanda ambapo mbali ya kueleza sura ya Mkoa wa Simiyu, Kafulila ameleza pia maamuzi 9 ya kimkakati aliyotekeleza ndani ya mwaka mmoja na mwezi 1 wa Utumishi wake katika nafasi ya hiyo ya Mkuu wa Mkoa huo wa Simiyu
SWALI,

kwanini wanaofurahia kutenguliwa Kwa Hapi na Kafulila ni watu Wa UpinzaNi?
 
Huyu jamaa ukuu wa mkoa haumfai level yake ni ya uwaziri au unaibu
 
Back
Top Bottom