Hatimaye leo nimefanikiwa kuchana vyeti vyangu

Hatimaye leo nimefanikiwa kuchana vyeti vyangu

Mimi siwezi vichoma Moto abadani...sawa havipi hela..but kuvipata hela nyingi ya wazazi na serekali ilitumika..

Pia na Mimi nikiweka effort kuubwa..So vikae tu...Kwani Kuna shida gani vikikaa kabatini vikapata vumbi..
Huyu anataka aponze vijana wengine humu wasiojielewa na wenye hasira na kutoajiriwa.
 
Acha wivu na English figure yangu mkuu😛! Kwakweli mimi kwa sahivi ajira yangu ndiyo dili langu aisee huko ndiyo itapatikana startup capital ya madili mengine.

Ila kuhusu dili nilifikiria hivi, unaweza ukawa umejiajiri ukapata tenda ya maana ila sasa wanataka atleast kufahamu your level of education! Hapo si vyeti vitatumika sasa mkuu. ?
Vyeti ni myeyusho. Mimi nilidrop university baada ya kupata wazo la kufanya kutoka kwenye masomo niliyosoma huko. Sasa hivi najiandaa kuajiri watu wenye degree pamoja na masters zao halafu mimi ambae sina hata cheti cha degree nakuwa boss wao.
 
Tuonyeshe picha,ila mwenyewe mwisho kutumia vyeti vyangu itakuwa 2025.ila Mimi sitovichana nitaviweka kama ukumbusho.
Ukumbusho ni ule ambao wajukuu watasema "kumbe babu zilikuwa zinachaji". Vikiwa na matokeo mabovu afadhali kuvichoma/kuvichana, ili wajukuu wakikuuliza uwambie viliibiwa/vilipotea. Mimi vyangu ninavyo vyote na navitumia kama inspiration kwa wajukuu wangu. ninawakoga sana na kile cha "permanent head damage", wanasumbua kuniomba tiba wakati utaalamu huo sina. Mwishowe wanaishia kunibeza eti daktari gani huwezi kutibu au daktari feki!
 
Mimi siwezi vichoma Moto abadani...sawa havipi hela..but kuvipata hela nyingi ya wazazi na serekali ilitumika..

Pia na Mimi nikiweka effort kuubwa..So vikae tu...Kwani Kuna shida gani vikikaa kabatini vikapata vumbi..
Kikubwa shule imenipa mwanga na network lakini sina mpango na kutumia vyeti vinanifanya mtumwa
 
ni jambo ambalo nimekuwa nalifikiria mara nyingi kuchana hivi vyeti maana vinanitia hasira sana hakuna vilichosaidia kwa miaka minne leo nimechana rasmi kuanzaia olevel mpaka chuo tukutane mtaani guys
Bangi, na ndio maana havikusaidii kwa hiyo ni uthibitisho wa mibange.

Unachana karatasi wakati ulichokisoma kipo kichwani. Haujui cheti ni sawa na ticketi ya basi inathibitisha tu kuwa umelipa lakini kinachokusafirisha ni pesa yako sio ticketi. Sawa na cheti ni uthibitisho tu kuwa umesoma chuo na kozi fulani lakini usitegemee cheti kitaajiriwa au kujiajiri kikuingizie pesa. Ndio maana kuna interview kuchuja vilaza kama wewe sawa na kwenye basi konda kukagua ticketi kubaini wazamiaji.

Chana au kata kichwa chako basi tukuone mjanja.

Achana na bangi za kuvutia kwenye mafuriko.
 
Aisee sawa kama unahisi ni uamuzi wa busara kwa sasa! Ila usije siku ukavikumbuka baada ya kutokea mchongo wa maana na vyeti ulishavichana. Kwani huwezi kuingia mtaani huku ukiwa umefungia kabatini hivo vyeti???
Mamii nilikukataza kuongea na watu wajinga..
 
Vyeti ni myeyusho.Mimi nilidrop university baada ya kupata wazo la kufanya kutoka kwenye masomo niliyosoma huko.Sasa hivi najiandaa kuajiri watu wenye degree pamoja na masters zao halafu mimi ambae sina hata cheti cha degree nakua boss wao.
Wow hongera mkuu! Uko vizuri naomba kwenye hizo nafasi unikumbuke pia Boss(am serious)😉
 
Bangi, na ndio maana havikusaidii kwa hiyo ni uthibitisho wa mibange.

Unachana karatasi wakati ulichokisoma kipo kichwani. Haujui cheti ni sawa na ticketi ya basi inathibitisha tu kuwa umelipa lakini kinachokusafirisha ni pesa yako sio ticketi. Sawa na cheti ni uthibitisho tu kuwa umesoma chuo na kozi fulani lakini usitegemee cheti kitaajiriwa au kujiajiri kikuingizie pesa. Ndio maana kuna interview kuchuja vilaza kama wewe sawa na kwenye basi konda kukagua ticketi kubaini wazamiaji.

Chana au kata kichwa chako basi tukuone mjanja.

Achana na bangi za kuvutia kwenye mafuriko.
bangi sivuti mkuu
 
ni jambo ambalo nimekuwa nalifikiria mara nyingi kuchana hivi vyeti maana vinanitia hasira sana hakuna vilichosaidia kwa miaka minne leo nimechana rasmi kuanzaia olevel mpaka chuo tukutane mtaani guys
Watu wenye ujasiri na maamuzi magumu kama wewe mpo wachache sana kwenye hili taifa. Naimani mngekuwa wengi basi hii nchi isingekuwa hapa tulipo
 
Back
Top Bottom