1. Swali la kupata ngapi sio universal. Inategemeana na number of factors
2. Baadhi ya factors zinazo determine lump sum payment (40%) na pension ya kila mwezi ya mstaafu yeyote ni:
(a) Mstaafu ni member wa mfuko upi.
(b) Muda aliofanya kazi kabla ya kustaafu. Miaka michache basi, matokeo yake ni kiinua mgongo na pension kidogo; na miaka mingi kazini, kiinua mgongo na pension kubwa pia
(c)Kiwango cha mshahara ulichokuwa unapata kabla ya kustaafu: Mshahara mkubwa, basi inakupa kiinua mgongo na pension kubwa na mshahara kiduchu, tegemea pia kupata kiinua mgongo na pension kidogo
Mathalani mtu mwenye mshahara wa 1,500,000 mpaka wakati anastaafu, hawezi kuwa na kiinua mgongo na pension sawa na mtu aliyestaafu na mshahara wa 3,000,000 na wote wakiwa wametumika miaka 35 labda!!