Hatimaye leo nimefanikiwa kuchana vyeti vyangu

Hatimaye leo nimefanikiwa kuchana vyeti vyangu

ni jambo ambalo nimekuwa nalifikiria mara nyingi kuchana hivi vyeti maana vinanitia hasira sana hakuna vilichosaidia kwa miaka minne leo nimechana rasmi kuanzaia olevel mpaka chuo tukutane mtaani guys
Nimetuma dogo mafuta ya taa kwa mangi. Haiwezekani uwe peke yako.
 
ni jambo ambalo nimekuwa nalifikiria mara nyingi kuchana hivi vyeti maana vinanitia hasira sana hakuna vilichosaidia kwa miaka minne leo nimechana rasmi kuanzaia olevel mpaka chuo tukutane mtaani guys
Milembe inakuhusu
 
Aisee sawa kama unahisi ni uamuzi wa busara kwa sasa! Ila usije siku ukavikumbuka baada ya kutokea mchongo wa maana na vyeti ulishavichana. Kwani huwezi kuingia mtaani huku ukiwa umefungia kabatini hivo vyeti???
Usimuamini atakuwa amechana photo copies ya vyeti, OG vipo.
 
Mleta mada bila shaka ulikuwa msindikizaji
Na wachangia mada wengi bila shaka walikuwa wasindikizaji
Ngoja niondoke mada hainihusu [emoji124]
 
ni jambo ambalo nimekuwa nalifikiria mara nyingi kuchana hivi vyeti maana vinanitia hasira sana hakuna vilichosaidia kwa miaka minne leo nimechana rasmi kuanzaia olevel mpaka chuo tukutane mtaani guys
Nielekeze na mimi.
 
Mimi nilivirudisha chuo vyeti vyangu nirudishiwe ada hata nusu
Kufumba na kufumbua nikajikuta ndani ya ambulance nimefungwa kamba mikononi na miguuni naelekea dodoma kutibiwa afya ya akili
 
Mleta mada bila shaka ulikuwa msindikizaji
Na wachangia mada wengi bila shaka ni wale waliokuwa wasindikizaji pia
Ngoja niondoke mada hainihusu [emoji124]
Unfortunately nipo vizuri upstairs
 
Dooh hata sasa bado it's your plan B mkuu! maana ukiamua kuvipata tena inawezekana Necta na chuo wanakuprintia tena mbona. Sijui mi naona kama ungekua hutaki kuvitumia ungevihifadhi mahali!siku utapata deal hata huko mtaani litaloweza hitaji hivo vyeti ukasumbuka[emoji2369]. Kila rakheri
Nikipata mke kama wewe.. Nitafanikiwa maishani
 
unfortunately nipo vizuri upstairs
Ndio upo vizuri upstairs sikatai ila ulisomea fani usiyoipenda, so direct wewe ulikuwa msindikizaji tu
By the way ulishawai kukiri kwamba hukupenda kusoma ulichokisomea ndo maana hata performance yako ipo low
 
Karibu mkuu kilimo cha jembe kinalipa sana ukiwa na commitment. Utakua empty pocket ila sio empty stomach.
Karibu kitaani mate, connection za saidia fundi zipo kibao
Thanks mkuu
 
Ndio upo vizuri upstairs sikatai ila ulisomea fani usiyoipenda, so direct wewe ulikuwa msindikizaji tu
By the way ulishawai kukiri mwenyewe kwamba hukupenda kusoma ulichokisomea ndo maana hata performance yako ipo low
Yeah sure mkuu
 
Nimesoma habari yako nikasikitika sana wewe sio wa kwanza na wala hautakuwa wa mwisho.
Vijana wengi wamechoma vyeti vyao kutokana na khari wanayokutana nayo mtaani haendani na uhalisia wa maisha au kazi wanazozifanya..ni sawa na dada wa Dodoma ana Masters anaendasha Bajaji huo ni ujinga na sio sifa kama Taifa yule vyeti kwake vya nini..ni upuuzi mtupu..
Kuna haja ya serikali kuangalia namna mpya ya kuwasaidia vijana pindi wamalizapo vyuo na sio kuwambia ujasiliamali unalipa kwa kuongeza vibanda vya umachinga na kuziba barabara.
 
ni jambo ambalo nimekuwa nalifikiria mara nyingi kuchana hivi vyeti maana vinanitia hasira sana hakuna vilichosaidia kwa miaka minne leo nimechana rasmi kuanzaia olevel mpaka chuo tukutane mtaani guys
Ngoja Magu aanze kugawa ajira kwa hasira mara tu atakaposikia hili.

Utaleta uzi mpya ukisema "wakuu nawezaje kurecover vyeti nilivyo chana na sijui vilipo?"

Mi ntakuambia nenda kaanze elimu ya msingi.
 
Back
Top Bottom