Hatimaye Hotel ya Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi 'Sugu' yafunguliwa

Hatimaye Hotel ya Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi 'Sugu' yafunguliwa

Serikali ya ccm wasije wakaipiga X tu waseme kavamia eneo...... la ujenzi wa reli
 
Kwakuwa ni chadema na msanii tutasema hongera sana Kamanda..ila angekuwa ccm hapa tungesema ni fisadi..tukapimwe akili
View attachment 579593
Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama ‘Sugu’ alianza kuijenga hoteli yake toka mwaka 2016 jijini Mbeya na aliweka wazi kabisa kwamba alipata mkopo wa kuijenga kutoka CRDB BANK.

Itafahamika kwa jina Hotel Desderia

Tayari hoteli imefunguliwa na kuna nafasi za kulaza wageni kwenye room zilizojengwa kisasa lakini pia hata kwa chakula ni bora ambapo mchakato wa kumpata Mpishi ulipatikana kwa njia ya usaili, ukitazama kwenye hizi picha hapa chini utaona chakula alichokitoa Mpishi alieshinda kwenye huo usaili.
View attachment 579603
Mojawapo ya sample iliyoandaliwa kwenye usaili

View attachment 579594
muonekano wa nje

View attachment 579595
Padri akinyunyizia maji ya baraka kuizunguka hotel

View attachment 579596
baadhi ya wageni wakipata huduma


Hongera umehustle sana na maisha
Politics ni ajira nzuri naona umuhimu wa wizara ya elimu kuongeza somo la siasa kwenye mtaala ili watu waijue miiko yake kwa sababu watu wengine ni wabwabwajaji kama baadhi ya viongozi wa siasa kutoka ccm na upinzani, siasa inakumfanya mtu kuwa brand kubwa na uwezekano wa kuitumia kibiashara upo.

Sugu ni akili kubwa hutosikia akiburuzwa mahakamani na serikali kila leo hana muda huo he is always thinking of business.

Thumb Up kwa Mh Sugu au Jongwe kama yeye anavyopenda kujiita

Source millard
 
Hongera Mr. Sugu. Ila majengo ya hiyo hotel yananikumbusha maisha ya hostel kipindi nasoma
 
Safi sana Sugu Mimi si shabiki yako katika mambo mengi yakiwemo siasa lakini kwenye jambo hili la maendeleo na kupongeza sana na Allah akujalie zaidi uweze kulipa huo mkopo na ikiwezekana uwekeze pengine...
Hongera sana..Sugu.
 
iliyomuingizia pesa kumiliki hiyo kitu.
Tatizo tunapenda kuonyesha tuna nini sio tumevipataje ili awape inspiration vijana anaowawakilisha huko.

mikopo
kilimo
ubunge kajichanga etc
natanguliza hongera kwake lkn
Great thinker mkuuuu ... Tumfanye kijana kua inspired na njia tulotumia kufanikiwa nasio Mafanikio tulonayo .

All in all ,shout out to you Mr.Sugu.
 
iliyomuingizia pesa kumiliki hiyo kitu.
Tatizo tunapenda kuonyesha tuna nini sio tumevipataje ili awape inspiration vijana anaowawakilisha huko.

mikopo
kilimo
ubunge kajichanga etc
natanguliza hongera kwake lkn
Inaonekana hata post nzima hujaisoma,umekimbilia kuandika tu.Kwenye Post hapo juu,imeandikwa kabisa Sugu amesema ni mkopo toka bank ya CRDB.

In this world,It doesn't matter who you are,But what you do to Survive.
 
Chakula alichokitoa mpishi aliyeshinda ni kiboko! Hotel iko Mbeya sehemu gani? Hongera Sugu!
 
Aangalie tu..... Sisiem sio watu... Mbowe wanazidi mfilisi tu

Ila kawazidi hadi bosi zake akili....
 
Back
Top Bottom