Hatimaye leo nimejiridhisha tatizo la Simba ni Viongozi

Mimi naunga mkono yale maneno ya Ali Kamwe ya kutaka hao viongozi wapelekwe Jangwani kwa bakora ili wakajifunze namna bora ya kuongoza klabu yao.
 
Sio waende hapo karibu Jangwani ili wasitumie gharama kubwa. TP Mazembe wameonesha njia wengine wafuate. Mfichaficha maradhi kifo humfichua.
Wamezoa kuahirisha kufikiri, (suspending individual reasoning), siku hizi mnasema kujizima data, zamani tulisema kujitoa ufahamu
 
Naunga mkono hoja shida ya Simba ni viongozi. Ukiona kwenye kwenye taasisi yoyote iwe kwenye siasa, makazini, kanisani, msikitini na sasa kwenye mpira kiongozi anategemea chawa ili aendelee kuongoza badala ya kutimiza anayotakiwa kutimiza basi jua hapo hamna kiongozi na ataondoka kwa aibu kubwa.. Ukitegemea chawa ili uendelee kuongoza uongozi wako ni wa muda mfupi tu lakini ukitimiza yanayohitjika kutimizwa katu kiongozi wala hatumii nguvu nyingi kukubalika na ataoongoza hiyo taasisi kwa muda mrefu na hata ikifika wakati wa kuondoka ataaondoka kwa heshima kubwa.
 
Chawa eti ndiye wa kukuvunjia barafu, (breaking the ice) ,kukufungulia njia ama kukusafishia njia duu hapo kazima ufeli
 
Game ya kmc na Singida ilikuwa nzuri kuliko kile kikao chao na sauti ilikuwa kama wanaongelea kwenye ndoo
Halafu watu wajifunze kuandika points za kuongea sio unaongea Kila linalokuja kichwani ili uitwe genius
 
Wote pale ni njaa tupu ndio maana hatuendi mahali, almost wote hawana kazi za kueleweka ndio maana wanaendekeza njaa zao na kufanya usajili wa hovyo na kula fedha !
 
Sasa mtu kama try again ukimuangalia tu machon unajua kichwan kuna jambo
 
unadhani bila utetezi huo wangesema nini?
 
Mechi za kimataifa kufungwa nje ndani na alahly kutoshinda game hata moja hatua ya makundi ni figisu za board ya ligi wasilete sababu zisizokuwa na mashiko wala maaana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…