Hatimaye Nime-Confirm Kuwa Balali Amefariki!

Status
Not open for further replies.
Hayawi hayawi sasa yamekuwa...

Muda si mrefu funeral crasher number 2 ninaingiza timu kwenye msiba wa Balali ili kupata yaliyomo...

Mipango yote inakamilika na heshima zote zitakuwepo ikiwemo ya kuzima simu na mawasiliano ya intaneti. I have my fingers crossed here..

5
4
3

I will do it live... I will do it live.... (kwa hisani ya Bill O'reilly).

5
4
3
2
1

.........

Usisahau picture.
 
Muungwana naye katoa rambi rambi?
Kama kamati yake haikumhoji then waliamini kuwa yeye hakuhusika..Sasa kwanini...Then wakati kafa/ama kukaribia kufa ndo wakaanza kumtafuta na kugundua kuwa keshakufa kabla ya kutuhumiwa na hivyo alikufa akiwa huru,na marehemu ni huru...Hata hivyo bado kuna utata hapo Muungwana aliotuonyesha wa either kutoamini kuwa Ballali kafa..Ama kufurahia kifo chake!
Na at the same time atayasimamia vipi magrupu hayo yaliyogawanyiaka?
Mengine yakiamini kwa soo litaisha na mengine yakiamini kuwa soo litasanuka na kutakuwa na hatari kwa utawala wao!
Kama wewe ni JK ungekuwa upande gani?
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa...

Muda si mrefu funeral crasher number 2 ninaingiza timu kwenye msiba wa Balali ili kupata yaliyomo...

Mipango yote inakamilika na heshima zote zitakuwepo ikiwemo ya kuzima simu na mawasiliano ya intaneti. I have my fingers crossed here..

5
4
3

I will do it live... I will do it live.... (kwa hisani ya Bill O'reilly).

5
4
3
2
1

.........

I SALUTE YOU................................
 
Daa!!!, hata wewe mushi tayari umeshagwaya? naoana umeshageuka do!!!!!, sijui tushike wapi, mnatuchandanya wakuu, jana ulikuwa umekaza kamba mara ulipotishwa tu, ooo!!!! chari,
 
Kama ndugu wanavyogombana wakati wa misiba, wengine kudai wana haki zaidi kuamua Marehemu azikwe wapi, nani awe "mrithi" wa kutunza familia, nani agawiwe mali na majukumu mingine ambayo ni kawaida ya binadamu, Jumuiya yetu nayo iko katika mvutano huo huo.

Najiuliza je ni kawaida yetu binaadamu kuwa na mvutano kuhusiana na kifo na hasa wakati wa msiba? je hii ni ni kawaida wakati wa maombolezo?

Nimejiuliza ya fuatayo na maoni yangu binafsi na imani yangu pamoja na maswali haya ni kuwa Ballali hayupo nasi tena. I believe Daudi Ballali is dead and I pray that his sould rest in peace.

Maswali ni haya;
  • Je Ballali amekufa?
  • Ni nani ananufaika kwa kifo chake
  • Kama bado yupo hai na taarifa ya kifo ni ulaghai, ni kwa faida ya nani?
  • Je tuna haki gani kutaka kuingilia mambo ya binafsi ya familia?
  • Je kwa nini familia haitaki Ballali agwe na wananchi na kufanya msiba wake uwe jambo la familia tuu? ni wapi ule mshikamano wa kiafrika na utamaduni wetu?
  • Je ni kwa nini kumekuwa na usiri mkubwa kuhusu kuugua kwake na hata kifo chake? je mimi nina haki gani au wajibu gani kujua kuhusu Ballali? kwa nini kuna utata mkubwa katika kila kitu kuhusu Ballali?
  • Kifo chake ni pigo kwa nani?
  • Kama sababu za kifo chake ni kuuwawa kama wengi wetutunavyokisia, kudhania au kuzusha, je ni nani aliyetaka Ballali afe? Ni lini aliuawa? na ni nini kilitumika kumuua?
  • Ni siri gani ambayo amekufa nayo au kawapa familia, marafiki na wengine waitangaze?
  • Je kifo chake kina sehemu gani au mahusiano gani kuhusiana/katika uchunguzi wa tuhuma za ufujaji mali, uhujumu na ufisadi wa pesa za Taifa Benki Kuu?
  • Je kufa kwa Ballali kuna maafa gani katika vita ya ufisadi?
  • Je familia yake inaungana vipi wakati kuna mgawanyiko kati yao kuhusiana na mazingira mazima ya yeye kutuhumiwa, kuugua na sasa kufa?
  • Ni nani hao ambao wanatoa vitisho au wametoa vitisho na kutaka kila kitu kinachohusiana na Ballali kiendelee kuwa ama usiri, utata au mara nyingine kuwa ni uzushi? kwa faida gani? na ya nani?
  • Je alikufa lini na wapi?lipi ni kweli na lipi si sahihi?
  • La mwisho, kwa nini Familia ilitaka iwasiliane na Serikali kwanza kutangaza kifo cha mpendwa wao? kwa manufaa gani kama Ballali alishapoteza kazi yake na Serikali kudai haina taarifa au haijui Ballali yupo wapi? je kuna ukweli gani katika hili?
Kama nilivyosema awali, nimesikitishwa (saddened)na taarifa na kifo cha Ballali. naheshimu uamuzi wa familia na nawapa pole. Naheshimu uchu wa Watanzania kutaka kujua ukweli.

Nasikitika (disappointed) kuwa Ballai kaondoka na siri kubwa na hakuchuka fursa yeyote wakati akiwa hai (kama hakuwa anaishi katika vitisho na "kutekwa nyara") kutoa ushuhuda kuhusiana na kilichosababisha aidhinishe malipo makubwa ya EPA, CIS, Meremeta, Tangold ambayo yamegundulika kuwa yalikuwa ni batili na kwa makusudi ya kuhujumu uchumi na Taifa letu.

Waswahili wanasema, yaliyopita si ndwele, tugange kwa ya mbele. Katika sakata la EPA na BOT kutumika kuhujumu nchi, Ballali hakuwa Alpha na Omega, kifo chake hakijafunga au kusitisha uchunguzi.

Wale walio hai, Gray Mgonja, Basil Mramba na Ben Mkapa waje mbele na kutupa taarifa, ni vipi kulikuwa na upotevu, ufujaji na uhujumu mkubwa uliofanyika wakati wao wakiwa katika madaraka na kushikilia hazina ya Taifa? Ilikuwaje Ballali akaruhusiwa kuidhinisha malipo makubwa kiasi hicho bila kuchukuliwa hatua za kinidhamu na mkubwa wake wa kazi?

Rest in Peace Ballali. You will forever be remembered.

Rev. Kishoka,

Ya Balali yanatuhusu kwasababu ni mwizi wa mali ya Watanzania wote. Kufa kwake kunatunyima wote kama Watanzania nafasi ya kujua ukweli juu ya hawa mafisadi.

Pili, je ni nani hao wangemteka Ballali? Akina RO walikuwa wanajua yuko wapi, akina Mkono wanajua, ambao tulikuwa hatujui ni sisi walalahoi ambao ndio tungetaka ajibu mashitaka kwanza.

Siamini Ballali ni mjinga kiasi hicho, kama aligoma kabisa kuongea, basi hapo kuna siri kubwa ambayo yeye mwenyewe ni mhusika mkubwa. Yeye sio victim kwenye hili na badala yake ni among the main players.
 
Kwa ukawaida kama walivyosema waungwana wengi ni kwamba kama kweli familia nayo ilikuwa na nia nzuri..

Then wangetafuta msaada wa Watazania kwa wakati huu mgumu ili kuweza kuwin back sympathy!Ni wazi kuwa ndugu zake Ballali sympathy wanayotafuta ya kuimply kuwa Ballali alikuwa hapendwi na watawala kama ambapo dili nzima ianvyotakiwa ionekane!

Hapo ndugu zake wanajitoa nishai wenyewe kwasababu hapa marekani alikuwa na uhuru wa hata kuita press conference kwasababu alikuwa keshafutwa kazi na tuhuma zilikuwa juu yake kuwa anatafutwa!

Usanii mtupu!

Kama kweli alikuwa huru,mbona alikufa ghafla wakati makachero walipofika huku?

Yani ina maana kuwa alitaka afe akiwa huru?

Kwanini afe mara baada ya uhuru wake kukaribia kwisha?

Na kwanini serikali ilikuwa ikisubiri afe ili afe na uhuru wake na habari zake?

Kwani nani hajui kuwa kwasababu alikufa akiwa huru basi hata yale aliyoyaacha haywezi kutumiwa tena kama ushaidi?

Yani kweli huu usanii...Lakini nawakumbusha wanafamilia kuwa bado wana nafasi ya kufanya kitu ili kuondoa hili wingu zito la utata linaloikabili nchi yetu kwasasa
 
Daa!!!, hata wewe mushi tayari umeshagwaya? naoana umeshageuka do!!!!!, sijui tushike wapi, mnatuchandanya wakuu, jana ulikuwa umekaza kamba mara ulipotishwa tu, ooo!!!! chari,

Mambo mazuri hayataki papara!
Nakuhakikishia kuwa bado tuko pamoja!
Tutafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa watanzania wanapewa haki yao!
Naomba tu tuombeane uzima kwasababu issue hii si ndogo!
 
Kwasababu Ballali alikufa akiwa huru..Hata ushahidi wake anaodaiwa kuuacha hauna nguvu tena kwasababu alikufa kabla hajatuhumiwa!
Ushaidi wake unaweza ukawa batili na hivyo kesi yote kufa kwasababu ni ushahidi wa marehemu asiyekuwa mtuhumiwa!?! Au ni aliyekufa kabla ya kuwa mtuhumiwa ama aliyekufa kabla ya kutumiwa!
Hivyo kwa wale wanaosema changa la moto wana HOJA NZITO!
 
Sasa ushaidi wa ballali utatumika kama ushahidi wa mtuhumiwa ama wa marehemu huru aliyekufa akiwa huru na kuzikwa huru na kwa uhuru?
 
Marehemu atatuhumiwa vipi kama alikufa akiwa huru?
Akishazikwa ndugu zangu upelelezi utaanza upya!
Unless kuwe na ushahidi kamili kuwa huyu mtu huru aliyekufa masaa machache kabla ya kuwa mtuhumiwa ni kweli amekufa!
 
Kama ndugu wanavyogombana wakati wa misiba, wengine kudai wana haki zaidi kuamua Marehemu azikwe wapi, nani awe "mrithi" wa kutunza familia, nani agawiwe mali na majukumu mingine ambayo ni kawaida ya binadamu, Jumuiya yetu nayo iko katika mvutano huo huo.

Najiuliza je ni kawaida yetu binaadamu kuwa na mvutano kuhusiana na kifo na hasa wakati wa msiba? je hii ni ni kawaida wakati wa maombolezo?

Nimejiuliza ya fuatayo na maoni yangu binafsi na imani yangu pamoja na maswali haya ni kuwa Ballali hayupo nasi tena. I believe Daudi Ballali is dead and I pray that his sould rest in peace.

Maswali ni haya;
  • Je Ballali amekufa?
  • Ni nani ananufaika kwa kifo chake
  • Kama bado yupo hai na taarifa ya kifo ni ulaghai, ni kwa faida ya nani?
  • Je tuna haki gani kutaka kuingilia mambo ya binafsi ya familia?
  • Je kwa nini familia haitaki Ballali agwe na wananchi na kufanya msiba wake uwe jambo la familia tuu? ni wapi ule mshikamano wa kiafrika na utamaduni wetu?
  • Je ni kwa nini kumekuwa na usiri mkubwa kuhusu kuugua kwake na hata kifo chake? je mimi nina haki gani au wajibu gani kujua kuhusu Ballali? kwa nini kuna utata mkubwa katika kila kitu kuhusu Ballali?
  • Kifo chake ni pigo kwa nani?
  • Kama sababu za kifo chake ni kuuwawa kama wengi wetutunavyokisia, kudhania au kuzusha, je ni nani aliyetaka Ballali afe? Ni lini aliuawa? na ni nini kilitumika kumuua?
  • Ni siri gani ambayo amekufa nayo au kawapa familia, marafiki na wengine waitangaze?
  • Je kifo chake kina sehemu gani au mahusiano gani kuhusiana/katika uchunguzi wa tuhuma za ufujaji mali, uhujumu na ufisadi wa pesa za Taifa Benki Kuu?
  • Je kufa kwa Ballali kuna maafa gani katika vita ya ufisadi?
  • Je familia yake inaungana vipi wakati kuna mgawanyiko kati yao kuhusiana na mazingira mazima ya yeye kutuhumiwa, kuugua na sasa kufa?
  • Ni nani hao ambao wanatoa vitisho au wametoa vitisho na kutaka kila kitu kinachohusiana na Ballali kiendelee kuwa ama usiri, utata au mara nyingine kuwa ni uzushi? kwa faida gani? na ya nani?
  • Je alikufa lini na wapi?lipi ni kweli na lipi si sahihi?
  • La mwisho, kwa nini Familia ilitaka iwasiliane na Serikali kwanza kutangaza kifo cha mpendwa wao? kwa manufaa gani kama Ballali alishapoteza kazi yake na Serikali kudai haina taarifa au haijui Ballali yupo wapi? je kuna ukweli gani katika hili?
Kama nilivyosema awali, nimesikitishwa (saddened)na taarifa na kifo cha Ballali. naheshimu uamuzi wa familia na nawapa pole. Naheshimu uchu wa Watanzania kutaka kujua ukweli.

Nasikitika (disappointed) kuwa Ballai kaondoka na siri kubwa na hakuchuka fursa yeyote wakati akiwa hai (kama hakuwa anaishi katika vitisho na "kutekwa nyara") kutoa ushuhuda kuhusiana na kilichosababisha aidhinishe malipo makubwa ya EPA, CIS, Meremeta, Tangold ambayo yamegundulika kuwa yalikuwa ni batili na kwa makusudi ya kuhujumu uchumi na Taifa letu.

Waswahili wanasema, yaliyopita si ndwele, tugange kwa ya mbele. Katika sakata la EPA na BOT kutumika kuhujumu nchi, Ballali hakuwa Alpha na Omega, kifo chake hakijafunga au kusitisha uchunguzi.

Wale walio hai, Gray Mgonja, Basil Mramba na Ben Mkapa waje mbele na kutupa taarifa, ni vipi kulikuwa na upotevu, ufujaji na uhujumu mkubwa uliofanyika wakati wao wakiwa katika madaraka na kushikilia hazina ya Taifa? Ilikuwaje Ballali akaruhusiwa kuidhinisha malipo makubwa kiasi hicho bila kuchukuliwa hatua za kinidhamu na mkubwa wake wa kazi?

Rest in Peace Ballali. You will forever be remembered.

Tutakacho sikia baada ya hapa ni unafiki tu,ambao haujengi.tulikuwa na nafasi ya kujua kila kitu lakini hatukuitumia.hivi kesi ya ditto kwani bado hipo ?
 
jmushi1
Vipi mara rangi 2? ama power? ok ama na wewe umethibitisha kama kaanza? mimi bado ni utata, sijui, na tangu nimezaliwa sikuwahi kusikia mtu azikwa kwa faragha, marehemu siku zote hana kosa sasa iweje asirudishwe hapa home jamani? ndugu zake wote wanaishi Iringa, mashamba yake yale ya bunju yanatosha kumuhifadhi,hii ndiyo Tz
 
Tanzania tanzania, ...............
nilalapo nakuwaza wewe.............,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom