Hatimaye Gerald Hando aaga rasmi kambi ya Ukapela

Hatimaye Gerald Hando aaga rasmi kambi ya Ukapela


image-jpeg.384993



Kaoa mzungu?
 
Haaa hongera zake vp hapo ndo huyo alieshika mike au ni huyo alovaa koti jekundu!
 
Zamani mtu ukivuta jiko au kuoa.....unaheshimika sana mbele ya jamiii.......na kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wenzako......

Kutokana na ndoa kugeuka kuwa magereza ya mateso.....na vifungo vya dhiki.....kijana kuoa imekuwa habari ya kushangaza sana na pengine kukuonea huruma.....

Wakati wao wanakushangaa.....na wewe unawashangaaa.....
kweli umekata tamaa
 
Ndoa zingekuwa kama unavyozielezea nafikiri tusingezishuhudia ktk nyumba za ibada na kusingekuwa na familia maana hakuna apendae gereza.

Visa vya taraka vinaongezeka kadri zinavyokwenda.....hii ni ishara kuwa kadri zinavyokwenda ndoa zinapoteza mvuto....na sababu kuu ni kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa wanandoa.......

Na hata wale ambao bado wapo kwenye ndoa....wanavumilia kuwepo huko si kwamba wanafurahia kuwepo huko......
 
Unakaa nchi gani wewe??? Tanzania hii kuna mwanaume atake kuoa na ashindwe(akose)?????

Hata kama ni hanithi. Mwanaume hakosi mke wewe kwa jinsi walivyojaa
Hata mimi nimemshangaa hadi nikahisi huenda sijamuelewa anamaanisha nini! Ilinichukua zaidi ya dakika 1 naikodolea macho post yake kabla sijaijibu... niliamini sijamuelewa!
 
Hao hao wembamba wengine wanaasili ya unene wakishaolewa wakazaa wanajiachia wanakuwa wanene..lakini kwenye harusi hapo utasema miss si huyu.
Kila mtu anataka kuoneka vizuri kwenye picha za harusi, si ajabu hapo imepita miezi 4 ya kushinda na njaa.
 
Wazazi wako hawakutakii mema ujue kuna wakati maisha ya kisela kwako inabidi yabaki historia ukioa unajifunza mengi sana katika maisha ukijumlisha pamoja na majukumu ya kuwa na familia
Nini unachojifunza ukishaoa? Wezi wote nchi hii nao wameshaoa! Waliokuwa wanatorosha makontena kule bandarini nao wameshaoa! Wazinzi wote ni wale wale ambao wameshaoa! Ni hao hao ambao wameshaoa, utakuta badala ya kutunza familia, wanaitekelekeza kwa ajili ya nyumba ndogo! I am sorry Sir, there's nothing to learn toka kwa wenye ndoa zaidi tu ya kujiunga kwenye timu ya mafedhuli!
 
Nini unachojifunza ukishaoa? Wezi wote nchi hii nao wameshaoa! Waliokuwa wanatorosha makontena kule bandarini nao wameshaoa! Wazinzi wote ni wale wale ambao wameshaoa! Ni hao hao ambao
wameshaoa, utakuta badala ya kutunza familia, wanaitekelekeza kwa ajili ya nyumba ndogo! I am sorry Sir, there's nothing to learn toka kwa wenye ndoa zaidi tu ya kujiunga
kwenye timu ya mafedhuli!
So unataka kusema hata wazazi wako hawaishi pamoja? Hawakuoana?
 
Back
Top Bottom