Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Kwa mashabiki, wanachama, na wadau wote wa michezo kwa ujumla! Habari ndiyo hiyo.
TFF na FIFA kwa pamoja wameifuta ile marufuku yao ya kuizuia klabu ya Yanga kufanya usajili.
Na hii ni baada ya mchezaji Lazarus Kambole kumalizana kwa amani na Wanajangwani.
Rai yangu kwa Yanga;
1. Timu ya wanasheria wa klabu iweke mazingira mazuri ya mikataba na wachezaji/makocha wanao ajiriwa na klabu, ili kuzuia migogoro na matukio kama haya kuendelea kujirudia mara kwa mara. Maana inaiharibia klabu ile taswira yake nzuri iliyojijengea ndani ya hii miaka michache iliyopita.
2. Uongozi/kamati ya usajili/ benchi la ufundi, nk. Wajiridhishe ipasavyo kabla ya kuwasajili wachezaji kama Lazarus Kambole, Gael Bigirimana, nk. Ili kuondokana na hasara zinazoweza kuzuilika.