Hatimaye kikokotoo chalegezwa, Serikali imepandisha Malipo ya Mkupuo kwa Wastaafu kutoka 33% hadi 40%

Kwa nini isiwe 50% apewe mstaafu 50% ibakie kwenye mfuko? Win win situation
 
Madogo ambao mnaishi kwa shemeji zenu mna maneno sana. Ebu toa maelezo namna ya kujipanga kwa mwalimu anaye lipwa laki 4 na hana posho yoyote mwaka mzima huku akiwa na wategemezi kadhaa.
Anataka ajilipe humo humo,haya maisha ndo siku hizi tunayashuhudia
kijana anaajiriwa leo,kichwani anawaza wizi tuu ili akistaafu asifanane na baba yake aliyejaza makabati kwa
hati za uadilifu akaishia kuchekwa na wadanganyika kwamba hakujipanga alipokuwa kazini.
 
Hivi unajua kwamba hiyo monthly pension unalipwa miaka kumi tu na ikitokea hujafa
basi mzigo ni wako na familia yako?
Ni heri wangeachana na kikokotoo watoe pesa yote kila mtu ajijue
kwani wabunge wanaolipwa mafao yao yote wanaishi vipi?
Sasa wabunge wanapewa sh ngap wakiwa na umri gn na labla wengine wanaweza kurudi tena bungeni au wakarudi kwenye System ya serikali halafu jilinganishe na ww ambaye ukistaafu ndio imetoka
 
Madogo ambao mnaishi kwa shemeji zenu mna maneno sana. Ebu toa maelezo namna ya kujipanga kwa mwalimu anaye lipwa laki 4 na hana posho yoyote mwaka mzima huku akiwa na wategemezi kadhaa.
Mm naishi kwa shangazi yangu, kwahy huyo mwalimu akistaafu ndio atatoboa kwa hayo mafao yake? Aisee kwa akili hizo serikali ipunguze hata hy 40% ya mkupuo mana mkipewa pesa zote hizo mtakufa mwaka wa kwanza wa kustaafu.
 
Kwahy unataka uwe mwadilifu mwnyw katikati ya wapigaji? Mama mwnyw amesema ule urefu wa kamba yako
 
Hivi unajua kwamba hiyo monthly pension unalipwa miaka kumi tu na ikitokea hujafa
basi mzigo ni wako na familia yako?
Ni heri wangeachana na kikokotoo watoe pesa yote kila mtu ajijue
kwani wabunge wanaolipwa mafao yao yote wanaishi vipi?
Ndio shida ya kutokuwa na taarifa sahihi halafu mtu anafanya maamuzi Kwa taarifa zisizo sahihi
Pension ya mwezi mtu analipwa maisha yake yote Hadi anafariki hata Aishi miaka 1000 ataendelea kulipwa ni yeye tu kuendelea kuishi
 
Mkuu ni wachache sana tunaelewa maana ya kikokotoo. Wengine badala ya kutaka kuelewa wanafuata mkumbo tu. Ila umemalizia vizuri, mtoto akililia wembe, mpe!
 
Ndio shida ya kutokuwa na taarifa sahihi halafu mtu anafanya maamuzi Kwa taarifa zisizo sahihi
Pension ya mwezi mtu analipwa maisha yake yote Hadi anafariki hata Aishi miaka 1000 ataendelea kulipwa ni yeye tu kuendelea kuishi
Na ukilipwa yote, hizo za Kila mwezi ndio imeisha hvy au
 
Ndio ukilipwa Zote hakuna pension ya mwezi na duniani kote hakuna nchi inalipa pesa Zote za pension Kwa mkupuo hazipo
Duh sasa hawa raia humu wanaotaka kulipwa zote, kama hizo akili ndio walikuwa wanazitumia huko kazini bc walikuwa mizigo huko kazin
 
Monthly pension itashuka sema waliobeza kikokotoo hawajielewi kuwa kadri unavyochukua Hela ya mkupuo kubwa monthly pension inashuka na Maisha ni monthly pension sio Hela ya mkupuo

Hela ya mkupuo hukata upesi
Sikia wewe Chawa. Kikokotoo kimeondoa monthly pension. Pesa ya mkupuo ndiyo hiyo imegawanywa na kufanya 33% unapewa, 67% ndiyo imefanywa monthly pension kwa Miaka 12. 5. Ile Pension kama Zamani iliyokuwa Watu wanapata 50% mkupuo haipo. I mean ikiwa ulistahili mkupuo 180m. Unapewa 80m, 100 ndiyo unagawiwa monthly kwa Miaka 12.5. ikiisha na bado unaishi ndiyo watakutafutia Pension Sijui toka wapi. Kwa hiyo Mstaafu Mafao yake ya Mkupuo ndiyo yamegawanywa kwa Staili hiyo. Kama vipi Wachukue 33% na 67% apewe Mstaafu Mkupuo wake.
 
Ndio ukilipwa Zote hakuna pension ya mwezi na duniani kote hakuna nchi inalipa pesa Zote za pension Kwa mkupuo hazipo
Siyo kweli. Back June 2022 Wastaafu walipewa 50% na Pension yao ipo Kila Mwezi tena kubwa tuu. Ulishawahi kusikia hao wakilalamika?? Bcoz walipewa Haki Yao Vizuri kama Mikataba ya ajira ilivyoianisha walivyoajiriwa. "Permanent and Pensionable "
 
Yaani wabaki na asilimia 33 wakupe monthly pension ya Kila mwezi asilimia 30 ya mshahara ulikuwa Ukipata kazini si utakufa baada ya muda mfupi tu

Mfano pension. Milioni 100 wanakupa milioni 70 hivi mtaani mnakujua hamkujui? Milioni 70 utafanya Nini Cha maana mtaani? Cha kukuingizia kipato.cha mwezi Cha kueleweka

Ukizeeka kubali tu kuwa Wewe tegemeo lako pension ya mwezi
 
Kwani wanakufa Mtaani no Wazee Wastaafu tuu? Hata wakifa wewe Una uchungu gani na wao? Wanakufia wewe au familia zao? Wazee wapewe Haki Yao ya Mafao ya Mkupuo. Mbona hii Huruma haiko kwa Vijana Wahitimu wa Vyuo wanaozurura Mtaani bila Ajira??
 
Kwa nini isiwe 50% apewe mstaafu 50% ibakie kwenye mfuko? Win win situation
Kwa formula hiyo.mfanyakazi ndie ana loose Serikali Haina Cha kupoteza maana yake ni kuwa mfanyakazi akichukua 50 monthly pension yake itakuwa nusu ya mshahara Aliokuwa Akipata kazini kadiri unavyopandisha asilimia ya pesa ya mkupuo upande wa pili wa monthly pension unashuka
 
Waweke mia% Mbona hao wabunge wapuuzi sana miaka m5 TU wanapata 280mil? Uonevu wa hali ya juu sana! Dadeki!
Hakuna nchinyeyote duniani inayolipa mfanyakazi wake akistaafu pension asilimia mia moja

Ubunge Sio ajira na hawalipwi mafao na mifuko ya pension

Asikimia mia hazipo nchi yeyote duniani
 
wanapaswa kuachia iwe 100% kabisa, kama mtu alikuwa anachangia, kwanini mnampangia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…