Hatimaye David Kafulila akabidhi ofisi, aendelea kusisitiza Rais Samia hakamatiki utekelezaji wa Ilani, amtaja kuvunja rekodi ya miaka 20 kwenye maji

Hatimaye David Kafulila akabidhi ofisi, aendelea kusisitiza Rais Samia hakamatiki utekelezaji wa Ilani, amtaja kuvunja rekodi ya miaka 20 kwenye maji

View attachment 2319594
Mhe. David Kafulila akimkabidhi Katiba ya JMT Mkuu Mpya wa Mkoa Mh. Dkt Yahya Mawanda kama nyenzo yake ya kufanyia maamuzi

Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mh. David Kafulila amesema kwamba Rais Samia Suluhu Hassan amevunja rekodi ya utekelezaji wa bajeti ya maji ya miaka ishirini (20) mfululizo iliyopita tangu mwaka 2000.

Mh. David Kafulila ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi majuzi huku akiwaahidi wakuu hao wa Mikoa walioachwa kuwatumia maeneo mengine anasema, "Wakati nakuja Simiyu kama mkuu wa mkoa baada ya kuaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan nilikuta kero kubwa kuliko zote kwa Mkoa wa Simiyu ni "Maji".

View attachment 2319595
Mh. David Kafulila akiwa katika picha ya pamoja na mkuu mpya wa Mkoa wa Simiyu Mhe Dkt Yahya Mawanda wakati wa makabidhiano ya ofisi mkoani Simiyu

Mh. David Kafulila anaendelea kwa kusema, Leo Mwaka mmoja huu niliokaa hapa Mkoa wa Simiyu tumeshirikiana kusimamia vizuri Sana mabilioni ya fedha za miradi ya maji zilizoletwa Mkoa wa Simiyu na Rais wetu Mhe Samia Suluhu Hassan ninyi nyote mtakuwa mashahidi wa hili.

Mh. David Kafulila anaendelea kwa kusema, Leo naondoka katika Mkoa huu wa Simiyu wote tunaona tatizo la maji limepungua sana hapa lazima tumshukuru sana na kumpongeza Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan.​


View attachment 2319605
Mh. David Kafulila akimkabidhi mkuu mpya wa mkoa wa Simiyu ripoti ya CAG ili aendelee kusimamia majibu yote ya hoja za CAG zinazohusu mkoa wa Simiyu

Anaendelea kwa kusema, Mkoa wa Simiyu upatikanaji wa maji safi na salama kwa mwaka wa 2020/21 Wakati Rais Samia anaingia madarakani nilikuta ni asilimia 56% leo tumefikia asilimia 73% na hii ni kufikia Juni 2022 lazima wana Simiyu kumshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan. Mh. Kafulila anasema, Lakini Rais Samia huyu huyu tayari ametuletea mradi mkubwa wa bomba la kilometa 190 kutoka Ziwa Victoria wenye thamani ya shilingi billioni 400. "Ndugu zangu Wanasimiyu mradi huu utapita kwenye zaidi ya vijiji vyenu 200 ambao kazi za awali nadhani tayari mnaona zimeanza. Asanteni sana kwa ushirikiano wenu huu mkubwa mliouonesha kwangu na kwa Rais Samia Suluhu Hassan".​

View attachment 2318676
Mh. David Kafulila akikishukuru Chama cha Mapinduzi mkoa wa Simiyu kwa ushirikiano katika kuitekeleza Ilani ya Uchaguzi 2020/25

Mh. Kafulila anaendelea kwa kusema, "niwambie ukweli, mimi nimesoma bajeti za miradi ya maji za miaka 20 mfululizo kuanzia ile ya mwaka 2000 mpaka ya mwaka 2020. Nataka niwaambie kwa miaka yote hii hakuna mwaka ambao fedha za miradi ya maji zilitolewa hata kwa asilimia 80 Tu. Lazima mfahamu, bajeti ya kwanza tu ya awamu ya sita( 2021/22) fedha za miradi ya maji zilizotolewa ni billioni 743 sawa na asilimia 95% ya bajeti iliyopitishwa na bunge na hii ni ndani ya miezi 9 tu Sio mwaka."​

View attachment 2318677
Mh. David Kafulila akimkabidhi Mkuu mpya wa Mkoa "SIMIYU MODEL" inayotamka kuwa "IF NO CASH THEN NO COTTON-SIMIYU"

Mh. Kafulila anaendelea kusema, "huu ni ushahidi mwingine kuwa Rais wetu anatekeleza kauli mbiu yake ya kumtua ndoo mama kichwani kwa vitendo. Rais Samia anaelewa kuwa maji ni uchumi, maji ni ustaarabu, maji ni afya na maji ni uhai. Mtakumbuka Ripoti ya shirika la Afya Duniani mwaka 2014 ilionesha kuwa kwenye kila dola moja inayowekezwa kwenye maji, inaokoa dola 4.2 ambazo zingetumika kutibu magonjwa yanayotokana na ukosefu wa maji safi na salama (UN- News, Nov19, 2014). Vivyo hivyo billioni 743 za miradi ya maji katika mwaka mmoja wa Rais Samia wa 2021/22 ni sawa na kusema Rais wetu kaokoa Shilingi trilioni 3.1 ambazo zingetumika kutibu magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji."​

View attachment 2319609
Vijana wa Mama Samia wakifurahia jambo katika ofisi ya mkuu wa mkoa Simiyu

Kafulila anaendelea kusema, "Labda niwakumbushe tu kwamba utafiti uliofanywa na taasisi ya SYNOVATE mwaka 2008 ulionesha kuwa kero namba moja kwa mtazania ni maji. Msiojua SYNOVATE ni taasisi 5 kwa sayansi ya uratibu wa maoni duniani wakati huo kabla haijachukulia na IPSOS ambayo kwa sasa ni moja ya taasisi 3 kubwa duniani kwa kazi hiyo(OPINION SURVEY)."​

View attachment 2319604
Mkuu mpya wa mkoa wa Simiyu Mh. Dkt Yahya Mawanda(kulia) katika makabidhiano ya ofisi ya Mkoa wa Simiyu toka kwa Mhe David Kafulila

Mkuu huyu wa mkoa Mstaafu anasema, "hiki ni kielelezo kuwa kiongozi anaetatua tatizo la maji anagusa maisha ya watanzania walio wengi na hasa vijijini ambao inawezekana hawana kelele nyingi kwenye mitandao wanaofahamika kama 'silent majority'. Hivyo tunaposema Mama anaupiga mwingi sio sisi ni takwimu za kitafiti."​

View attachment 2319596
Mh. David Kafulila akiwashukuru viongozi wenzake kwa upendo na ushirikiano mkubwa waliompa

"Hivyo tuendelee kuwasaidia wananchi kwa kuhakikisha wakandarasi wanatekeleza mikataba na tuendelee kuvunja mikataba ya wababaishaji kama tulivyofanya siku zote kuhakikisha kuwa fedha anazoleta Mh. Rais kukabili kero ya maji zinafanya kazi kwelikweli."​

View attachment 2318678

View attachment 2320722
Mh. Dkt Yahya Mawanda akiwalisha wafanyakazi wenzake keki kama ishara ya unyenyekevu wake kwao

Hayo yamesemwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh. David Kafulila wakati wa makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kati yake na Mkuu wa Mkoa Mpya Mhe Dr Yahaya Mawanda.​
Kapumzike nyambafu weye. Uliwatesa sana watumishi
 
Hayo maelezo angeandika warka juu ya mipango aliyokuwa nayo ampe ofisi,kuongea hkufanyi aonewe huruma.
 
Hayo maelezo angeandika warka juu ya mipango aliyokuwa nayo ampe ofisi,kuongea hkufanyi aonewe huruma.
Maelezo gani? Kafulila anaowajibu wa kumsemea Mama kama ilivyo kwa wanachama wengine
 
===
Kama kuna RC alimwelewa na kumwelezea Vizuri Rais Samia kwa Umma basi ni huyu Kafulila

Hamu yangu RCs waige mazuri ya Kafulila hasa kusema mazuri ya Rais wetu na Serikali anayoiongoza.

Hebu angalia hii ni kazi ya Rais Samia kwa mkoa mmoja tu Simiyu ,

Yule anayebisha Rais Samia kiboko yao anashida kubwa ya akili
VIVA SAMIA VIVA CCM VIVA
Sure
 
Kama kuna RC alimwelewa na kumwelezea Vizuri Rais Samia kwa Umma basi ni Kafulila

Hamu yangu RCs waige mazuri ya Kafulila hasa kusema mazuri ya Rais wetu na Serikali anayoiongoza.

Hebu angalia hii ni kazi ya Rais Samia kwa mkoa mmoja tu Simiyu ,

Yule anayebisha Rais Samia kiboko yao anashida kubwa ya akili
Kafulila tumemmis Sana aise
 
Back
Top Bottom