Hatimaye Kibanda awataja waliomtesa

Hatimaye Kibanda awataja waliomtesa

FUHRER

Member
Joined
May 29, 2013
Posts
87
Reaction score
644
Jamani mimi ni mtaalamu wa nadharia za njama (ConsipiracyTheoretician) by profession lakini pamoja na facts nilizo nazo, nimejaribukutengeneza theory kibao kuhusiana nakutekwa kwa Kibanda, lakini kila niki-feed facts katika hypothesisnilizotengeneza zinakataa. Nafasi iliyokuwa imebaki ku-prove theory zanguilikuwa ni kumsikiliza kibanda mwenyewe face to face na kuyasoma mawazo yake. Leokibanda kaongea kwa mara ya pili tokea arudi kutoka Afrika ya Kusini akiwaametulia zaidi channel 10 katika kipindi cha Generali on Monday. Pamoja nakuzunguka sana na kujitahidi asitaje jina la mtu wala taasisi, lakini bilakujua amewaondoa ambao walikuwa wanatajwa kuhusika na hivyo kutusaidia watutuliokuwa tunafuatilia sakata lake tukiwa na nadharia nyingi ku-narrow down nakupunguza nadharia na kubakiwa na chache ambazo zina mantiki.

Facts Alizoziongea kibanda Channel 10 leo ambazozina-eliminate theory nyingine zote ni hizi,
1. Watuwaliomteka wana nguvu na uwezo wa kifedha
2. Watuwaliomteka wana madaraka wanauwezo wa kuingilia uchunguzi na kuamrishauchunguzi uelekee wanakokutaka wao.
3. Wapowatumishi wakubwa wa serikali waliostaafu kwenye vyombo vya dola wanaofuatiliauchunguzi huu bila kuyumbishwa.
4. Vyombovya dola na baadhi ya waandishi wamefanya jitihada za makusudi kupotosha tukiozima la kutekwa kwake
5. Watekajisio watu barabarani ni watu wenye utaalamu wa kusomea wa jinsi ya kumdhurubinadamu
6. Tukiohili lina uhusiano wa moja kwa moja na kazi yake kibanda kama mwandishi namtazamo wake katika yale anayoyaandika.

Kwa facts hizi alizoongea Kibanda ukijumlisha namwonekano wake (body language) pale studio kuna theory moja tu ndio inabakinayo ni “Kibanda kateswa na kikundi cha watu waliopo serikalini wenye madarakaau wanaotaka madaraka ambao wana baraka zote za mkuu wan chi (Raisi) ndio maanahakuna linalofanyika kuhusiana na kesi ya kibanda zaidi ya siku 100 tokea ateswe”.
 
Hakika kama hataki kuwataja basi nae ni mmoja kati ya watu wasiopenda maendeleo ya taifa hili kwani kuwataja hawa watu kutapelekea uchaguzi uja waTz kuwakataa kwa nguvu ya sanduku la kura endapo serikali haitawafungulia mashtaka pia atakuwa amewasaidia waTz wengine watakaodhuriwa baadae na hawa watu, so kibanda kuwa Mzalendo
 
mi naombeni kujua marudio ya jenerali on monday ili niweze kuangalia alichozugumza na kuulizwa ama wale wataalum wa video kama mnayo tuwekeeni humu jamvini ili tutililike.
 
Wenye akili wameshajua, ila kauli ya kibanda ambayo iliniuma ni kuwa " Hakudhani kuwa jambo hili lingeweza kuja mtokea yeye, alidhani huwa yanawatokea wao akina Mwangosi na waandishi wengine ambao wamewahi patwa .....na akina ulimboka . . . .. Kumbe hata kwake yanaweza". Mwandishi hulazimishwi, ila unashauliwa kutumia kalamu yako kwa haki . . . haki haimtupi mtu. Kwa Kibanda kuna untold story otherwise angeweza kufunguka zaidi kuwa bahasha ngapi amewahi pata, na amewahi hakikishiwa usalama wake inawezekana na mtu ambaye mpaka leo wewe mwandishi wa habari unaogopa hata kumsalimia na hata hakujui na bado yalimpata Kibanda. . . . . Jikague upya mshika kalamu.
 
Kazi ya uandishi wa habari ni ngumu kwa sababu kila siku unagusa maslahi ya wenye nguvu kwa namba chanya au hasi. Ukigusa kwa namna chanya au hasi repercussion zake ni kubwa sana in all directions. Sidhani kama waandishi wanaelewa haya. Ninawaonea huruma, leo kwa Kibanda kesho kwa mwingine yeyote. Kama waandishi wangekuwa na umoja na kuacha tama wangepona alipouawa Mwangosi. lakini wahariri wameandika kidogo wamekaa kimya. Leo yamemkuta Kibanda wameandika kidogo, hakuna aliyefanya uchunguzi wa maana, wamekaa kimya.Kesho itatokea kwa mwingine.
 
sasa tumuamini nani km hata yeye Kibanda anashindwa kuwataja? mbona kuna mitandao mingi atume yoyote awataje kuliko kuwaficha km Ulimboka.
Humu JF kuna taarifa za wenzake Waandishi waliunda Tume na wakaileta humu sasa tuamini ipi?
 
[h=2]''Hatimaye Kibanda awataja waliomtesa'' Kichwa cha habari na ulichoandika ni tofauti kabisa. Ni nan ambaye hajui kuwa alitekwa na watu...?! Hiyo habar imejaa watu, watu, watu , watu......!!! Pretender mkubwa wee[/h]
 
Kibanda. Unakumbuka ulivyomfagilia Kinana. Oo Kinana Jembe! Aje akusaidie kupata haki huyo jembe lako!
 
Hawezi wataja hata siku moja na pia hata ungekuwa wewe usingewataja kwani hata akiwataja hawatachukuliwa hatua yoyote na pia ni hatari kwa uhai wake. Bora achune tu kwani yeye hapendi kuishi!??? Tujifunze kwa Olimboka.
 
Jamani mimi ni mtaalamu wa nadharia za njama (ConsipiracyTheoretician) by profession lakini pamoja na facts nilizo nazo, nimejaribukutengeneza theory kibao kuhusiana nakutekwa kwa Kibanda, lakini kila niki-feed facts katika hypothesisnilizotengeneza zinakataa. Nafasi iliyokuwa imebaki ku-prove theory zanguilikuwa ni kumsikiliza kibanda mwenyewe face to face na kuyasoma mawazo yake. Leokibanda kaongea kwa mara ya pili tokea arudi kutoka Afrika ya Kusini akiwaametulia zaidi channel 10 katika kipindi cha Generali on Monday. Pamoja nakuzunguka sana na kujitahidi asitaje jina la mtu wala taasisi, lakini bilakujua amewaondoa ambao walikuwa wanatajwa kuhusika na hivyo kutusaidia watutuliokuwa tunafuatilia sakata lake tukiwa na nadharia nyingi ku-narrow down nakupunguza nadharia na kubakiwa na chache ambazo zina mantiki.

Facts Alizoziongea kibanda Channel 10 leo ambazozina-eliminate theory nyingine zote ni hizi,
1. Watuwaliomteka wana nguvu na uwezo wa kifedha
2. Watuwaliomteka wana madaraka wanauwezo wa kuingilia uchunguzi na kuamrishauchunguzi uelekee wanakokutaka wao.
3. Wapowatumishi wakubwa wa serikali waliostaafu kwenye vyombo vya dola wanaofuatiliauchunguzi huu bila kuyumbishwa.
4. Vyombovya dola na baadhi ya waandishi wamefanya jitihada za makusudi kupotosha tukiozima la kutekwa kwake
5. Watekajisio watu barabarani ni watu wenye utaalamu wa kusomea wa jinsi ya kumdhurubinadamu
6. Tukiohili lina uhusiano wa moja kwa moja na kazi yake kibanda kama mwandishi namtazamo wake katika yale anayoyaandika.

Kwa facts hizi alizoongea Kibanda ukijumlisha namwonekano wake (body language) pale studio kuna theory moja tu ndio inabakinayo ni "Kibanda kateswa na kikundi cha watu waliopo serikalini wenye madarakaau wanaotaka madaraka ambao wana baraka zote za mkuu wan chi (Raisi) ndio maanahakuna linalofanyika kuhusiana na kesi ya kibanda zaidi ya siku 100 tokea ateswe".

Hitimisho lako hapo chini limejaa uzushi wenye lengo la kumchonganisha Rais/ Vyombo vya dola na wananchi. Hii ni tuhuma nzito kwa Rais, hivyo unapaswa kuthibitisha hili, unaposema kwamba Kibanda aliteswa kutokana na baraka za Rais Kikwete... Unaweza kuthibitisha hili? watu wengine bana , kujitafutia matatizo tu. Kwani kwenye sheria kuna ukomo wa uchunguzi wa criminal conduct? Kuna 100 days deadline??? Rubbish. Watu kama wewe ni hatari kwa Taifa letu.
 
Kikweli bahasha huwa zinawaponza sana waandishi,wanamtumikia fulani kwa kumchafua fulani......pole sana kibanda ila naamini ukweli unaujua zaidi ww mwenyewe,suala la kutowataja watesi wako sidhani kama linakusaidia zaidi ya kuweka watanzania gizani na kuhisi kama hivi tunavyosoma hapa.
 
Kwa staili hii ya kuficha majina ya watuhumiwa, wengi watang'olewa kucha na meno
 
Kama hawezi kuwataja akae kimya

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Watanzania tuna matatizo makubwa,
Kama mtu anawafahamu watesi wake kwanini asiwataje?
Imefikia mahala vyombo ya usalala wa raia na mali zao imekuwa haiaminiki kiasi hiki!
La hasha!
Serikali hii inakoelekea ni kubaya,haki imekuwa tunu ya thamani ambayo watanzania wa kawaida kuipata ni Adimu.
Mungu ibariki Tanzania
 
Kuna siri kubwa sana ambayo wateswa wote wanayo moyoni, na wanalishwa Yamini kali sana ambayo haiwezekani kuicross kwa namna yoyote(nadhani baadhi yenu mmesoma mambo ya viapo vya freemasons ambapo wanapewa kiapo at dagger-point), yani kitu cha ncha kali kinasogezwa shingoni wastani wa milimita mbili toka kwenye koromeo!

Haiwezekani wote wakirudi wanazimika ghafla na kuwa kondoo, huku wakiongea kwa kuchagua maneno sana.

Ulimboka kwasasa hatujui hata alipo au anafanya shughuli gani, nadhani ukimwambie aongelee watesi wake mtakorofishana sana. Alimtaja yule mng'oa meno wa UwT baada ya Kubenea na Mwanahalisi kumweka hadharani, huenda bila hivyo angekauka!

Mwakyembe ndo huyo, pamoja na kuahidi kuwa na maongezi na waandishi lakini hakuthubutu kutaja jina la wabaya wake, huku akiishia kusindikizwa makanisani na Akina Sitta kutoa sadaka...kimyaa, mpaka kesho.
 
Back
Top Bottom