Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Tangu Awamu wa 1 Kenya alijitanabaisha kama Silent enemy wa Tanzania na hii lilisababishwa na tofauti za kiitikadi/kiuchumi baina ya Mataifa haya mawili
Ugomvi wa Kenya na Tanzania ulianza mara tu baada ya Tanzania kutangaza kufuata mrengo wa kijamaa hapo mwaka 1967 na kilichofuata baada ya hapo ni vita vya ujasusi baina ya mataifa haya 2
Katika vita hii, Kenya waziwazi aliunga mkono watu waliokuwa either wanataka Tanzania isitawalike au waliokuwa wakizipinga serikali za Chama cha Mapinduzi.
Mfano tu:
Mwaka 1967 Kenya walitumika kumtorosha mpinzani wa 1 wa Nyerere aliyejitoa kwenye serikali Ndugu Oscar Kambona. Kambona baada ya kutofautiana na Nyerere alikimbilia Uingereza kupitia Nairobi
Mwaka 1981 Kenya walimtorosha aliyeongoza kikundi cha wanajeshi waliotaka kumpindua Mwl Nyerere ndugu Khatib Ghand
Kenya pia ilitumika kama njia ya kuwatorosha marubani walioteka ndege ya Tanzania kumlazimisha Nyerere kung'atuka
Baada ya Nyerere kuondoka na Kenya kutawala uchumi wa Afrika Mashariki , Kenya ilibadili mbinu za kuidhoofisha Tanzania na kuhamia kwenye mbinu za kudhoofisha mipango yote ya maendeleo ambayo inaweza kuifanya Tanzania ikawapiku kiuchumi
Njia kuu aliyotumia Kenya kudhoofisha mipango ya Maendeleo ya Tanzania ni siasa maana aligundua mambo yote ya kimandeleo ya Tanzania yanaamuliwa kisiasa
Kupitia siasa , Kenya alifanikiwa kudhoofisha miradi ifuatayo ya Tanzania na baada ya miradi iyo kukwama Tanzania akaenda kuifanya kwake
1. Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo
Njia kuu aliyotumia Kenya kukwamisha mradi huu ni kueneza propaganda kuwa Bagamoyo anauziwa mchina. Hoja hii ilifanya mradi huu ukakwama Tanzania na hatimaye Kenya akatengeneza Bandari kama hiyo Lamu tena kwa kupitiq mchina huyo huyo
2. Mradi wa Satellite City, Kigamboni
Kenya alijua kigamboni ikifanikiwa basi ndo itakuwa Dubai ya kwanza Afrika Mashariki na akatumia propaganda kuwa George Bush amenunua kigamboni na siasa ile ikasabisha Tanzania tushindwe kuwa nchi ya 1 ukanda huu kuwa na satellite city. Sasa Kenya ndo imekuwa ya 1 baada ya kuanzisha mradi wa Konza City
Sasa ugonjwa huu umepatiwa Dawa:
Kiukweli maraisi takribani 5 wa Tanzania kutokana na kuendekeza kuwa populist walishindwa kujinasua kutoka kwenye mbinu hizi za Kenya. Ni Samia Suluhu Hassan aliyejaribu na napenda kusema anaenda kufanikiwa kwa kuzishinda propaganda za Kenya kwenye hili suala la Loliondo/ Ngorongoro
Ni ukweli usiopingika kuwa sasa Kenya anahangaika usiku kucha ili aimalize sekta ya utalii ya Tanzania ambayo kiuhalisia ndo tishio kubwa zaidi kwa uhai wake kiuchumi ambao unategemea hasa kiutalii
Ndoto kubwa ya Kenya ni kuua uti wa Mgongo wa utalii wa Tanzania ambayo ni kaskazini mwa Tanzania. Ukiongelea kaskazini wa Tanzania unaongelea Loliondo, Ngorongoro, Serengeti na kilimanjaro bila kusahau Manyara.
Njia pekee anayotegemea Kenya kufanikisha hili ni kuhakikisha siasa inatumika ipasavyo ili shughuli za kibinadamu zisikome kwenye mbuga hizi maana kwenye shughuli za kibinadamu mnyama hakai na pasipo na mnyama basi mtalii hawezi kuja.
Katika suala la Ngorongoro/ Loliondo, Kenya kaja na propaganda ya kisiasa kuwa eneo lote lile anapewa mwekezaji hivyo Wamasai hawatakiwi kuwepo
Propaganda hii kusema kweli imefeli vibaya sana na kwa mara ya kwanza chini ya Rais Samia tumeona propaganda za Kenya zikishindwa na Serikali ikitekeleza wajibu wake kwa Maslahi mapana ya Taifa
Hongera Samia! Huo ndo mwendo wa kwenda, Kenya wametuchelewesha sana!