Hatimaye Mahasimu wa Muda Mrefu Jay Z na Nas wamekutana tena kwenye Album ya Dj Khaleed

Hatimaye Mahasimu wa Muda Mrefu Jay Z na Nas wamekutana tena kwenye Album ya Dj Khaleed

anonymousafrica

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2016
Posts
611
Reaction score
640
Wimbo unaitwa SORRY NOT SORRY. Mpaka sasa nimeskiliza kipande cha Nas tu, navuta pumzi nimsikilize Jay. Licha ya bifu lao au mgongano kuisha toka miaka ya 2006 lakini hadi leo hii, wapenzi wa utamaduni na muziki wa Hip Hop hawaishi kuongelea msuguano huu uliotokea kwenye Album ya Nas (stillmatic) mwaka 2001 kwa kibao chake cha ETHER- naweza kusema ESTHER ni kati ya Diss Track 3 bora kuwahi kutokea duniani.

Nas-Stillmatic-Backcover.jpg

Nas alimchana baada ya Jay kumshambulia Nas vibaya sana kwenye wimbo wake wa TAKEOVER alioutoa mwaka huo huo 2001 kwenye album yake ya THE BLUEPRINT akimsema Nas kwa flow mbaya na kudanganya kwenye nyimbo zake kuwa anayoyaimba hajayaishi-ameyaona kupitia vitabu na vyanzo vingine.

Jay pia alikuwa akijipima ubora na wasanii wote wa kizazi cha 90's kama Mobdeep- ndomana Nas kwenye Esther anamwambia Jay- inamaana wewe unataka kujifananisha na Biggie, Gayz, Cock-A-Fella Records na maneno mengi machafu na hii kuifanya Esther kuwa Wimbo mkali wa miaka yote

nas-jay-z.jpg
wenye kudiss
Walisample watu kibao na kuifanya nyimbo ya kuwachana wengine Beat hili aliwahi kulitumia Eminem kumchana Jumanne Dupri (Jermaine) na hata hapa karibuni aliwahi kulitumia Remmy Ma kumdiss Nick Minaj na yeye aliita Shether.

Licha ya bifu hii kuwanufaisha wote wawili Jay Z alimwomba msamaha Nas na familia yake baada ya bifu kufika mbali na kujibizana maneno machafu kwenye nyimbo zao, mfano kwenye U Don't Know"Jay alisema (nimelala na mama yako Nas ukiwa mdogo).

sqwgtcclwcmcsuwhdupj.9.jpg

Mwaka 2006 Nas alimshirikisha Jay kwenye wimbo wake wa Black Republican ulioachiwa kwenye album ya Hip hop is Dead. Mwaka 2007 Jay z naye akatoa album yake ya American Gangster na kumshirikisha Nas kwenye kibao cha I Do It For Hip Hop Wakaendelea kupeana shavu.

Japo watu hawajaacha kulizungumzia bifu la Ether, na wamekuwa wakilinganishwa muda wote licha ya wao kuyamaliza. Na sasa tunamwona Dj Khaled akiwakaribisha wawili hao kwenye Album yake ya KHALED KHALED.

Screen-Shot-2021-04-29-at-9.19.03-AM-713x400.png
 
DJ Khaled ni wale wanafunzi chuoni hawafanyi Group Assignments ila wao huomba kuwekwa JINA tu![emoji16][emoji16][emoji16]

Au wale hata hawahusiki kuandaa PRESENTATION, just put their NAMES on the list.[emoji2957]

ANOTHER ONE [emoji1487][emoji276]
 
Siyo kweli Mkuu.

Ungesema ni wale wanafunzi ambao kazi yao ni kukusanya points kutoka kwa wenzao, kuorganize points za nani zikae juu, kuzitype na kuandaa kava.

Na wanahakikisha jina lao linakuwa juu.
 
DJ Khaled ni wale wanafunzi chuoni hawafanyi Group Assignments ila wao huomba kuwekwa JINA tu![emoji16][emoji16][emoji16]

Au wale hata hawahusiki kuandaa PRESENTATION, just put their NAMES on the list.[emoji2957]

ANOTHER ONE [emoji1487][emoji276]

Nyimbo yake anashirikisha msanii mkalii halaf ye utasikia tu another one [emoji23][emoji23][emoji23] ila nyimbo zake nzurii sana
 
DJ Khaled ni wale wanafunzi chuoni hawafanyi Group Assignments ila wao huomba kuwekwa JINA tu![emoji16][emoji16][emoji16]

Au wale hata hawahusiki kuandaa PRESENTATION, just put their NAMES on the list.[emoji2957]

ANOTHER ONE [emoji1487][emoji276]

DJ Khaled ni producer..beat maker na arrangements ya hizo nyimbo zote anafanya yeye...

Baada ya ma producers wengi kuona hawapati hela inayolingana na jasho Lao ndo
Walianza hii ya kumiliki wimbo Kwa kuwashirikisha wasanii ambao wameshawafanyia production..

Timbaland kafanya Sana na wengine..

So usione haimbi chochote ..
Ni production yake...
 
Dj qyalid

Another one
 
Umenielewesha jambo nililokuwa silifahamu.
 
DJ Khaled ni wale wanafunzi chuoni hawafanyi Group Assignments ila wao huomba kuwekwa JINA tu![emoji16][emoji16][emoji16]

Au wale hata hawahusiki kuandaa PRESENTATION, just put their NAMES on the list.[emoji2957]

ANOTHER ONE [emoji1487][emoji276]
I'm number one in this b!tch and I'ma stay there!! We the best of the best.
 
Nas ana jealous tu. Jizzo ni tawi jingine yule. Gheto boy, kama unataka kumwelewa Jizzo sikiliza inteview zake. Very humble. I don't understand why people hate him! Even Queen B mwenyewe ageuzi. Unajua kwasababu gani? Jamaa ni genius kinoma, we sikiliza rylics zake. Kwahiyo Nas hawezi kugeuza kwa J. Na huo ndio ukweli na kila mtu anajua
 
DJ Khaled ni wale wanafunzi chuoni hawafanyi Group Assignments ila wao huomba kuwekwa JINA tu![emoji16][emoji16][emoji16]

Au wale hata hawahusiki kuandaa PRESENTATION, just put their NAMES on the list.[emoji2957]

ANOTHER ONE [emoji1487][emoji276]
Hahahahaha yaani mule mule .

Jamaa kazi yake Ni kuweka jina tu[emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom