The dataz ni kwamba......
1. Ubalozi wetu DC umekuwa ukijaribu kujiingiza kwenye msiba lakini mpaka jana ulikuwa bado haujakubaliwa na mjane wa marehemu, labda kama leo atawakubalia wawepo huko kwenye mazishi, lakini uwezekano ni nill.
2. More dataz ni kwamba mjane is very bitter pia na gazeti la TZ Daima, kwa kitendo chake cha kukimbilia kuzitoa habari hizi, wakati zilitakiwa zibaki ndani ya familia.
3. Ndugu wa marehemu walianza kuwasili DC toka Jummane, hadi leo wameendelea kuwaisli huko kwa ajili ya mazishi na msiba.
4. Mkuu Mtanzania, kwa ulelewa wangu mdogo, Grreen Card ni lazima iwe validated kila mwaka kwa kuingia ndani ya US at least once a year, ukishindwa kufanya hivyo automatically inaisha kazi, na hayo yamempata mshikaji wangu mmoja aliyerudi kugombea ubunge hapa bongo, na kushindwa kurudi kule US on time na sasa hawezi kwenda tena. Lakini kunaweza kuwa na ukweli zaidi ya huu!
5. Now ninaomba nirudie kuwa kwangu binafsi, huu mjadala ni mijadala yote mingine huwa ninaichukulia very serious, kwa sababu ninaamini kuna wananchi wengi sana wanaokuja hapa kupata habari muhimu kwa taifa lao, hapa tunashirikiana kuhabarishana na kuelimishana, na wengi wetu tulikuja hapa JF kwa sababu ya ku-create alternative ya habari muhimu za taifa letu, hasa baada ya mtandao kununua media zote za bongo,
Sasa kama una habari muhimu kuhusiana na hii topic, tafadhali ziweke hapa ili tuelimishane na tuhabarishane, ninawaomba baadhi ya ndugu zangu muelewe kuwa taifa zima liko hapa kujaribu kupata habari, ukiangalia wiki hii nzima habari za magazeti kuhusu hii ishu ya marehemu, 90% zinakuwa zimetoka hapa JF, kama kuna habari yoyote hapa unaona ina makosa basi irekebishe kwa kuweka marekebisho, binafsi ninapata feedback nzito sana za kutoka kwa wananchi wengi sana kuhusiana na habari zetu hapa,
Ninawaahidi wananchi na taifa zima kuwa tunajaribu kila njia kutafuta habari za ukweli na kuziweka hapa, inapotokea kuwa zina kasoro inakuwa ni kasoro za kibin-adam ambazo haziwezi kuzuilika, lakini sio kwamba tunajaribu kwa makusudi kuwa-mislead, ninawaomba sana ndugu zangu kuwa tujaribu kuwa serious kidogo na michango yetu hapa, taifa linatuangalia, in the last two weeks nimeshuhudia the media bigs wa taifa letu wakitutafuta tuwape habari, I am humbled, lakini tutaziweka hapa tu JF.
Ahsante Wakuu!