Hatimaye kikokotoo chalegezwa, Serikali imepandisha Malipo ya Mkupuo kwa Wastaafu kutoka 33% hadi 40%

Hatimaye kikokotoo chalegezwa, Serikali imepandisha Malipo ya Mkupuo kwa Wastaafu kutoka 33% hadi 40%

Sio lazima watumishi wote kulipwa kwa kikokotoo kimoja. Wanaweza kupewa options kila mti achague kilingana na circumstances zake. Unaweza kuweka options tatu;
1. No lump sum. Mtu analipwa pesa ya mwezi tu kwa kiasi kinachokaribiana na mshahara aliokuwa analipwa.

2. Lump sum 25% , kinachobaki analipwa monthly.

3. 40% lump sum, kinachobaki analipwa monthly.

Watu wanatofautiana circumstances, kwahiyo kukiwa na namna moja tu ya malipo, wapo watakaoathirika. Hali hiyo inaepukika kwa kuwapa options.
Uko sahihi
 
Sa
Monthly pension itashuka sema waliobeza kikokotoo hawajielewi kuwa kadri unavyochukua Hela ya mkupuo kubwa monthly pension inashuka na Maisha ni monthly pension sio Hela ya mkupuo

Hela ya mkupuo hukata upesi
Sasa unataka hiyo Hela ukatumie Mbinguni? Umestaafu una miaka 60, kufikisha 70-80 Bahati,Sasa Hela ibaki serikalini ya Nini? Halafu unamaana nikishastaafu nitashindwa kabusaaa kuishi eti Mshahara mdogo? Wazee wetu ambao hawakuajiliwa mbona wanaishi fresh TU na wanatoboa 70-90 huko? Acheni vitisho bwana
 
Mama tunampenda sana - apongezwe kwa hatua HIYO. Lkn aone umuhimu wa kukiondoa kabisa wafanyakazi walipwe 100 na wakizila zikaisha wajijue wao
 
Akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali Bungeni, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imesikia kilio cha Wastaafu na hivyo imepandisha Malipo ya Mkupuo kutoka 33% hadi 40%

Pia, Dkt. Mwigulu amesema Rais Samia ameagiza kuongezwa kwa malipo hayo kwa Wastaafu waliokuwa wakilipwa 25% sasa watalipwa 35% katika Mwaka huu wa Fedha


====

Pia soma: LIVE - Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, leo Juni 13, 2024 Bungeni, Dodoma
Binafsi nashukuru hata kwa hili limewatea nafuu wastaafu, ingawa bado uwiano haufai.

Walau tufikie kwa mtu anaye staafu kwa miaka 60 apate 70% matarajia hapa life expectance hivyo amalize vimeo vyake duniani na familia ifurahie utumishi wake.

Kwa wale wanaostaafu kwa hiari walau wapate 55%.
 
Niache kuishi kwa raha wakati napokea 100% ya mshahara wangu nije kuishi kwa raha wakati napokea 75% ya mshahara?! kama sielewi hivi
Hata Mimi hapo aijapaelewa vizuri, Halafu kinachonishangaza ni pale watu hujifanya wanatuonea hurumaa kana kwamba mtumishi hawezi kuishi nje ya Mshahara.Wekeni 50/50 hakuna mtu atalalamika
 
Monthly pension itashuka sema waliobeza kikokotoo hawajielewi kuwa kadri unavyochukua Hela ya mkupuo kubwa monthly pension inashuka na Maisha ni monthly pension sio Hela ya mkupuo

Hela ya mkupuo hukata upesi
Asante kwa SoMo hili
 
Monthly pension itashuka sana waulize wastaafu waliolipwa mkupuo asilimia 25 wanaishi maisha ya Raha sana pension ya Kila mwezi hawapishani sana na walioko ofisini sababu monthly pension ni kama 75 percent ya mshahara walikuwa wanapata

Ukiweka asilimia 50 maana yake unataka monthly pension Yako iwe nusu ya mshahara uliokuwa Ukipata kazini haiko vizuri Kwa mstaafu

Binafsi ningepekeza wastaafu walipwe asilimia kumi tu mkupuo ili monthly pension Yao iwe asilimia 90 ya mshahara waliokuwa wakipata kazini

Lakini mtoto akililia wembe mpe ndicho serikalli imefanya
🤔🤔🤔🤔🤔🤔
 
Ukipewa chote pension ya Kila Mwezi hamna huko nyuma Mtu alikuwa akistaafu anapewa chake chote ilikuwa aibu unakuta Mtu alikuwa mkuu wa idara,taasisi au Jeshi au katibu mkuu analia Lia kuwa ohh sisi tumetumikia nchi lakini ona tulivyochoka anamaliza pension yake ya mkupuo anaanza kusumbua ndugu na watoto kuwa ohh hawanijali anasumbua ndio ikaamuliwa hapana Mtu awe na chake monthly pension Cha kumsaidia asisumbue ndugu au serikali na toka hapo imesaidia.

Kikongwe kastaafu atafanya nini kazeeka kachoka mwili Hadi akili ubunifu sifuri ataishia kutapeliwa tu na kufungua vibiashara uchwara ambavyo faida haitafika Hata asilimia 10 ya mshahara alikuwa akilipwa kazini
Kwahiyo Wanasiasa wao ndiyo wanauwezo wa Kutunza pesa Yao ya Pension? Halafu watumishi ndiyo Mambumbu sanaa hayawezi eti?
 
Anataka ajilipe humo humo,haya maisha ndo siku hizi tunayashuhudia
kijana anaajiriwa leo,kichwani anawaza wizi tuu ili akistaafu asifanane na baba yake aliyejaza makabati kwa
hati za uadilifu akaishia kuchekwa na wadanganyika kwamba hakujipanga alipokuwa kazini.
Aahaaaaa

Eti za uadilifu
 
1. Swali la kupata ngapi sio universal. Inategemeana na number of factors

2. Baadhi ya factors zinazo determine lump sum payment (40%) na pension ya kila mwezi ya mstaafu yeyote ni:

(a) Mstaafu ni member wa mfuko upi.

(b) Muda aliofanya kazi kabla ya kustaafu. Miaka michache basi, matokeo yake ni kiinua mgongo na pension kidogo; na miaka mingi kazini, kiinua mgongo na pension kubwa pia

(c)Kiwango cha mshahara ulichokuwa unapata kabla ya kustaafu: Mshahara mkubwa, basi inakupa kiinua mgongo na pension kubwa na mshahara kiduchu, tegemea pia kupata kiinua mgongo na pension kidogo

Mathalani mtu mwenye mshahara wa 1,500,000 mpaka wakati anastaafu, hawezi kuwa na kiinua mgongo na pension sawa na mtu aliyestaafu na mshahara wa 3,000,000 na wote wakiwa wametumika miaka 35 labda!!
Hilo liko wazi Kila mtu anajua na ndiyo maana hakuna mtu anasema mtu wa Mshahara wa 700,000/- mfano afanane na wa 1,500,000/ au 2,000,000/-Kinachotakiwa Hesabu ya Kikokotoo irekebishwe na Kila mtu apate haki yake na Wala siyo kufanana malipo
 
Bado hiyo si sababu ya mtu(mstaafu)kutokudai fedha zake halali.Hakuna kinachohalalisha lolote bila mwenye fedha zake kuridhia.Hata slay-queens wakipita nazo hilo siyo shauri la mtu.Wangapi kwani wametapeliwa hadi ihalalishwe kwa wote?Huo ni utapeli wa lugha lainilaini.
Mimi nashangaa sana, mtumishi aliweza ku manage Mshahara ila kumanage pension hawezi? Haya si matusi haya?
 
Ndio shida ya kutokuwa na taarifa sahihi halafu mtu anafanya maamuzi Kwa taarifa zisizo sahihi
Pension ya mwezi mtu analipwa maisha yake yote Hadi anafariki hata Aishi miaka 1000 ataendelea kulipwa ni yeye tu kuendelea kuishi
Hivi ni kwa nini tunahangaika na watu waliopo kwenye mfumo rasmi wa ajira ambao ni asilimia ndogo sana ya watanzania?
kama pension fund ndo mpango mzima wa maisha ya uzeeni,ni kwa nini hatufanyi jitihada ya kuwaelimisha wakulima na wafanya biashara nao wajiunge na mifuko hiyo ili nao wafaidi uzeeni?
Mambo kama haya ya kushughulika na wenye cash in hands ndo yanatufanya tuamini tunafanyiwa utapeli mchana kweupe.
 
Hilo liko wazi Kila mtu anajua na ndiyo maana hakuna mtu anasema mtu wa Mshahara wa 700,000/- mfano afanane na wa 1,500,000/ au 2,000,000/-Kinachotakiwa Hesabu ya Kikokotoo irekebishwe na Kila mtu apate haki yake na Wala siyo kufanana malipo
Liko wazi kwako

Niliyemkwoti aliuliza swali kutaka kuelewa

So, this is for him/her not for you
 
Akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali Bungeni, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imesikia kilio cha Wastaafu na hivyo imepandisha Malipo ya Mkupuo kutoka 33% hadi 40%

Pia, Dkt. Mwigulu amesema Rais Samia ameagiza kuongezwa kwa malipo hayo kwa Wastaafu waliokuwa wakilipwa 25% sasa watalipwa 35% katika Mwaka huu wa Fedha


====

Pia soma: LIVE - Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, leo Juni 13, 2024 Bungeni, Dodoma
Siyo takwa la wastaafu. Ni sawa na kumkata vidole vitano akasema uonevu ukaanza kumkata vinne na kujigamba, umeingiwa na huruma na kuachana na ukatili.
 
Back
Top Bottom