Hatimaye dawa ya Kenya kukwamisha Maendeleo Tanzania imepatikana rasmi!

Hivi mbona mataga ya Lumumba mnadanganya watu hivyo. Yaani mshindwe kuwaletea wananchi msingizie wakenya. Achen ujinga aisee. Mnaanzisha mipango wenyewe halafu mnasingizia jiran ndo anakuamisha hiyo mipango huo ni ujuha wa hali ya juu mnoo aisee. Hizi sababu zote ulizizitoa hapa hazina mashiko. Kwa ufupi mmeshindwa kuendesha nchi. Mnatumia Dola tu.

Rasilimali tulizonazo mmeshindwa kuondoa watu kwenye umaskin. Mnasingizia Kenya.

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 

Ukiona mtu kwa kushindwa kwake maisha analaumu wengine jua ni kichaa, huwezi kufanikiwa kwa kutupia lawama wengine kwa matatizo yako mwenyewe haipo hiyo
 
Unahitaji elimu sana juu ya espionage
 
Poor exposure ndio kinawatafuna ccm , exposure sio kutembea nchi nyingi hapana tuna maana exposure ya kiakili maana wana ccm ukisema exposure wanapanda ndege kwenda ulaya na marekani wakihisi ndio exposure kumbe hawajielewi,
 
Ukiona mtu kwa kushindwa kwake maisha analaumu wengine jua ni kichaa, huwezi kufanikiwa kwa kutupia lawama wengine kwa matatizo yako mwenyewe haipo hiyo
Shida sio wewe! Shida ni akili yako na upeo wako! kukosa kwako exposure unashindwa hata kuelewa dunia inaendaje

Kwa taarifa yako hakuna cha bahati mbaya duniani! Kila nchi inafanya umafia kwa faida yake. Hakuna kitu cha bahati mbaya
 
Poor exposure ndio kinawatafuna ccm , exposure sio kutembea nchi nyingi hapana tuna maana exposure ya kiakili maana wana ccm ukisema exposure wanapanda ndege kwenda ulaya na marekani wakihisi ndio exposure kumbe hawajielewi,
Exposure sio kupanda ndege

Elegant mada ndo uchangie kama hujaelewa omba ueleweshwe
 
Shida sio wewe! Shida ni akili yako na upeo wako! kukosa kwako exposure unashindwa hata kuelewa dunia inaendaje

Kwa taarifa yako hakuna cha bahati mbaya duniani! Kila nchi inafanya umafia kwa faida yake. Hakuna kitu cha bahati mbaya

Nimekupa tafsiri ya exposure kwa current world maana wewe poyoyo unadhani kuland airport nyingi ndio exposure kumbe tunamaanisha mindset exposure, ndio maana mnabaki mnadandia mambo ili msingizie wengine corona, vita ya ukraine ndio vichaka vyenu nasubiri na mkimaliza kuwalaumu kenya muanze kuwalaumu Rwanda na Congo vita yao imefanya maisha yapande si ndio au?
 
Miradi ya Bandari ya Bagamoyo na KIGAMBONI iliuliwa na Marehemu Mwendazake.
 
Naona somo limekuingia. Tulia sasa na jifunze kusimamia maslahi mapana ya nchi yako

Huo ukhanithi wa neno maslahi mapana ya nchi naona mmelishana mnadhani kila mtu anatabia ya kujikomba.
 
Ukielewa diplomasia ya uchumi huwezi kuandika huu upuuzi ulioandika hapa

Umeshawai ona Rais wa Marekani akiisema vibaya Urusi anapokutana na Rais wa Urusi?
Si anamwogopa mbona waafrica wote tumeitwa kuwa ni shit hole na rais wa marekani
 
Imagine mleta mada ndio alikuwa tegemeo la Lisu kwenda ikulu!
 
hivi kigamboni ilikuwa wa[ewe wamarekani wajenge satellite city au kituo cha kijeshi?

miradi inayohusiana na wachina siyo ya kupigia chapuo, hata wakenya wanajuta leo kujengewa sgr na wachina. na bado bandari ya lamu. itafika wakati si bandari ya mombasa tu hata mamlaka ya mapato ya kenya inaweza ikachukuliwa na wachina siku moja ili wasimamie deni lao lilrudi. Wachina ni kama wale wakopeshaji wanakaa na card za benko za walimu
 
Uhasama baina ya Kenya na Tanzania ni UTANI tu wa asili kama watoto mtu na mdogo wake wanavyokuwa na uhasama hapa na pale lakini wanabaki kuwa ndugu, nothing serious, joto kama hili huwa linapanda na kushuka katika vipindi tofauti, na hali itaendelea kuwa hivyo hivyo milele!
Mbona Tanzania ilipowahujumu Kenya na kuliteka bomba la mafuta kutoka Hoima kwenda Tanga badala ya Mombasa na kila kitu kilikuwa kimeshakamilika, lakini hujaandika kwamba trunataka kukwamisha maendeleo ya Kenya? Acheni kihemuhemu kama kuku mtetea anayetafuta kupandwa!
 
Miradi ya Bandari ya Bagamoyo na KIGAMBONI iliuliwa na Marehemu Mwendazake.
Je, mwendazake alikuwa na hoja au zilikuwa papara tu. Baadhi ya wahafidhina wanaulinganisha mradi wa Bagamoyo na ule wa Sri Lanka ambao umeiacha nchi mahututi kiuchumi na mchina amekaa pembeni utadhani hahusiki. Hata wakenya wanalizwa na deni la mradi wa SGR. Bado wakopeshaji, wajenzi na waendeshaji wa miradi yote ni wachina. Je, kuna ukweli katika ulinganisho huo. Tuelezane, na bila ushabiki, ukweli ni upi. Baada ya kupata ukweli ndipo tutaweza kumbembesha lawama mwendazake.
Miradi ya Bandari ya Bagamoyo na KIGAMBONI iliuliwa na Marehemu Mwendazake.
 
Wameshikwa papaya safari hii! Hawana pq kutokea

Na hatua ifuatayo tunagawa vitambulisho vya uraia kwa Watanzania wote Ngorongoro na Loliondo! Mtu akiingia lazima aoneshe kitambulisho safari hii
Kenya wanajiona wana akili nyingi yale yale ya Kagame na fitina za mpaka wa DRC. Hatimaye wakongomani wamechoshwa kuwatumikia watu fulani wachache tu.
 
Kenya watatuachaje nyuma wakati wanategemea almost kila kitu kutoka Tanzania?

Leo hii ukifungwa mpaka, athari kwa Tanzania itakuwa fedha ila kwa Kenya ni pesa na njaa juu
Mkuu, ni wazi huelewi 'dynamics' za nchi hizi mbili, hasa za hao Kenya zinavyofanya kazi. Ushauri wangu kwako, jaribu kuelewa wanavyoendesha mambo yao na msukumo unaowafanya wajibidishe ku'undermine' juhudi zetu kila mara.

Uchambuzi uliouweka pale juu ni 'shallow' sana.
 

Chanzo cha ugomvi ni Kenyatta kuukataa Muungano. Nyerere alitaka Kenya iungane na Tanganyika baada ya hizi nchi kupata uhuru tena alikuwa tayari kumwachia Kenyatta aongoze lakini Kenyatta alikataa. Muungano ukabaki kuwa wa Tanganyika na Zanzibar.
 
2015 na 2020 mlidai ni Wapinzani ndiyo wanawachelewesha,imekuwa ni Kenya tena?CCM hakuna mnachoweza zaidi ya kutafuta vichochoro vya kusingizia wengine kwa matatizo mliyoyasababisha wenyewe!Mkenya gani aliyewaambia serikali ya CCM kuwa Wamasai ni waharibifu wa mazingira/uhifadhi?
Hizo propaganda zenu haziwezi kuwaponya.
Sisi Wananchi wa Tanzania tunataka kuandika Katiba Mpya kuanzia pale ilipoishia Rasimu ya Jaji Warioba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…