Hatimaye Libya yawa shamba la Bibi, officially

Ndio madhara ya kuongozwa na dikteta! Akiondoka anaacha chuki na visasi mpaka nchi haikaliki.
Tatizo sio viongozi madikteta bali ni kuwa na wapinzani uchwara. Mawakala wa mabeberu. Kila jambo wao ni kama watoto wanaodeka. Lazima wakimbilie kwa mabwana zao kujiliza
 
Huyu jamaa namchukia
 
Gbabo yupo jela!?
Jela ya wapi?
 
Kwao wanamwaga mboga? Hakuna faida ,bora kuwa walivyokuwa mwanzo. Nawalaumu wazungu tu, halafu nalaumu uwezo wa kupambanua mambo tulionao waafrika kusoma ulaya wala kujuana na mzungu si tija, tuwasikilise lkn tuamue kivyetu
 
Muslim Brotherhood hawajawahi kuwa kundi salama. Nchi yoyote ikiwazuia naiunga mkono. Na hao extremists kuuwawa ndo lilikuwa suruhisho, kama hutaki kwani huwaoni kina Khalifa Haftar?
Walilalamika kuwa Gaddafi amekaa sana madarakani, wakamuua. Leo hii kuna serikali ya GNA bado wanapigana nayo. Sasa watu kama hawa unaniambia nisiwaue? Hata mimi nikiwa rais kuna wapuuzi wanatakiwa kutangulia. Hata hizo nchi zako za Democracy zinafanya hivyo sema mahaba tu yanawasumbua. Nikuulize, kwanini US walimuua Martin Luther Jr.?
 
Ni Kweli lakini mtu kama yeye hakutegemea kukamatwa kama panya kwenye mtaro na vijana aliowaita panya na mende hapo mwanzoni wakati maandamano yameanza!
Sasa kwani si wanaishi kama panya kwa sasa. Unadhani alikosea kuwaita hivyo? Panya ndiye mnyama anayekimbia kwenye usafi akaingia kwenye takataka na mabaki. Mende anaishi kwenye uchafu, ukimpa usafi anateseka. Nao waliteseka sana na maisha yao safi, wakaamua wamechoka kuishi kwenye maghorofa na huduma bora za kijamii. Wakaamua kulipua majengo yote ili waishi kwenye magofu na ukosefu wa huduma za afya. Wakaona kuongozwa na mtu mmoja sio sawa, wakamuondoa na kuweka serikali maandazi ambazo hazina complete control. Wala hawakuona jeshi lao linafaa, wakaunda vikundi kibao na sasa bado wanapigana na hawajui wanataka nini. Hao si ni kama panya tu.
 
Hivi kuwepo madarakan kwa kiongozi lakini maisha ni safi hiyo si ndio democracy au democracy ni kuachiana vipindi vya uongozi lakini mazingira kama wanayo ishi Libya ya sasa
 
Off course gaddafi alikua anafaidi sana na ndio maana hakutaka kuachia madaraka mpaka alipofurushwa kwa nguvu na wananchi wake.
Sasa hata wangefanikiwa kumtoa Gadaffi pasina machafuko unadhani kipi cha ajabu ningekuwepo? vitu vyengine havina maana sidhani kama waliona ni bora kupitia wanachopiti sasa kuliko kutawaliwa na mtu mmoja?
 
Wewe unaona Hilo pekee, je hao wenye uchu na madaraka Wao sio sababu?

Kwani Gadafi ndio Raisi wa Kwanza huko Libya
 
Libya ilishawahi kuwa NAMBA MOJA DUNIANI KIUCHUMI SABABU YA MUHAMMAR GADDAFI.
Ila ndo hivyo tena walishikiwa masikio na wamagharibi na wamashariki wakamuona BABU YAO HAFAI
 
Shida sio KUNG'ANG'ANIA MADARAKA.
mbona uingereza hyo demokrasia hamna?.
Uingereza wanaongozwa na malikia.
Kwanini wamarekani na wazungu waone kuwa gaddafi hafai?
 
Mimi naelewa sana labda useme hutaki kunielewa ama unajitia hunielewi

Siungi mkoni marais wanaokaa milele ama muda madarakani nawala siwapingi

Sababu nnavyoamini mimi kilataifa kinauhuru wakuyaamua mambo yao wenyewe kwamifumi nasera wanazozihisi zinafaa

Nandio maana leo hii kupitia demokrasia wazungu wanaona ndoa zajinsia moja nihalali ila nyie waafrika wengi bado munaona hazifai

Jengine hapa nilikua nataka niwaoneshe unafiq wahao mnaowatetea kumuuwa gadafi kwakisingizio chakulinda ama kupeleka demokrasia ndio hao hao wanaotumia nguvu kubwa sana kuyalinda mataifa mnayoyaita yakidikteita yote yaliopo mashariki yakati kuanzia SAUDIA mpaka QATAR nakwengineko (sasa hawa wanataka demokrasia ama wanalinda maslahi yao kwanguvu zozote ikibidi kuuwawa watu wao hawajali!?)

Mfano MISRI ya Muhammed Mursi waliunga mkono mapinduzi ya Alsisi wakati tunajua serikali ilipo madarakani ilikua wanayoitaka wao yakidemokrasia ila akaja sisi ni dikteita
IRAN aliondolewa shah aliokua dikteita akaja alokuja wakamletea figisu
VENEZUELA pia jamaa wanaendabkidemokrasia zengwe haliishi


Pia kama wanahisi mfumo wakupokezana mamlaka ndio mfumo sahihi wangemshinikiza na MALKIA wa UK natawala zote zakifalme ama zinazopokezana madaraka ULIMWENGUNI kwamba waziwe namifumo yakiimla


Endeleeni kuwatetea hao wanaojiona MIUNGU watu kama hawatakaa wafe vile...
 
wakujifunza ni viongozi wa africa, huwezi kukaa madarakan muda mrefu eti kwa sababu unawapa kila kitu.
Mngepaza hzi sauti nakwayule BIBI wa UK mungekua munaeleweka sana ila mmekalia UNAFIQ tu[emoji12][emoji14][emoji12]
 
Hivi hapo wa kulaumiwa ni nani? ni Gadafi kung'ang'ania madaraka au hao waliyokinukisha kwa wao nao pia kutaka madaraka?
wote hawakusoma alama za nyakati na kutokufikirisha bongo zao juu ya madhara wanachokifanya.

1;GADAF alipaswa angejitoa mapema kabisa baada ya kuona kelele zinaanza kuliko kuanza kushindana na kelele

2:Raia nao hawakufikiria kwa kina kwa hiki tunachoenda kukifanya na kutambua madhara yake hapo abadae
 
1)Maji bure 2)Umeme bure 3) Bei ya Mafuta ilikuwa sawa na tshs 200 kwa litre 4)Hamna kodi ya nyumba 5)Elimu bure hadi chuo kikuu na kwa wale waliopendelea kusoma nje pia walilipiwa na serikali 6) Serikali ya Libya ilitoa takribani $ 60,000 karibu milioni 150 kwa kila wanandoa wapya ikiwa ni pesa ya kuanzia maisha.
7) Mwanamke aliyejifungua alipewa dola 5,000
8) Pia endapo mlibya atapata tatizo la kiafya ambalo haliwezi tibika nchini kwake alilipiwa gharama zote za matibabu nje ya nchi na Serikali.
9) Libya ndo nchi iliyokuwa na reserve Kubwa barani Afrika na haikuwa na deni la hata senti. Reserve ya Libya ilikuwa Dola Bilioni 150. N.K.




HAYA YOTE NI BURE KAMA HAKUNA UHURU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…