Hatimaye Nime-Confirm Kuwa Balali Amefariki!

Status
Not open for further replies.

Usisahau picture.
 
Muungwana naye katoa rambi rambi?
Kama kamati yake haikumhoji then waliamini kuwa yeye hakuhusika..Sasa kwanini...Then wakati kafa/ama kukaribia kufa ndo wakaanza kumtafuta na kugundua kuwa keshakufa kabla ya kutuhumiwa na hivyo alikufa akiwa huru,na marehemu ni huru...Hata hivyo bado kuna utata hapo Muungwana aliotuonyesha wa either kutoamini kuwa Ballali kafa..Ama kufurahia kifo chake!
Na at the same time atayasimamia vipi magrupu hayo yaliyogawanyiaka?
Mengine yakiamini kwa soo litaisha na mengine yakiamini kuwa soo litasanuka na kutakuwa na hatari kwa utawala wao!
Kama wewe ni JK ungekuwa upande gani?
 

I SALUTE YOU................................
 
Daa!!!, hata wewe mushi tayari umeshagwaya? naoana umeshageuka do!!!!!, sijui tushike wapi, mnatuchandanya wakuu, jana ulikuwa umekaza kamba mara ulipotishwa tu, ooo!!!! chari,
 


Rev. Kishoka,

Ya Balali yanatuhusu kwasababu ni mwizi wa mali ya Watanzania wote. Kufa kwake kunatunyima wote kama Watanzania nafasi ya kujua ukweli juu ya hawa mafisadi.

Pili, je ni nani hao wangemteka Ballali? Akina RO walikuwa wanajua yuko wapi, akina Mkono wanajua, ambao tulikuwa hatujui ni sisi walalahoi ambao ndio tungetaka ajibu mashitaka kwanza.

Siamini Ballali ni mjinga kiasi hicho, kama aligoma kabisa kuongea, basi hapo kuna siri kubwa ambayo yeye mwenyewe ni mhusika mkubwa. Yeye sio victim kwenye hili na badala yake ni among the main players.
 
Kwa ukawaida kama walivyosema waungwana wengi ni kwamba kama kweli familia nayo ilikuwa na nia nzuri..

Then wangetafuta msaada wa Watazania kwa wakati huu mgumu ili kuweza kuwin back sympathy!Ni wazi kuwa ndugu zake Ballali sympathy wanayotafuta ya kuimply kuwa Ballali alikuwa hapendwi na watawala kama ambapo dili nzima ianvyotakiwa ionekane!

Hapo ndugu zake wanajitoa nishai wenyewe kwasababu hapa marekani alikuwa na uhuru wa hata kuita press conference kwasababu alikuwa keshafutwa kazi na tuhuma zilikuwa juu yake kuwa anatafutwa!

Usanii mtupu!

Kama kweli alikuwa huru,mbona alikufa ghafla wakati makachero walipofika huku?

Yani ina maana kuwa alitaka afe akiwa huru?

Kwanini afe mara baada ya uhuru wake kukaribia kwisha?

Na kwanini serikali ilikuwa ikisubiri afe ili afe na uhuru wake na habari zake?

Kwani nani hajui kuwa kwasababu alikufa akiwa huru basi hata yale aliyoyaacha haywezi kutumiwa tena kama ushaidi?

Yani kweli huu usanii...Lakini nawakumbusha wanafamilia kuwa bado wana nafasi ya kufanya kitu ili kuondoa hili wingu zito la utata linaloikabili nchi yetu kwasasa
 
Daa!!!, hata wewe mushi tayari umeshagwaya? naoana umeshageuka do!!!!!, sijui tushike wapi, mnatuchandanya wakuu, jana ulikuwa umekaza kamba mara ulipotishwa tu, ooo!!!! chari,

Mambo mazuri hayataki papara!
Nakuhakikishia kuwa bado tuko pamoja!
Tutafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa watanzania wanapewa haki yao!
Naomba tu tuombeane uzima kwasababu issue hii si ndogo!
 
Kwasababu Ballali alikufa akiwa huru..Hata ushahidi wake anaodaiwa kuuacha hauna nguvu tena kwasababu alikufa kabla hajatuhumiwa!
Ushaidi wake unaweza ukawa batili na hivyo kesi yote kufa kwasababu ni ushahidi wa marehemu asiyekuwa mtuhumiwa!?! Au ni aliyekufa kabla ya kuwa mtuhumiwa ama aliyekufa kabla ya kutumiwa!
Hivyo kwa wale wanaosema changa la moto wana HOJA NZITO!
 
Sasa ushaidi wa ballali utatumika kama ushahidi wa mtuhumiwa ama wa marehemu huru aliyekufa akiwa huru na kuzikwa huru na kwa uhuru?
 
Marehemu atatuhumiwa vipi kama alikufa akiwa huru?
Akishazikwa ndugu zangu upelelezi utaanza upya!
Unless kuwe na ushahidi kamili kuwa huyu mtu huru aliyekufa masaa machache kabla ya kuwa mtuhumiwa ni kweli amekufa!
 

Tutakacho sikia baada ya hapa ni unafiki tu,ambao haujengi.tulikuwa na nafasi ya kujua kila kitu lakini hatukuitumia.hivi kesi ya ditto kwani bado hipo ?
 
jmushi1
Vipi mara rangi 2? ama power? ok ama na wewe umethibitisha kama kaanza? mimi bado ni utata, sijui, na tangu nimezaliwa sikuwahi kusikia mtu azikwa kwa faragha, marehemu siku zote hana kosa sasa iweje asirudishwe hapa home jamani? ndugu zake wote wanaishi Iringa, mashamba yake yale ya bunju yanatosha kumuhifadhi,hii ndiyo Tz
 
Tanzania tanzania, ...............
nilalapo nakuwaza wewe.............,
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…