Wanajamii tujifunze kuandika ukweli,baadhi ya maneno yetu humu yananukuliwa na magazeti na kusambaza habari zisizo za kweli.Habari hizo hazijengi bali zinabomoa.Mindi hana mahusiano yoyote na Rahma Kharoos.Huyu dada ni mfanyakazi wa serikali toka mwaka 2006 alipomaliza shule yake kule Minneapolis/St.Paul,Minnesota.Kwa kipindi tofauti amesoma Warldof ,Iowa na baadaye Milwaukee,Wisconsin alipokutana na Mumewe Alex Tarimo.Mindi Kasiga ambaye amezaliwa mwanzoni mwa miaka ya 1980 ana Dada zake wawili,Kalunde (Kay) na Emma ambao wanaishi katika Jiji la Minneapolis.Mara baada ya kumaliza shule yake Mindi Kasiga aliajiriwa Ikulu - Dar-Es-Salaam katika Idara ya mawasiliano akifanya kazi na Asha Mtwangi,baada ya Mkataba wao kuisha alifanyakazi ktk Ofisi za UN,Dar kabla ya kuingia Foreign Affairs.Katika Mikutano ya Dicota September/2011(Washington -DC), Mindi alikuja akiambatana na Ujumbe kutoka Foreign Affairs.Kupangiwa kazi Ubalozi wetu DC ni maombi maalumu ya Mama Balozi,baada ya kuona kuwa Kasiga ana ufahamu na mambo ya USA kutokana na kuishi na kusoma huko.Tumpe ushirikiano,ni kijana mdogo lakini mwepesi kujifunza.Ni kweli Mama mzazi wa Mindi ni Dada yake Mama Mkapa,Kama ilivyo kwa Balozi Sefue na Balozi Mstaafu Ben Moses.Baba yake mzazi Mindi ambaye ni Marehemu ni mzaliwa wa Tabora,na kipindi cha nyuma alikuwa Daktari katika makambi ya Wapigania uhuru.Mindi ameolewa na ana mtoto mmoja.