Hatimaye jana uso kwa uso huyu Kicheche na cha moto kakipata

Hatimaye jana uso kwa uso huyu Kicheche na cha moto kakipata

Huyu itakuwa ndio kama aliemkata kuku wangu kichwa nini..?maana juzi nimekuta kuku wangu mkubwa amekufa kichwa kimekatwa kama aliechinjwa na hakipo...
 
Huyu itakuwa ndio kama aliemkata kuku wangu kichwa nini..?maana juzi nimekuta kuku wangu mkubwa amekufa kichwa kimekatwa kama aliechinjwa na hakipo...
Pole mkuu huyu mdudu katili sana.
 
Vicheche nuksi sana... Ila kuna yule mwingine anakamata anachinja hlf ananyonya damu tu , hali nyama hata kidogo... sijui anaitwaje
Ata huyu siyo aisei, kaangusha viranga wawili faster in a minute.. Mama yao alimshinda kamtia jeraha mgongoni.
 
Muda sasa takribani mwaka na miezi nasumbuana na huyu kicheche. Kicheche huyu bwana ni kama alikuwa anatumwa, amekula viranga na kuku wangu sana, huwa anafumua nyavu za banda na kutinga ndani usiku, anasomba vifaranga kimyakimya nikiamka mama kuku hana viranga.

Mara chache sana huwa inatokea mama kuku akistuka nitaamshwa na mayowe makubwa natoka nduki bandani mara mlango ukilia tu, huyo anasepa.

Sasa jana shetani wake kazidiwa ujanja na Mungu wangu akamtuma mapema sana, kabla ya saa mbili maana amezoea huwa anazamia mida ya wachawi usiku wa manane, jana nikiwa nipo nje napunga upepo natega nikaone taarifa ya habari nikasikia kelele za mama kuku, nikatoka nduki hadi bandani abadani USO KWA USO na huyo mbaya wangu kicheche, nilichofanya nikazima taa na kuwasha hivyo hali ile ili mchanganya sana KICHECHE akapotea njia yake aliyochonga kwa pesa ya makinikia.

Mungu saidia nikakimbilia upande alipo chonga njia, ile anataka apande nilimpa buti la haja, akatoa mlio kama simba, kidogo nijikojolee kujikaza kiume nikamuita mshikaji wangu njoo huku vita ni vita mura takenya mura waituuh..(hapa najua ni akina mwita na bhoke wameelewa).

Kicheche kanichimba biti, na Mungu saidia nikapata kipande cha ubao nikaenda naye SAKO KWA BAKO anakala rugu ya kichwa mara chini ila sema ukweli hii vita ilikuwa kubwa mno..! Mungu saidia nikawa nimeshinda vita na kicheche mwenyewe huyu hapa chini[emoji116][emoji116][emoji116]View attachment 621811View attachment 621812View attachment 621813View attachment 621814

Wataalam mnaojua vicheche njooni mtwambie huyu kicheche wa namna gani, na anawezaje kuishi mjini kabisa dsm, katikati ya mji maana sikai maeneo ya mashambani.

Nasubiri vita iendelee maana naamini atakuwa na familia niombeni nishinde vita hii.

ASANTENI .
Mfanye kitoweo
 
Huo sio ubalozi mkuu. Hiyo ndo ikulu yenyewe...! Yaani hapo haruhusiwi hata kugusa geti..! [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]

Ni rahisi mtoto kuchezea maziwa ya mama yake kuliko kuchezea makende ya baba yake. Kaguta Museveni.
 
Back
Top Bottom